Nilimjibu tu ungekuwa wakupeleka ungeshapeleka, kama uliweza kunibaka bila ridhaa yangu, hio mahali inasubili ruhusa yangu kivipi, Albert aliuza tu " unamaanisha unachokiongea?, sikujibu nilimpushi nikaenda zangu kulala, nilisema nijiegeshe nikiamka napika tu cha usiku tunalala,lakini uchovu ukafanya nikaamka saa 4 usiku, nikakuta Albert ameshapika, nilimshukuru tu make dah, alinikaribisha nikashangaa mmh, nilikaa tukala, nikamuuliza inamaana ulikuwa unanisubiri? " Ndio kuna kazi hapa pia nilikuwa naifanya nikaona nitumie muda huo kusubiri uamke, kwa sababu pia nina hitaji tu kukuomba utoe taarifa kwenu, kesho kutwa napeleka mahali, nimeshaongea na mzee kesho anakuja ili kesho kutwa tupeleke, nilimtizama kama sijamwelewa, nikakausha ata sikupiga simu nilikumbuka kuna jirani yangu, alidanganywa na bwana ake wakajipanga bwana anakuja kutoa mahali, na apo kishka uchumba alishatoa, apo ilihitajika tu mahali, wazazi wake wamepika wameita ndugu baadhi na majirani muhimu,mwanaume imefika jioni kazima simu mazima mpaka saa tatu usiku, anakuja kuona tu mashemeji wanapost kumpongeza mwamba kamvisha mtu mwingine tena pete ya uchumba ni picha tu zinasambaa, aibu aliyoipata na kawaingiza wazazi wake kwenye gharama za kupika yani heeeπ...
Nikajiongeza yasijekunitokea puani acha niendelee na mambo mengine sikumuamini yeye alijua nimemuelewa, make sikujibu chochote, kesho yake aliniaga anaenda kumpokea mzee wake, atamleta tusalimiane afu atampeleka kwingine kulala, nikajua ehee inamaana anamtu apa mimi ni kwakuwa tu nimezaa nae, sikuuliza apo nilikuwa najipa majibu kichwani...
Niliewa pesa ya maandalizi nyumbani, lakini sikuifanyia chochote, niliendelea tu na mambo yangu, mzee alikuja nilikuwa tayari nimepika, nilimsalimia vizuri kabisa, nikatambulishwa na akapewa pia taarifa kuwa kuna B, alifurahi mzee alitamani kumuona, akaambiwa yuko kwa bibi yake, walimaliza wakaondoka,Albert akaniambia niende nikalale nyumbani kwetu yeye harudi nikajua yale yalee,atasikujisumbua, ila nilikuwa nimemmis mwanangu, nikaamua tu nikamchukue kulala peke yangu ngumu, nilienda, mpaka nyumbani, mama akagoma usiku umeingia, hatuwezi kuondoka nilale, afu kesho mdogo wangu anatolewa mahali nisaidie kupika, nilikubali last born wetu alikuwa anaolewa...
Niliamka asubuhi tukaanza pilika pilika, mpaka saa sita ivi tukaoga kusubili wageni, B akaanza kumuulizia baba ake, mama akasema tena ngoja hili liishe unipe maelezo yakinifu, nikajua kabisa mwanangu kashatoa ubuyu kwa bibi yake, mda huo wote, toka kumekucha Albert hakuwa amenitafuta hata kunijulia hali, nikajua kabisa nilichokuwa nakiwaza ni sahihi..
Nikapotezea tu make nishazoea, mimi ni wa hivi hivi, mida ya saa saba nikiwa zangu chumbani, nikasikia mama anakuja kama kavurugwa, akanitizama kama ananishangaa "wewe mama B kwa nini hukusema kama unaugeni? Nikashangaa unasemaje mama? Inamaana hukuwa unajua kama Baba B anakuja utupe taarifa, ndo nikashtuka mmh mama kwani kaja? "Ivi unauliza ujinga gani? Kwa hio ulikuwa unajua kabisa anakuja ila ukaamua tu leo tupate aibu, isingekuwa mdogo wako kuandaa kwa ajili ya wageni wake leo tungeweka wapi sura zetu?...
Mama mimi nilijua anatania hamaanishi sikutegemea kama atakuja kweli, "yani wewe mtoto π, alitoka mama akaja na kuomba nisitoke mpaka niitwe na hio nguo haifai akampigia mdogo wangu Judith akamueleza, alikuwa kaenda kuchukua vinywaji, akamwambia anichukulie nguo, make nipo nipo tu, kwanza adi yeye akashangaa, ikabidi tu wanichukulie nguo ikawahishwa na ilinitoa vibaya mno, utazani nilijiandaa kumbe siri yangu na familia...
Wageni wa mdogo wangu pia walifika ikabidi tuwachamganye tu, na kutoa utambulisho, kisha tukaitwa mimi na mdogo wangu, nilikiwa na kitete sio poa kwanza sikuamini kama ndo naposwa kweli ama naota jamani, Albert alitozwa adi faini na akalipa, aisee nilitamani ata kulia, kiutani utani ety na mimi naolewa, nilitamani ata nipige kelele kwa nguvu...
Nilikuwa na furaha sio poa, kila kitu kilikaa sawa, nikapewa muda wa kuongea na mwenzangu pembeni, nilijikuta tu cha kwanza namkumbatia uku nalia kimya kimya, alinikumbatia pia, apo hakujua kama nalia, alitaka kunitoa nikagoma, ikabidi aniache nilidhike kwanza, nikajifuta machozi ili asijue kama nilikuwa nalia, ila macho yaliniumbua, akaniuliza tu " ulihisi sitokuja? Niliinama tu macho chini, sikujibu alijiongeza mwenyewe, akasema " Joy nakupenda nisingeweza kupindua nakuhitaji wewe na mtoto wetu...
Itaendelea...π₯
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments