Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MTOTO WA MAID ACHIA MOYO WANGU Chapter 7--8 mama alipopona tulirudi Nilimuuguza wakatufukuza,

18th Sep, 2025 Views 23



nilimshukuru Mungu make mama alikuwa hataki kabisa kuacha kazi,tulibeba vitu vyetu tukaondoka hawakujua kama tumejenga hatukuwahi kumshrikisha mtu kabisa, tulihamia kwetu, maji na umeme vyote tulikuwa tushaweka, adi kitanda tulinunua kimoja na godoro moja, nyumba ilikuwa ya vyumba vitatu kimoja self, seble, jiko na store, ilikuwa nzuri sana na Kaka Benny aliitendea haki mno.

Basi bwana, tuliamua kufanya biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai, tulianza biashara uku tumefungua ka genge pale pale nyumbani, ka mboga za majani, dagaa, vitungu, yaani vitu vichache vichache vya gengeni, muda huo nikawa nawaza chuo itakuwaje, siku likizi ilifika Dada akaja, nilienda kumpokea, alikuja na kitanda na godogo, alidai tuache kumbana mama, nilifurahi hata mama alifurahi, akasema hakutegemea kama ataweza kuishi bila kazi, alikuwa anaogopa sana, kwa maisha aliyopitia bila kazi aliogopa mno kuipoteza kazi yake, tulimuelewa, na alianza kunenepa nikajua kumbe mama angu ni mrembo nyie, anashep atari mimi sasa mmh, sijui huu mwili nilifata wa nani kwanza hauna shukrani, ata nile vipi, siongezeki nipo nipo tu, nikicheza vibaya ata upepo wa kawaida tu, unanidondosha...

Sikui, Dada anapenda kunitania mwili wangu hauna shukran kabisa, leo tulikuwa bze tunacheza mdako mama na mabint zake, yani hatuna habari kabisa, ugeni ukatufikia, alikuwa ni G na mzee wake, tuliwakaribisha, tukahangaika sasa apo tulishukuru tunafuga, kuna kuku wa mayai na kuku wa kienyeji kwa ajili ya mboga, na hapo hatukua na hela, tulikaa pembeni tukaanza kujadili kufuga kuna raha yake, yani kama hapa leo tulikuwa tunaenda kudhalilika vibaya, ndani tuna elf 3 tu, afu wageni, hee tulichinga, tukawapikia, wakasema wamekuja kuchumbia...

mama Mimi niligoma, nilikuwa sijui najisikiaje tu, ilibidi mama na dada wanipike mpaka nikakubari, wakatoa kishika uchumba, mahari aligoma kupokea akaomba kwanza atupe muda kama tutaelewana ndo atapokea, walikubali, Lakini wakati wanaondoka, Baba ake na G aliuliza jina la mama, na historia yake kwa ufupi, mama alimtizama kwanza kabla ya kujibu, Dada akajiongeza akatuondoa sisi wakabaki wazee tu...

Itaendelea....

Chapter 8

Mama alimpa hatukujua yaliyojili, "G naomba naa wewe usije ukaniacha utaniumiza sana plz, nilimtizama sana, alionekana kuwa serious, ata dada alishangaa, akaamua kituacha mahali tuongee wenyewe, G aliomba kunikumbatia, alinikumbatia nikahisi hali furahi ya tofauti sana, aalinikumbatia kwa muda kisha akanikiss na kusema nakupenda, ila mimi moyoni nikawa naona kama nadanganywa tu, yani jinsi alivyo mzuri mmh, sio rahisi kunipenda mimi, yani nikahisi kabisa kuna tatizo, haiwezekani mkaka mzuri iv aty hana mtu, anipende mimi....

Ilikuwa ngumu sana kumuamini kwakweli,mda huo nilikuwa nimefunga kitambaa, kikawa kimeachia afu nywele zangu zilikuwa zimerefuka atari zimevuka kwenye mabega, nilitaka kurudishia kitambaa, G akanizuia, akazipapasa nywere zangu uku anazisifia, uku mimi nilikuwa nahisi kama nambembelezwa nilale, ule mpapaso ulifanya nikafunga kabisa macho nisikie raha vizuri, G hakuwa amegundua, alivyokuja kunicheki, akagundua nimenogewa na tuko sehemu inaonekana, aliamua kunikumbatia, akaacha kwanza alichokuwa anakifanya, akaniminya kiuno, nilishtuka adi wenge likakata, akatabasam nakusema, nimependa sana nywele zako naomba usizishave kabisa, gharama ya matunzo juu yangu, ila naomba chonde chonde usizitoe kwanza laini, nzuri, yani dah, umefanya nichanganyikiwe zaidi, Gift we mrembo mno, nilishusha tu macho kwa aibu...

Dada alitutafuta kama tuko tayari ili aje turudi nyumbani, tulimwambia aje tu, alikuja tukarudi wote, tumefika, mama alikuwa tu kawaida, tukajua kila kitu kiko sawa,G aliondoka na mzee wake, tukabaki wenyewe, nikaanza kupewa wosia, nikawa naitikia tu ila ata siwaelewi,siku ikaisha, kesho yake, nikapigiwa simu nipokee kuna mizigo yangu, nikapokea ilikuwa na mtu wa Bolt, ilikuwa ni tv make hatukuwa na Tv ni bufa tu ndo tulikuwa nalo, ilikuwa tv na meza yake, na mafuta yanywere, shapuu, stiming, na loshen ya mwilini, na vitenge pea nne, mbili za mama moja dada moja mimi, na vigauni, nilishukuru, nikasaini nakuingiza ndani, tulifunga wenyewe, wakaanza kunitania, nilivyomweupe, na nilikuwa natumia samona, sasa ivi loshen si nitakuwa mzungu na izi nywere, nikawa nacheka tu, make rangi yangu nikama mwarabu, alienusurika kuwa zeruzeru...

Niliamua kuanza kujipenda,awee nilikuwa pisi haswa, japo pisi kimbaumbau, Ronard alianza tena kuniandana, nilizima location, make najua tu ataanza usumbufu, na mimi sitaki heka heka, kibaya zaidi kwao sitakiwi, mama ake na Rose wote hawanitaki, na kibaya zaidi hawezi ata kunitetea ananipenda ila kunitetea hana ubavu,huwa anaacha tu afu anakuja kunituliza pembeni...

Niliamua kumpotezea, mawazo yakabaki chuo sasa, tukaomba mkopo ukagoma, nikaamua kusomea unesi tu,tukaanza kujichanga apo ata G sikumshirikisha, nilitamani kuomba nikasome kwenye chuo cha G atusaidie tulipe taratibu taratibu ila nikaogopa, ana Hosptal na chuo hapohapo, na ilikuwa nzuri zaidi mafunzo kwa vitendo...

Itaendelea....

FULL 1000
WHATSP 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MTOTO WA MAID ACHIA MOYO WANGU Chapter 7--8 mama alipopona tulirudi Nilimuuguza wakatufukuza,   >>> https://gonga94.com/semajambo/mtoto-wa-maid-achia-moyo-wangu-chapter-7-8-mama-alipopona-tulirudi-nilimuuguza-wakatufukuza

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest