Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

WAKILI HUCHOKI JAMANI 🫣* *______________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA SITA*

12th Sep, 2025 Views 106



Albert unasemaje? "Mama mimi tayari ninamke na mtoto yani kifupi ni mme wa mtu, sasa huyu mimi nampeleka wapi? " Albert usinichanganye we mtoto, yani umeoa mimi sijui, afu unatamba unamwanamke mimi huyo simtambui ninaemtambua ni huyu aliekuja mpaka kwangu akatambua umuhimu wa mama, "sasa mama hata ukimtambia inasaidia nini mwenzie ana uhali wa kisheria na moyo wangu pia aya uyo mbona mnataka kunichumia dhambi za bure, kwanza nilishagundua muda tu kama uyu mwanamke ni kibaraka wako ndo nikazidi kumchukia kwanza sio type yangu...

Pili hana akili, zipo za darasani tu ila kuhusi maisha ni sifuri, uyu acherewi kutoa siri za ndani nje, kupika hajui, yani yupo yupo tu, kitandani kwenyewe hajui step anakatika ovyo ovyo tu utadhani tyre ya pancha, hajui nafasi ya mwanaume kitandani hadi nje,naoa napeleka wapi? Au ndo kunifanya niwe nachit kila siku? " Mama angu nakuheshimu sana ila naomba uadui wako na mme wako mimi usinihusishe na usinieleze kabisa kama kweli ni mbaya kiasi hicho ulikuwa na muda wa kuachana nae mbona mpaka leo mpo pamoja na kumpa unampa?..

Mama kumbuka sisi ni wanao, izo chuki unazotupandikiza zinamadhara makubwa kwetu, tukipata laana ya mzee, unazani maisha yetu yatakuwaje, huhitaji tumhudumie, ilihali yeye alituhudumia ata kama nikwa uchache lakini alitoa, mama hukua na kazi wala biashara, kuvaa ata kama ni nguo mbili kwa mwaka alikuwa ni huyo huyo unaemsema, hatukuwahi kulala njaa japo kuna muda tulinusurika ulienda kukopa mara kadhaa tukala hilo ni jukumu lako kama msaidizi usilichukulie hatia kwa sababu alipopata mzee si alilipa ayo madeni?..

Najua hata yeye anamengi ila kwa sababu anajua nafasi yake kakaa kimya kutulinda sisi na kulinda heshima yako, mama najua kila kitu saiv sitaki tu kukutia aibu mbele ya mpambe wako nimebadilika baada ya kujua wewe na baba ugomvi wenu ni wenu, na hauhusiani kabisa na sisi, na chanzo ni mzee afu wewe ukamalizia na kubwa kuliko bila kujua unajipalia kaa la moto hukutumia hekima ukaamua kutumia hasira na matokeo yalipotokea unarudisha tuhuma zote kwa mwenzako yakwako umeyakumbatia, nakutizama sana mama naomba ukae mbarli sana na vita yangu hii nikihitaji msaada wako nitakuomba kwa sababu bado wewe ni mama kwangu, siwezi kwepa unanafasi kubwa kwenye maisha yangu lakini sio wewe tu ninyi nyote wawili kwangu ni wa thamani sana, nilikuwa nakuja nyumbani naleta zawadi yakwako tu, ata kunikumbusha kama mzazi na baba ako hapana, James alimletea baba shart tu ukalichoma moto ili tu mwanao asipate baraka ya mzazi wake, hio roho mama sio, nilikuwa nakuachia pesa jikoni nyingi afu nakuja kukukabidhi tena sebleni nyingne kwa ajili yenu nimegundua nilikuwa nakosea sasa hivi mtapata pasu kwa pasu na nguo nitakazomnunulia baba angu naomba kwa upole kabisa usizichome tutagombana, ulikuwa unamshindisha na njaa apa kwako ili hali anaumwa, sawa na nyumba hii kajenga mwenyewe, nimekuacha nimemchukua baba nimempeleka kwenye matibabu sasa hivi yuko sawa kabisa, anatembea mwenyewe, na hivi karibuni atarudi nyumbani kwake jiandae make uliyoyafanya unayakumbuka vyema kabisa, mama Albert alishtuka wewe mtoto umefanya nini? Umeamua kumtibu baba ako ili aje aniue si ndio? Albert alitikisa tu kichwa akaingia zake chumbani kwake akachukua vitu vyake vya muhimu nakusepa...

Itaendelea....πŸ”₯

Offer offer offer
Pata full kea kwa sh 800
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

WAKILI HUCHOKI JAMANI 🫣* *______________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA SITA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/wakili-huchoki-jamani-______________________________________-sehemu-ya-kumi-na-sita

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest