Siku zilizidi kusogea na miezi lilizidi kwenda mbele. Siku moja majira ya saa saba mchana jua kali lilikuwa linawaka, Shahid alikuwa kwenye gari na Aisha walikuwa wanaenda sehemu mara ghafla Shahid alihisi kama kumuona Shania. Aliangalia kwa makini aligundua kwa ni yeye na wakazi huo Shania alikuwa na tumbo kubwa, alikuwa kachoka alitembea huku akiwa anavuta
miguu na mdoli wake alikuwa kuning'iniza.
Shania. Shahid alijikuta kuongea kwa mshangao huku macho yake yakiwa yanaangukia nje kupitia dirishani na huku akiendesha gari kwa mwendo mdogo mdogo. Aisha alikuwa amesikia na akawa makini
kuangalia kule alikokuwa anaangalia Shahid
aligundua kuwa huyo Shania ni yule mwanamke
kichaa.
"Shahidi huyo Shania ni yule kichaa? Shahidi alitaka kumuangalia na hakuona haja ya kumficha.
"Ndio.
"Kuna kitu gani au kuna siri gani unaendelea kati yako na huyo mwanamke kichaa? "Alijitolea sana na nilikuwa nampa chakula mara
kwa mara. Aisha alijikuta moyo wake unatilia na kucheka
kidogo. Alseee kumbe sikuwa na haja ya kulibeba hili kumbe mtu mwenyewe ni kichaa. Shahid alimkata jicho kisha akaendelea
kuendesha gari lakini akili yake haikuwa sawa kumuona Shania akiwa kwenye hali ile kulizua maswali mengi kichwani kwake..
Kuanzia siku hiyo shahidi alitamani kuwa mwenyewe alimwambia Aisha aende kwao kwanza anataka kusafiri kikazi. Siku iliyofuata Aisha aliondoka akarudi kwao na
shahid alipata muda mzuri wa kutafakari mambo yake bila kuchanganywa na maneno. Alianza kufuatilia kuhusu Shania
Siku moja akiwa sehemu alimuona Shania anagombana huku akimtishia mawe kijana mmoja. Ilibidi shahidi aende kujua nini kimetokea Shania alipomuona alianza kulia akamfuata na kumkumbatia "Nini kinaendelea hapa? Shahidi aliuliza watu
waliokuwepo karibu huku Shania akiwa bado kamkumbatia. Yule kijana alikuwa anamtania anakuita
mchumba. "Huyu kichaa huwa hapendi utani na wanaume. Shahid alimbembeleza baada ya hapo
alimchukua wakaenda kukaa sehemu. Shahidi Alimuangalia jinsi alivyokuwa kachoka na lile tumbo lake
Mungu wangu hii mimba inaweza kuwa ni mimba yangu. Alijisemea shahidi Shania alikuwa anamuangalia tu.
"Nataka embe.
"Sawa naenda kukununulia.
Nataka na juice. Shahidi alimuangalia na kuachia tabasamu.
"Njaa ina kuuma? Alimuuliza na Shania akitikisa kwa kichwa. "Sawa subiri kidogo utakula.
Shahidi aliemuacha pale akaenda kutafuta chakula na baada ya dakika chache alirudi akampatia chakula na Shania akaanza kula. Shahidi alikuwa akimuangalia mpaka alipimaliza kula alimshika mkono wakafika upande wa pili wa barabara wakaenda sehemu wanayouza matunda akamnunulia matunda akawekwa kwenye mfuko. Shania sasa nenda nyumbani ulale haya matunda.
"Haya. Shania aliitikia kisha akaondoka huku shahidi akiwa kasimama akimsindikiza kwa macho.
"Kweli damu zenu zinaendana huyu binti hana
ukaribu na mwanaume yoyote na huwa anakuwa mkali sana yani na watu wanajiuliza hiyo mimba kaipataje na huyo mwanaume alimshawishi vipi mpaka akafanikiwa kumvua chup. Mama muuza matunda aliongea, shahidi alinyamaza kimnywa, Shahidi akilipa hela ya matunda kisha akaondoka kwenda kupanda kwenye gari lake.
Kumbe wakati akiwa amekaa na Shania akiwa anakula Rashidi alikuwa amewaona mpaka walipovuka barabara na kunukia matunda pia aliona.
Shahidi alipokuwa anaendesha gari kuelekea nyumbani kwake Rashidi nae alikuwa akiendesha gari kumfuata nyuma.
Shahidi alipoingia tu ndani na Rashidi nae alifika. "Vipi? "Safi, nataka tuongee.
"Sawa,
"Shahid unahusiana vipi na mimba ya yule kichaa? "Unasemaje?
"Nauliza wewe ndio muhusika wa ile mimba ya yule kichaa?
Hili swali lilikuwa gumu kwa shahidi kujibu moja kwa moja alisimama na kumtolea macho Rashidi.
"Ukimnya wako ni jibu Shahid, unamaana ni kweli yake nilivyosikia? Bado Shahid alikuwa kimnya.
Unaleta albu gani kwenye familia? Hujui kama hii ni kadhia mbaya sana na vipi kama Aisha mpenzi wako akijua unaenda kuwa na mtoto na
kichaa?
Anaitwa Shania na usimuhukumu kutokana na matatizo yake. Yule ni mwanamke na anahaki ya kupendwa kama wanawake wengine. "MUNGU WANGU hiki ninachokisikia kutoka kwako ni kweli ama naota ndoto za mchana?
"Kama unaota basi amka, amka kaka yangu Rashidi na usikie ukiwa unajielewa. "Daaaah hii kali ya mwaka aiseee sikutegemea
kusikia hili kutoka kwako yani kwa jinsi ulivyo wala hauendani na matendo umayofanya kwanza ulianzaje kulala na mtu wa aina ile? "Ni kama wewe unavyofanya tu. "Hahahaha huna kinyaa wewe?
Wakuona kinyaa. ni wewe ambae unawabadilisha ila kwangu ilikuwa burudani tu na tamu kupita maelezo.
Shahidi walimaliza kuongea kisha akaelekea chumbani kwake. Rashidi alibaki kasimama na kusema.
"Hii ni aibu ya mwaka bora kunyamaza
nimuachie mwenyewe. Ila nae anatakiwa kupimwa akili yake huenda kaambukizwa uchizi au ndio tuchukulie ule msemo ukikaa na waridi lazima unukle sasa yeye anapata uchizi.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments