Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

*UDHAIFU WA MR CEO _____________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA* Basi ndio rasmi tukaanzisha mahusiano na my wangu

14th Sep, 2025 Views 107

, na alikuwa ananipenda sana na alikuwa hataki kukaa mbali na mimi kwa namna yoyote ile, na bahati nzuri umaridadi na uhidar wa kazi zake ukawa unazidi kwa mimi kuwa pemben yake, siku moja nikamuuliza ilikuwa je mpaka katika hali kama ile..

Akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema cha msingi ni wewe kuwa karibu yangu na habari zangu hazikuhusu..

Nilijisikia vibaya sana kwa jibu lake, ila sikutaka kuonyesha ghadhabu zangu, nikataka ajue kuwa nipo sawa, nikaanza kufuatilia sana kuwa anashida gani, maana hio hali aliyo nayo sio hali ya kawaida kabisa, ni lazima kuna story huko nyuma na nahisi huenda ikawa sio simulizi nzuri, Ila hakuwa ananipa ushirikiano kwenye majibu ndio changamoto..

Basi nikawa nachunguza sana, mpaka siku moja nikaja kufatwa na mwanaume mmoja, kwa kumuambgalia utajua anaweza kuwa zaidi ya miaka hamsini, akaniuliza kuwa wewe ndio shimena..

ndio nani mwenzangu? Na mimi ikabidi nimuulize yeye..

Akacheka kidogo kisha akanambia kuwa yeye ni baba yake na Edward, nilishtuka sana, maana kuanzia nimemjua Edward sijawah kuhisi kama anamzazi, maana alikuwa anaishi maisha ya kipweke sana kuliko kawaida, kana kwamba alikuwa ni mtoto yatima asiekuwa na wazaz wala walezi, au mwanaume ambae aliachwa na mwanamke ambae alikuwa anampenda sana...

najua unataka kujua taarifa za Edward akasema na kweli nilimuangalia kwa shauku kubwa sana maana ni kweli nilitaka kujua ni kwanini alikuwa alikuwa kwenye hali ambayo alikuwa nayo wakati ule....

Akanambia kuwa hio cd ina kila kitu kumuhusu Edward ila kabla sijapokea nikashangaa imepokelewa na mtu nyuma yangu, nakuja kugeuka nashangaa nakutana uso kwa uso na Edward kiukweli nilishtuka sana, akaichukua ile flash kisha akasema " mzee nilishasema kuwa sitaki kuwa karibu na wewe hata kidogo, kwanini umekuja kunifata kwenye maisha yangu tena, unataka nini, mbona nimekuacha na maisha yako, mbona mimi najua siri zako na nimetulia tu kama sipo, unafikiri kwa ulichomfanyia mkeo na mwanao watu wakijua wataendelea kukuona kama kiongozi wao au ndio watakuuwa mara moja, naomba uachane na mimi na ukae mbali na mwanamke wangu, na ukae mbali na maisha yangu...

Kisha akanishika mkono akaanza kunikokota, tulipotoka nje akaniachia kisha akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akanikumbatia kwa nguvu kwa karibu dakika mbili bila kusema neno lolote lile, kisha akanambia

nimeogopa sana ulipokuwa umekaa na baba yangu..

Basi akajitoa kwenye kumbato na kusema " hata kama kukiwa na shida gani naomba usije ukawaza kuniacha mamaa, wewe ndio kila kitu kwenye maisha yangu kwa sasa hivi, naomba usije ukawaza kukaa mbali na mimi, utaniua...

Nilimuonea huruma sana na kuendelea kumuahidi kama ambavyo huwa namuahidi kila siku kuhusu kuwa karibu nae kwa wakati wote basi akanielewa na kuwasha gari, na tukaanza kwenda kwenye mgahawa flani, tukala ila wakati wote huo Edward alikuwa kimya, na mara baada yua kumaliza kula akataka twende nyumba hata sikubisha, tukaanza kuondoka kuelekea nyumban, akaleta na popcorn kisha akanambia kuwa ana simulizi anataka kunipigia, basi nikaweka maskio yangu juu juu kama ungo nikaanza kumsikiliza...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*UDHAIFU WA MR CEO _____________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA* Basi ndio rasmi tukaanzisha mahusiano na my wangu  >>> https://gonga94.com/semajambo/udhaifu-wa-mr-ceo-_____________________________________-sehemu-ya-kumi-na-moja-basi-ndio-rasmi-tukaa

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest