Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MIMBA YA BESTMAN 05

2nd Jun, 2025 Views 3

MIMBA YA BESTMAN 05

Mulky alikuwa anaumia sana na hakuweza kumueleza yoyote kile anachokiita ndani ya ndoa yake.

Kuanzia hapo Yasini aliamua kutumia ukali kama siraha alitaka kumfanya mulky amuogope ili aache kumsumbua kudai haki yake ya ndoa.
Njia yake ilifanikiwa mulky hakuwa alimuongelesha tena kuhusu swala la unyumba aliamua kuishi kama pambo ndani ya nyumba na kuonekana mke mwenye furaha ndani ya ndoa yake mpaka ikafikia baadhi ya ndugu na marafiki kumuonea wivu na kumsifia kuwa kapata mume bora ambae anamjali na kumpatia kila anachotaka , Mulky alitamani kusema kitu lakini alipokumbuka kauli ya Yasini ya kuwa endapo atasikia popote atakiacha nae aliamini swala la mwanamke kuachwa talaka tatu ni jambo la aibu na hakuanini kama akisema kuna ambae atamuamini kuwa anapitia hayo.

Mulky aliendelea kuvumilia kwenye ndoa yake huku akiwa anatamani kuomba ushauri hata kwa rafiki lakini akaogopa kutoa siri za ndani ya ndoa yake.
" Itakuwaje kama nikasema nje na taarifa zikisambaa si nitaonekana mimi ni mwanamke wa ajabu nimeshindwa kustiri aibu ya mume wangu.
Wakati Mulky anawaza hayo alikuwa jikoni anaandaa chakula.
Hatimae alizama kwenye dimbwi la mawazo akajisahau kabisa kama anapika Alikuja kushituka baada ya Yasini kufika pale jikoni na kuzima jiko.
" Yani upo hapa na bado unaunguza chakula?
Aliuliza Yasini huku akiwa anamuangalia usoni na Mulky alikuwa kaduwaa anamuangalia tu
" Naongea na wewe una matatizo gani?
" Nilipitiwa . Alijibu mulky huku akishika sufuria iliyobandikwa jikoni kwa mkono , mara aliachia ile sufuria baada ya kuungua.
" Una matatizo gani wewe kwahi hujui kuwa hiyo sufulia niya moto unashika bila chochote.
Mulky alinyamaza kimnya akawa anaangalia mkono wake ulipungua huku akipuliza.
Yasini alimuangalia mulky akahisi kumuonea huruma alitambua kile anachofanya ndicho kinachomfanya awe kwenye ile hali.
" Inawezekana haya yote anayopitia yanatokana na mimi? Sasa nitafanya nini sijui ni mpe talaka ili awe na amani mmmmh hicho kitu haliwezekani nampenda sana mke wangu naamini ipo siku mulky wangu atakuja kuwa na furaha , uwanaume wangu utarudi nitahangaika na kutafuta tiba mpaka hali yangu itakapokuwa sawa .

Yasini alisogea karibu zaidi alafu alinyoosha mkono wake na kuushika mkono wa Mulky iliokuwa umeungua, aliangalia sehemu aliyofungua ilikuwa nyekundu.
" Pole.
" Asante
" Twende nikakupake dawa.
" Haina haja nitakuwa sawa.
" Acha ubishi umeungua sana.
Mulky alikubali kwenda kupakwa dawa alipomaliza alinyanyuka na kurudi jikoni, alichukua sufuria nyingine akaweka jikoni ili apikee chakula kingine maana kile cha mwanzo liliungua kikawa hakifai.

Yasini alimfuata jikoni akazima jiko alafu wote wakawa wanaangaliana.
" Haina haja ya kupika chakula kingine nenda ndani kajiandae tutoke.
Mulky hakuongea neno alitoka jikoni akaenda chumbani akajiandaa kavalia nguo yake nzuri akapendeza .
Ni kawaida sana kwa Mulky kupendeza kutokana na uzuri wake kila nguo aliyovaa ilimtoa bomba pia umbo lake zuri ilichangia nguo
kumkaa vizuri.

Yasini alimuangalia mke wake alivyokuwa alimfuata kwa mwendo wa Madaha akajikuta anaachia tabasamu kwa mbali lakini alipokumbuka kuwa ndoa yao haina amani tena kwa sababu yake lile tabasamu lilifutika. Alienda kufungulia mlango wa gari , mulky alipanda nae akaenda kupanda na kuwasha gari.
" Unapenda twende wapi tukapata chakula cha usiku? Aliuliza Yasini.
" Popote kwangu ni sawa.
Aliongea Mulky huku akiangalia mbele bila kumuangalia Yasini.
" vipi maumivu ya ulipopata jeraha?
" Yamepungua.
Baada ya hapo kimnya ilitawala walifika hotelini wakaagiza vyakula wakawa wanakula kila mmoja akiwa kimnya.
Yasini aliamua kuvunja ukimya.
" Mke wangu najua na kunyima raha na unaniona kama mtu mwenye roho mbaya sana kwako.
Yasini aliweka kituo akitegemea mulky ataongeza chochote lakini haikuwa kama alivyotegemea mulky alikuwa kimnya.
Yasini alinyoosha mkono wake na kuushika kiganja cha Mulki ambacho kilikuwa juu ya meza.
" Naomba izidi kunivumilia ipo siku itasahau haya yote tunayopitia kwa sasa.
" Nashindwa kukuelewa huniqwki wazi kama kuna tatizo ungeniambia ili tuhangaike pamoja.
" Aaaaaah usijali mke wangu muhimu kinacho hitajika niusiri na uvumilivu wako.

Kwa mara nyingine tena mulky alimuelewa mume wake alidhia kuwa na Subra mpaka mume wake atakapokuwa sawa japokuwa hakujua nini kinamsibu mpaka inashindwa kuwa kama wanaume wenzake wanaosimamia ndoa zao vyema .

Siku moja Mulky alienda saloon akiwa na gari mpya , wenzake walivyomuona walianza kumsifia.
" Mulky wewe sio mwenzetu maisha imeyapata hongera shoga yangu.
" Mmeanza maneno yenu kwanza msije kunipiga kijicho.
" Kwa kweli hapa hakuna mwenye kijicho tunakutana tangia miaka na hakuna aliemuwekea mwenzie kijicho.
" Nilikuwa na tabia mashoga zangu. Tayana hebu nitangenezee nywele zangu.
Alisema mulky huku akiwa anakaa kwenye kiti tayari kwaajili ya kupata huduma.

Story ziliendelea huku mulky na wenzake wakiendelea kupata huduma .
" Hamida mbona umekaa huko huishi nywele zako?
Mulky walimuuliza mmoja wa mashoga zake.
" Sina hela shoga yangu nimekuja kutengeneza kucha tu.
" Nywele zipo rafu sana hizo hebu tuongee huruma.
" Sasa sina hela nafanyaje?
" Nitalipa.
" Huo upendeleo mulky hata mimi utanilipia.
Alisema mwajuma.
" Hakuna shida .

Mwajuma na Hamida walifurahia ofa waliyopewa na kumuombea dua kedekede.
" Mwenyezi Mungu akujaalie kizazi chema.
" Uzao wako uwe mapacha.
" Na ndoa yake iwe yenye baraka na upate kila anachokitaka kutoka kwa mume wako.
Badala ya kufurahia dua alijikuta ananyongonyea alikuwa kashajikatoa tamaa kama ipo siku atamzalia mume wake na kupata furaha ya ndoa kama wengine.

Itaendeleaaaaa

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest