Ilipoishia sehemu iliyopita........
"Tarifa gani???"
"Inasemekana baada ya siku tatu Prince atatambulishwa mbele ya wananchi wote wa ADELI,Nzegi alimpata tarifa zile general".
"Hahahahahahahaha mda ambao nilikuwa nikiusuburi kwa miaka ishirini (20) sasa umewadia....
ENDELEA NAYO......
"Hahahahahahahaha mda ambao nilikuwa nikiusuburi kwa miaka ishirini (20) sasa umewadia"
"Unamaana gani General kuongea ivyo??"
"Nzegi wewe ni mlinzi wa mda mrefu katika jumba la kifalme unajua siku zenye matukio makubwa ulinzi huimalishwa sehemu moja tu katika ufalme wetu huu"
"Hahahaha nimekuelewa General nasijui kwanini sikufikilia hili mapema".
"Mda wangu wa kutoka gerezani umefika bora wangeniua tu kile kipindi ila kuniacha hai ni kosa ambalo hawatokuja kulisahau".
Ni mpango uliokuwepo kati ya General pamoja na mlinzi mkuu Nzegi na hii ni hatari sana kwa familia ya kifalme kama General akifanyikiwa kutoroka gerezani.
*****************
Familia ya Mfalme Kojo ikiwa katika meza ya chakula.
"Mtukufu mfalme nimesikia tarifa za kutambulishwa kwa Prince,tarifa hizi zinaukweli wowote baba??, Princess mkubwa aliye fahamika kwa jina la Yanite alimuuliza baba yake au Mfalme kojo"
Mfalme kojo hakuwa na la kujibu zaidi ya kumtazama na kumfanya Princess Yanite anyamaze kimya.
"Ata mimi pia nataman nimjue kaka yangu tuwe tunacheza wote, mtoto wa mwisho wa mfalme kojo aliyefahamika kama Princess Yanni aliongea"
Mfalme kojo hakutaka tena kuendelea kukaa katika meza ile ya chakula alinyenyuka na kuondoka na kuiacha familia yake katika meza ya chakula.
"Huwa nawambia siku zote mda wa kula hamtakiwi kuongea ovyo,Malikia aliongea kwa hasira"
"Lakini mama sinikweli hichi tulicho kizungumza??, Princess Yanite aliongea".
"Mda ukifika mtajua kila kitu".
Mfalme Kojo akiwa anatembea baada ya kutoka katika meza ya chakula alikumbuka kuwa anasiku tatu alizo ahidi za kumtambulisha Prince mbele ya halaiki,
Palepale aliamua kuita asikari wake anao waamini na kuwapa kazi kwenda nchi za mbali kumtafuta kijana atakaye kuja kuchukua nafasi ya Prince kwa mda mfupi.
"Nimewaamini nyinyi na ndio mana sitaki kumhusisha Mlinzi mkuu Nzegi hili swala ivyo nendeni mkatekeleza maagizo yangu na yoyote atakayevujisha izi tarifa kifo kinamhusu"
"Tumekuelewa mtukufu mfalme".
"Na ivi ni vipande vya dhahabu ambavyo mtampatia huyo kijana kama malipo yake ya mwanzo badae nitamumalizia malipo yake mengine baada ya kazi".
Asikari waliondoka katika jumba la kifalme na kutekeleza jukumu walilopewa na mfalme wao,
Pia walipewa barua maalumu yenye muhuri wa kifalme kama ishara ya popote pale watakapofika kwenye mipaka ya falme zingine waweze kuingia bira kuwa na kipingamizi.
********************
Ndani ya kijiji cha Nyengweli kilicho katika ufalme wa ADELI,
"Nashukuru sana kwa matibabu ya mjukuu wangu sikutegemea kama atarudi katika hali yake"
"Usijali babu ni kazi yetu kusaidia watu kwa kuwatibu,binti Amma alimjibu mzee yule"
"Naomba nishike mkono wako nikuangalie inaonekana ni mtu mwenye bahati sana".
Binti Amma alimpatia mkono mzee yule.
Palepale yule mzee alipiga magoti chini na kumfanya mjukuu wake kushangaa!!!.
"Babu unamatatizo gani????"
Mjukuu wake alimuuliza baada ya kuona babu yake amepiga magoti mbele ya binti Amma.
"Mimi sipaswi kusimama mbele ya mtu mkubwa katika ufalme huu wa ADELI nakuomba upige magoti mjukuu wangu utoe heshima juu ya huyu binti".
Maneno yale yalimtoa ndani baba yake na Amma baada ya kusikia mazungumzo ya yule mzee.
"Mzee wangu emu amka haina haja ya kupiga magoti"
"unabahati sana katika uzao wako".Mzee yule aliongea.
"unamaana gani kusema ivyo???".
"Yakupaswa uelewe tu unabahati katika uzao wako na pia nashukuru kwa matibabu ya mjukuu wangu na sina cha kuongea zaidi ila najivunia kuona mtu ambae sikutegemea kama ipo siku nitafanyikiwa ata kumshika kwenye maisha yangu"
Mzee yule aliongea na kuondoka zake pamoja na mjukuu wake aliyekwisha kutibiwa na kuwaacha Amma pamoja na baba yake katika maswali mengi yasiyo na majibu......ITAENDELEA.
Kwa sh 1000 tu unajipatia mwendelezo huu mpaka mwisho lipia sasa kwa NAMBA 0613083801 HALOPESA jina John Bugumba, kisha nitumie SMS ya malipo kwa njia ya whatsapp namba 0748697173 upate Full simulizi 🙏🙏🙏🙏🙏.
Kipi ambacho mzee huyu amekiona kwa binti Amma mpaka kupelekea kupiga magoto mbele yake na je? asikari waliotumwa na Mfalme Kojo watafanyikiwa kumpata kijana atakayechukua nafasi ya Prince Yao kqa mda mfupi????, tukutane sehemu inayofata..
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni