Shahidi alinyamaza kidogo.
Nilmekuuliza nataka jibu Shahid.
Mama naomba kesho nije tuongee kwenye simu hatutaelewana.
Nataka kesho mapema kabisa uje, yani kabla haujaenda kazini. Baba yako anahitaji kujua hili kwa kina
Sawa mama. Shahid alikata simu na kuendelea kucheza na Shania.
Kesho yake Shahid aliamka mapema sana huku Shania akiwa Kalala pembeni Akimuangalia na kujisemea. yake
Hakuna mtu wa kuvunja upendo wetu Shania, nitapambana, nitakupigania wewe na mtoto wangu sitakubali uwende mbali na mimi.
Baada ya kufikiria alinyanyuka akaenda jikoni, alimkuta Tessy anaanza kufanya usafi.
*Habari Tessy.
*Salama baba kijacho mmeamkaje?
Shahidi alitabasamu
Salama, vipi umeandaa kifungua kinywa?
Bado nafanya kwanza usafi ndipo niandae.
Achana na mambo ya usafi nilikwambia
ukitamka tu anza kuandaa kifungua kinywa
unajua Shania huwa anaamka na njaa sana.
Sawa Boss naandaa sasa hivi. *Fanya haraka tafadhali.
Sawa.
Ilipofika Mida ya saa tano Shahid aliondoka na kuelekea nyumbani kwao kwaajili ya kuongea na
wazazi wake.
Alifika nyumbani kwao na kusalimiana nao baada ya hapo kikao kilianza.
Shahid kuna kitu gani cha ajabu umefanya ? Mama yake aliuliza.
"Hakuna kitu cha ajabu nilichofanya.
Kwahiyo unataka kusema kuishi na kichaa ni
kitu cha kawaida? Baba yake alidakia.
Wazazi wangu naombeni mnipe muda kidogo. niweze kujielezea.
*Utatuambia nini tukuelewe wakati unatusibisha
na kushusha heshima yetu? *Sio kweli wazazi wangu kumbukeni hata kichaa
nae ni mtu anatakiwa kupendwa na
kuthaminiwa. *Toa maneno yako ya kipuuzi hapa huyo kichaa
wako sitaki kumsikia. Mtanisamehe wazazi wangu nampenda sana
Shania na yeye ni mama wa mtoto wangu anayetarajiwa kuzaliwa mwezi ujao tu. Shahid mwanangu hivi kwa wadhifa wako ni
wakiwa na mwanamke kichaa kweli? Mama nilipokuwa na Aisha ulikuwa uliniambia ni mwanamke jeuri, hana heshima, ufujaji wa
pesa hafikirli maendeleo yeye ni anasa na starehe. Na mimi niliona hilo na nikakubali tabia
zake japo kuwa nilikuwa nakupa muda nikidhani atabadilika lakini kabla sijasikia nilipokuwa natarajia kufika ikatokea bahati mbaya kwa
Shania na akapata ujauzito.
*Hivi mwanangu watu si watasema Ulimboka kichaa kwasababu ya kupata pesa. *Wacha waseme mama ukweli najua mimi.
*Sisi hatumtaki.
"Wazazi wangu siwezi kumuacha.
Sikiliza wewe kama huwezi kumuacha huyo
kichaa wako basi hatutafikia kwako. Aliongea baba yao kwa hasira kisha akanyanyuka na
kuingia ndani.
Shahidi umeona baba yako kakasirika shauri yako upate radhi ya baba yako.
*Mama hakuna radhi ya aina hiyo.
Sasa kaa na ubishi wako litakalo tokea na huyo kichaa wako sisi hatupo. Ngoja siku moja ukiwa
usingizini akunyonge mpaka ufe.
Shania ni kichaa kweli lakini sio mkorofi. Hakuna kichaa ambae sio mkorofi nyie ndio
wale mnaambiwa mke wako kipofu unasema hapana ni chongo, sasa endelea kumlea huyo chizi wako likikukuta ndio utaelewa tulikuwa tunaongea nini.
*Lakini atakuwa mama wa mtoto wangu. Hiyo sio sababu ya wewe kung'ang'ania nae akijifungua tunamnyang'anya mtoto
anaenda zake mtaani.
Haiwezekani hatuwezi kufanya dhuruma atamlea mtoto wake kwanza vichaa wanajua
malezi.
"Eeeee... Sasa kaa na ujinga wako pumbavu. Mama yake pia aliondoka na kumuacha akiwa amekaa.
Shahidi alikaa kwa muda huku akiwa anafikiria ni
jinsi gani atamsaidia Shania na kurudi kwenye hali ya kawaida maana maneno ya wazazi wake yalimuumiza sana alipamani kuibuka mshindi
kwenye swala la Shania. Baada ya muda alinyanyuka akaenda kupanda kwenye gari lake na kuondoka.
Alielekea moja kwa moja kwa shangazi yake Shania.
Shikamoo shangazi.
*Marahaba. Shahidi kuna usalama kweli, mbona asubuhi asubuhi?
Ni salama shangazi ila kuna baadhi ya mambo kuhusu Shania nataka kuyajua ili yaweze
kuwawakilisha kwa daktari kabla ya kuanza matibabu yake.
Eheee unataka kujua nini?
*Kuna sababu iliyosababisha Shania kuwa vile? Ndio kuna sababu iliyofanya Shania kuchanganyikiwa na kuwa kichaa.
Itaendelea....
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments