Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

*MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI* *06....10* *_______________________________________* *SEHEMU YA 06* Eeeeeeh Walahi kipigo kilikuwa ni cha mbwa mwizi jamani, Yaani hamad alinipigia utazani anaapiga mwizi

13th Sep, 2025 Views 42

wala hakujali Kuwa Mimi ni mwanamke wake lakini pia nimebeba Mtoto wake.

Kipigo na maumivu vilinikolea mwisho nilipoteza fahamu kabisa.

Baada ya hapo nilikuja kuamka baada ya masaa mawili baadae na nilijikuta nikiwa sebuleni, bado nilikuwa na maumivu makali sana na sehemu niliyokuwa nimelala kulikuwa na damu za kutosha na zilikuaa zikitokea kwenye sehemu zangu za Siri.

“Mtoto wangu “

Nilizungumza kwa huzuni uku nikipapasa tumbo langu.

Nikajikongoja na kutafuta simu yangu na nilipoipata tu nikampigia Rafiki yangu Yaani Yule Neha na kumuomba msaada ili aweze kunisaidia maana sikuwa na mtu mwingine na sikutaka kuwapa wasiwasi wazazi wangu ambao pia hawako Sawa kutokana na kila kitu.

Neha Bwana ni best friend kweli kweli, nilimtumia location tu na baada ya muda akafika akiwa na mumewe, kwa pamoja wawili hao wakanichukuwa na kuniwaisha hospital.

Nilifika hospital na dokta akadhiilisha kweli Kuwa nimepoteza ujauzito, nikasafishwa pale na kupelekwa wodini kwaajili ya kuongezewa damu kwani nilipoteza damu nyingi sana.

“Shamsa sijakuzoea hivyo shoga Angu, Mbona Kama umekuwa mzembe Saana eeeh wewe sio Yule Shamsa niliyekuzoea “

Alizungumza Neha baada ya Mimi kumsimulia mambo yanayoendelea kwenye ndoa yangu.

“Neha maisha yanabadilika sana, ata hivyo hamad amebadilika gafla tu “

“Simaanishi hivyo Namaanisha jinsi ambavyo umekuwa mzembe na kuvumilia hayo manyanyaso, Shamsa wewe ndio ulinifundishaga Kuwa imara lakini pia kujipenda imakuwaje sasa hivi umekuwa hivi shoga Angu “

Aaaah nilikosa majibu na kubaki nikilia tu.

Baada ya muda mfupi baba na mama yangu walifika pale wodini kwani niliwapatia taarifa, muda huo ilikuwa ni Saa 3 usiku.

“Huyu muuwaji amekuja hapa ??”

Baba yangu aliniuliza baada tu ya kunijulia hali.

“Hajaja”

Nilijibu kWa sauti ya chini.

“Hii ndoa haipo Tena na kesho atakupatia taraka zote Tatu, najua si Jambo jema kwa Allah lakini pia haya sio maisha ya ndoa ambayo Mungu ameyaandika “

Alizungumza baba yangu akiwa amechukia sana na alimaanisha kila alichokuwa akizungumza.

******

Kwa upande wa hamad Bwana taarifa zilimfikia lakini pia hakuna umuhimu wa kuja hospital kuja kuniona zaidi Aliwasha na mziki pale Nyumbani yeye na mwanamke wake lakini pia na watoto.

Kiukweli watoto wangu hawakuwa wakielewa kitu chochote kile zaidi walikuwa wamepumbazika na upendo ambao baba Yao amekuwa akiwaonesha na jinsi ambavyo alikuwa akiwapa zawadi mfululizo.

******

Hatimaye siku nyingine ikashika nafasi nikiwa hospital lakini pia nilikuwa nikiendelea vizuri sana.

Majila ya sana 2 asubuhi baba yangu alifika hospital Lengo lake likiwa ni kuhakikisha Kuwa napata taraka kutoka kwa mume wangu hamad.

“İli shetani lako alijaja ??”

Baba yangu aliniuliza.

Ila nyie baba yangu amechukia sana, Yaani baba yangu hakuwai kutumia Maneno machafu kwenye maisha yake lakini kwa sasa ni anazungumza kwa hasira na kutamka Maneno machafu.

“Vipi kuhusu watoto wangu baba?”

Nilimuuliza baba yangu kwa hali ya utulivu sana.

“Watoto wamefanya nini ? Yaani pale unabeba kila kilichokuwa chako na watoto “

“Sijui Kama hamad atakubali baba Angu “

Baba aliniangalia mwisho akaniuliza.

“Huyu daktari wako anasemaje kuhusu kutoka ??”

“Nimesharuhusiwa baba kuna mtu namsubilia tu “

“Huyo mtu atawasiliana nae kwa sasa Twende uko kwa huyo shetani wako “

KWa taratibu kabisa nikakaa wima na kuzungumza.

“Baba Saa hizi hamad atakuwa kazini kwake “

“Kokote alipo Tunaenda “

“Unamaanisha nini baba “

“Yaani Leo hii lazima akupe taraka zako na tuna rudi Nyumbani hakuna cha kusubili “

Pasi na kufikilia Mara Mbili Mbili nikajibu.

“Siko tayali kuachana na mume wangu baba, ata hivyo ni wewe ndio uliniambia Kuwa taraka si Jambo jema kwenye maisha ya watu wawili ambao wameunganishwa na Mungu “

Baba aliniangalia na kuniuliza.

“Umelogwa au ?”

“Sijalogwa baba lakini siwezi kuachana na mume wangu Tena gafla hivi “

Baba yangu alichukia sana na kwa sauti ya ukali akazungumza.

“Kama utaendelea hivi Basi Mimi sitakiwa na radhi na wewe Tena Shamsa, Kama Mimi ni baba yako Basi utafatisha kile ambacho Mimi nakuambia”

Baba yangu alimaliza kisha huyo akaondoka zake na kuniacha Mwenyewe.

“Shamsa akili Yako iko Sawa kweli ??”

Alikuwa ni Neha ambaye aliingia wodini baada ya baba yangu kutoka ni wazi Kuwa Neha alisikia mazungumzo yangu na baba yangu.

“Sio rahisi kunielewa lakini haya ni maamuzi magumu sana kWa upande wangu, ni maamuzi ambayo yanaitaji ukomavu wa akili “
Nilizungumza kWa huzuni uku nikifuta machozi yaliyokuwa yakitililika kutoka kwenye macho yangu.

“Unamaanisha nini Shamsa ?”

Neha aliniuliza.

“Wasiwasi wangu ni kukosa watoto wangu, Neha hamad ni mtu Mwenye Pesa sana, na ukiachana na Pesa Ana connection nzito sana Unafikili itakuwa rahisi Mimi kupata watoto wangu ? Hamad anaweza akanipeleka mahakamani halafu nikashindwa kupata watoto wangu, Sina pa kushika Mimi Sina ata sehemu ya kusema naweza nikapata msaada “

Neha aliweza kunielewa na kwa huruma akanikumbatia kwa nguvu sana na kuniambia.

“Hakikisha Kuwa unakuwa imara “

“Usijali Neha “

Baada ya muda Neha akanichukua na kunirudisha Nyumbani kwangu kisha akaondoka.

Naweza nikasema Kuwa kitendo cha hamad kunipiga mpaka kusababisha mimi kupoteza Mtoto wangu kilinifanya nimchukie sana hamad, Yaani nilimchukia kuliko kawaida, Yaani Sijui Kama mnanielewa lakini namchukia sana huyu mwanaume.

“Ulikuwa wapi ??”

Hamad aliniuliza pale tu niliipoingia Nyumbani Kana kwamba ajui Kuwa nilikuwa hospital.

Kabla Sijajibu swali lake gafla watoto wangu walikuja na kunikumbatia kWa nguvu sana.

“We miss you mama “

Walizungumza watoto wangu wakiwa na furaha kubwa sana ya kuniona mama Yao.

“Mama amerudi sasa niliwamisi pia “

Hamad alibaki akinishangaa tu, kwa upande wangu nilichukua watoto wangu na kwenda nao chumbani kwao na kuanza kucheza nao uku na uku Kiukweli walikuwa na furaha sana.

Majila ya jioni nikaingia zangu jikoni na kuanza kuandaa chakula na nilikuwa naandaa chakula changu tu na watoto wangu.

“Wife material huyo “

Alizungumza Hadija baada ya kuja jikoni na kunikuta nikiendelea na mapishi yangu.

“Za jioni Hadija”

Nilimsalimia tu maana sikuwa na kitu kingine cha kumjibu.

“Hamad anataka kula makaloni Leo na maini, lakini pia anataka na juice ya embe hivyo utaandaa”

Alizungumza Khadija na kutaka kuondoka, Ila kabla ajaondoka nikazungumza.

“Jiko ni kubwa sana ili Khadija Karibu upike “

“Shamsa unatania sio ? Yaani Mimi ndio nipike ? Yaani Mimi ndio niharibu kucha zangu na wewe upo ? Bye the way wewe ndio mke KIJAKAZI kwenye hii Nyumba “


Weeeee nilijikuta nikichukia sana haraka nikamsogelea na kWa sauti iliyojaa maumivu nikamwambia.

“Kuna siku utavaa viatu vyangu, lakini pia utaelewa huu msemo wa mwenzako akinyolewa tia maji nywele zako “

Khadija akaniangalia na kwa dharau ya hali ya juu akanishushia msonyo mmoja Matata sana na kuondoka.
.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI* *06....10* *_______________________________________* *SEHEMU YA 06* Eeeeeeh Walahi kipigo kilikuwa ni cha mbwa mwizi jamani, Yaani hamad alinipigia utazani anaapiga mwizi  >>> https://gonga94.com/semajambo/mume-wangu-alivyoniolea-mke-wa-pili-06-10-_______________________________________-sehemu-ya-06-eeeee

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest