Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

SIKUJUA LECTURER NI MJEDA 8

13th Sep, 2025 Views 42



Nikiwa pale nikaanza kuhisi kama kuna mtu ananiangalia sana, ila kiukweli sikumzingatia maana kwanza sikuwa nahisi kama kuna mtu ambae ananijua eneo lile, sasa inakuwaje mpaka mtu awe ananiangalia na hanijui hata kidogo...
Nikageuka ila sikumuona vzr hivyo nikapuuza zangu nikaendelea na mambo yangu, basi kuna muda akaja mkaka akakaa pemben yangu, nikashangaa namba ngeni inaingia kwenye simu yangu na kusema "upo wapi?..
Sikujibu maana nilihisi mtu kakosea namba..
Mara nikaona sms nyingine inasema "sophy upo wapi?..
Nikaona sasa huyu ananijua..
Nikauliza "nani mwenzangu?....
"Jibu kwanza swali kabla ya kuuliza swali lingine, nakuuliza upo wapi?..
"Siwez kumjibu mtu nisie mjua mimi, nikajibu..

Nikawa nimekaa zangu, mara yule kaka akanisogelea na kusema " dada mambo..

Nikamuangalia kwa sura ya bashasha na kujibu "poa..
"Mbona haujaagiza chakula bana, muhudumu mletee huyu kuku nusu na chips, kisha akanigeukia na kusema " hupaswi kuja sehemu kama hii na usiagize kitu cha kueleweka..

Sikuwa na chakusema zaidi ya kusema "asante..
Kweli baada ya muda mchache akaja muhudum na kuniwekea ile chips kuku, nikachukua umma ili nianze kula, ila hata kabla sijaanza kula nikashangaa mtu kakaa pemben yetu,kisha akavuta ile sahani na kuanza kula yeye, si ndio nikasema nimuangalia nashangaa namuona kelvin...

Yule mwanaume akataka kuleta vurugu, aisee alimuweka kofi moja kisha akamuambia " sio kila mwanamke unaemuona unahisi ni chagudoa yupo mawindon, wengine wapo na watu wao hivyo jiepushe na mademu wa watu, kisha akakaa na kuendelea kula na yule mwnaaume akawa analalamika, ila kelvin akawa hata hashughulik nae, akala kwa hasira sana, yaan alikuwa anafakamia kana kwamba hakuwa amekula siku kadhaa, au ameona chakula ambacho alikuwa anakitaman muda mrefu, na baada ya kumaliza kula akanishika mkono na kuanza kunikokota...

“ unanipeleka wapi wewe, naomba uniachie, nikaanza kulalamika, akili yangu ikanituma kuwa huenda anataka kwenda kuniingilia bila ridhaa yangu tena, na sikutaka kitu kama hicho kitokee kwenye maisha yangu kwa mara nyingine tena…
“ nitapiga kelele kuwa unaniteka, nikaanza kusema…
Kelvin akasimama kisha akacheka sana, na kunibeba taksi bega na kusema “ haya anza kupiga kelele sasa, maana nitaonekana kabisa nakuteka kwa ushahidi, nikaona sasa hichi kichwa sicho kabisa….

Akanipeleka kwenye gari kisha akaanza kuliendesha kwa fujo, nikaanza kupiga kelele na kulalamika na kusema “ naomba unishushe kelvin niamb ie unanipeleka wapi, ila hata hakuwa ananijibu akawa anaendelea kuendesha zake gari kana kwamba hakuwa ananisikia kabisa yaan…
Alipoona nimezidisha usumbufu akasimamisha gatri na kusema “ unapenda sana offer si ndio, embu nambie ni offer gani nyingine unayoipenda nijue kabisa…
“ nipende offer nisipende offer inakuhusu nini, yaan wewe ni mwanaume wa ajabu ambae unapenda kulazimisha mambo kama mwenda wazimu vile, yaan sijui kwanini mungu kanikutanisha na shetani wa mguu mmoja mimi..
Kelvin akapanic kutokana na maneno yangu sasa, akawa anataka kuniweka kibao, niliogopa maana sikujua kama anaweza kunipiga, nikajikuta nimeweka sura ya huruma, aliponiona ni kama mawazo ya kunipiga yakabadilika na kuanza kuniangalia sasa, ghafla akanikiss kwenye lips zangu na kusema “ usije ukarudia kuniangalia hivyo tena, maana nitakukula siku nzima, ikabidi nipoe na kiburi na maneno yote ya ajabu niyaweke mfukoni maana akili za kelvin hazijawah kutabirika hata mara moja….

ITAENDELEA

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIKUJUA LECTURER NI MJEDA 8  >>> https://gonga94.com/semajambo/sikujua-lecturer-ni-mjeda-8

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest