Wakati huo jua lilikuwa linapotea juu ya anga na giza lilichukua nafasi yake
Wakiwa kwenye gari kimnya kilitawala na safari hii Victor waliendesha gari kistaarabu.
" Suzan najua unaniona mtu mwenye roho ya ajabu ila nafanya haya yote kwasababu nakupenda.
" Mmmmh.... Suzan aliishia kuguna.
" Mbona unaguna?
" Sijawahi kuona mapenzi ya aina hii, mapenzi ya kulazimisha haupo romantic unalazimishwa mambo unafikiri mimi naweza kukupenda kwa moyo wangu wote kwa haya unavyomfanyia kweli?
Victor alitabasamu
" Mimi najua umeshanipenda tangia siku nyingi .
" Sio kweli na kama unahisi nilikubusu kwasababu ya upendo basi unajidanganya ule ulikuwa ni mchezo tu na ndio ulio niponza.
" Mchezo gani wa kuhusu mtu hadharani?
Suzan alimuelezea jinsi walivyokuwa wakicheza mchezo wao na marafiki zake mpaka ikafikia hatua ya yeye kumbusu.
Victor alicheka.
" Hiyo ilikuwa ni bahati kwangu yani nimejikita dodo chini ya muarobaini. Na kuhusu swala la kupenda nadhani sio inshu kubwa utanipenda mbele ya safari.
Hatimae walifika nyumbani kwa kina Suzan walipofika getini geti likifunguliwa na mama suzan alikuwa anatoka na kusimama pale nje kama vile alikuwa akimuangalia mtu. Suzan alipomuona mama yake alishituka sana.
" Mungu wangu, mama yule pale sijui nitajibu nini leo na ameshaanza kunitilia mashaka.
Victor alimuangalia suzan jinsi alivyokuwa na wasiwasi.
" Naweza kukusaidia kwenye hili?
" Kivipi?
" Naenda kuongea nae...
" Hapana itazidisha matatizo.
" Sawa lakini kama kutakuwa na tatizo utanijulisha mapema. Victor hakuongea kama kwamba anaweza kumaliza kila kitu na kuhakikisha Suzan anakuwa salama.
" Sawa. Nikishika tu naomba uondoke nitajua jinsi ya kujitetea.
Suzan alishuka kwenye gari akafunga mlango.
" Asante kaka Mungu akubariki. Suzan aliongea kwa sauti wakati huo mama yake alikuwa akimuangalia.
Victor aliwasha gari akaondoka na suzan alifika pale aliposimama mama yake.
" Shikamoo mama.
" Muda huu unarudi nyumbani alafu unarudisha na gari mpaka mlangoni mbona umejivua vazi la aibu wewe mtoto unataka nini?
" Mama huyu ni rafiki yangu.
"Hivi umeona wapi urafiki wa mwanamke na mwanaume? Na huyu mwanaume ndio huyo aliekutia madoa shingoni kwako?
" Hapana mama
" Suzan , suzan bado upo mikononi kwangu naomba usiniletee balaa kama huyo mwanaume ni mpenzi wako....
" Hapana mama mimi sina hayo mambo , siyajui kabisa.
" Hujui wakati ulikuja na alama shingoni na sasa umetoka kushushwa kwenye gari yani kuna muda naanza kuamini kile ninachojisikia huku nje.
" Kitu gani mama?
" Kila mtu anajua huwa unaletwa na magari.
Suzan hakuwa na alisema alinyamaza.
" Sikiliza mwanangu kama mwanaume anakupenda hawezi kupotezea muda na kukuchezea huko pembeni , mwanaume mwenye nia atakuja nyumbani kujitambulisha na kufuata utaratibu. Hebu nenda ndani ninahitaji muda wa kuongea na wewe kwa kina.
Suzan aliingia ndani kama vile mfungwa anaingizwa gerezani kutumikia kifungo chake.
Alipofika chumbani kwake alienda kuoga maana siku hiyo alitokwa sana na jasho.
Alipotoka bafuni alichukua simu kwenye mkoba wake akakutana na messege nyingi za James pamoja na missed call za kutosha. Alifungua messege moja baada ya nyingine , messege zote lilikuwa za malalamiko.
" Ulichinifanyia leo kimeniumiza sana sikujua kama unanichukulia kama fala kumbe una mwanaume mwenye hela anaeweza kutimizia kila unachotaka. Kwa hali hii bora nijiweke pembeni masikini mimi .
Suzan aliumizwa na messege za James alishindwa kujibu hata moja maana ukweli halisi umeonekana na hata alimueleza James anaweza asimuamini.
Akiwa bado inashikilia simu yake iliingia messege kutoka kwa Victor.
" Vipi malkia wangu mambo yanaendaje huko? Hakuna kilichokupata?
Suzan hakujibu ile messege baada ya dakika tatu messege nyingine iliingia.
" Nijibu basi acha kuniweka roho juu.
Suzan aliona kama usumbufu aliamua kuzima simu.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments