Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

KICHAA NA MIMBA YA BOSS SEHEMU YA SABA*

9th Sep, 2025 Views 41



Shahidi hakuingia tena ndani aligeuza na kwenda qetini kumpokea.

Sorry baby

"Shahidi hii ni sawa kweli?

"Nisamehe Aisha nilipitiwa.... Yani unapitiiwa wakati unajua mpenzi wako nakuja.

"Nisamehe bure mama.

"Umenikera bwana yani nimekuja na shauku zangu nimekumiss najua nitakukuta uwanja wa

ndege kumbe wewe upo tu huku umesimama na kwahiyo yule yule msichana sijui ni nani msichana ndio aliekuchekewesha si ndio?

Mmmm baby hebu acha hizi, mbona hubadiliki yule ni msichana wa kazi Tessy.

"Kwahiyo anaishi hapa ndani?

"Ndio lakini mambo mengine tutaongea badae twende ukapumzike kwanza.

Shahidi alimshika wakaingia ndani lakini bado

Aisha alikuwa na hasira. "Yani badala ya kwenda nyumbani nikaona nije

huku. Waliingia ndani shahidi aliongea nae na kuomba msamaha na mambo yakaanza sawa.

Siku zilizidi kwenda Kwa upande wa Shania alionekana kunyongonyea mara nyingi alikuwa akifika sehemu analala tena analala usingizi mzito pia alikuwa mnyonge kama vile anaumwa.

Siku moja shania hakuwa Ametoka nyumbani alikuwa amejilaza nje kwenye kimvuli cha mti.

Shangazi yake alipomuona alisema. "Leo ajabu hajaenda kuzurula au atakuwa ana umwa?

Inaonekana hayupo sawa alafu siku hizi amekuwa mpole sana. "Hiyo hali imeanza lini?

"Nimemuona kama wiki moja hivi.

Sasa tufanye mpango apelekwe hospitali huwenda ana Natalia au taΓ­fod maana vyakula

anavyokula huko mitaani havieleweki..

Mama watu wa aina hii huwa Mungu

anawalinda na maradhi kama hayo.

"Ni kweli lakini wasiwasi ndio akili. Hebu nenda kaandae maji tumuogeshe. Sawa lakini nadhani tungempa dawa za

maumivu.... "Sitaki udaktari wako ambao hauna vyeti fanya kama ninavyosema.

Mama Farida (shangazi yake Shania alienda pale chini ya mto kumuamsha Shania. "Shani, Shania mwanangu hebu amka, shangazi

anakuita.

Shania alifumbua nacho akamuangalia shangazi yake usoni na kuachia tabasamu la mbali.

"Amka mama yangu.

Shania aliamka na mama Farida aliushika mwili wake kupika joto kama lipo juu.

"Wala hana joto la homa. Shania twende ukaoge mwanangu.

"Aaaaaaa shangazi mimi sitaki bwana nasikia

baridi. Mimi nataka embe.

Sawa ukaoge kwanza alafu nakupa embe na juice sawa.

"Haya, utanipa na nia mbili?

"Ndio binti yangu mzuri.

Shania alinyanyuka haraka wakaingia ndani na

shangazi yake.

Mama Farida alimvua nguo na kumfunga kitenge kisha wakaenda bafuni alimuogesha vizuri mpaka akahakikisha ametakata wakaenda ndani akampatia mafuta na kumvakisha nguo

safi. Baada ya hapo walipanda bajaji na kwenda kwenye dispensary ya mtaa wa pili. Shania alikuwa akifurahia bajaji ilivyokuwa unatembea mkono watu waliokuwa aliwapungia wakitembea kwa miguu.

Kwa upande wa shahidi walikuwa wamekaa chumbani na Aisha lakini Shahid hakuwa sawa, alikuwa mtu mwenye mawazo.

"Nipo hapa lakini huchangamkia, kuna tatizo au haujaenda mimi kuwepo hapa?

Shahidi alimgeukia akamuangalia.

Unaongea ni wewe ningekuwa sitaki uje

usingekuwa hapa saizi? Nataka kujua huyu msichana wa kazi huwa anaishi hapa? Na ukemuajili lini?

"Ndio, ana kama miezi kumi sasa..

Shahid inawezekana vipi msichana kukaa ndani ya nyumba yako tena mkiwa wawili wewe

na yeye? Shahidi alimgeukia na kumuangalia usoni kwa

makini. "Kwahiyo unataka kusema nini?

Aisha alinyamaza kimnya maana Shahid

aliongea kwa ukall.

"Sikiliza wewe mimi sio mwanaume wa kishenzi naomba unipe heshima yangu. Namuheshimu

Tessy kama mdogo wangu na kama ingekuwa kama hivyo unavyofikiria basi nisingeruhusu

wewe kuwa hapa. Ukiniona nimejiinamia basi tambua nafikiria mambo ya msingi..

"Basi yaishe. Alisema Aisha kwa upole. Kimnya kilitawala Aisha akijisigeza karibu na Shahid. "Baby naomba leo unite out.

"Ukafanye nini?

"Tukale hata chakula cha usiku huko nje sio lazima tule chakula alichopewa house girl.

"Kama imechoka chakula cha house girl basi ingia jikoni kapike tuonje mapishi yako. Shahidi aliongea kwa ukali kisha akatoka nje.

Shania na shangazi yake waliingia chumba cha daktari mama Farida alitoa maelezo kwa daktari kisha daktari aliandika na kuwaambia wakafanye vipimo.

Walitoka na kwenda maabara wakachukuliwa vipimo

Baada ya kama dakika 15 majibu ya vipimo yakawa yameshatoka walirudi kwa daktari.

"Mama umesema huyu ni nani kwako? "Binti yangu, mtoto wa marehemu kaka yangu.

"Ok, tumefanya vipimo hana taifod wala maralia

"Sasa anaumwa nini jamani? " Vipimo vinaonyesha ni mjamzito.

Mama Farida alishituka aksmtolea daktari

macho.

"Daktari umesemaje?

"Vipimo vinaonyesha Shania ni mjamzito.

Mtumeeee nani kafanya hili jamani? Alisema mama Farida huku mikono ikiwa kichwani

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KICHAA NA MIMBA YA BOSS SEHEMU YA SABA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/kichaa-na-mimba-ya-boss-sehemu-ya-saba

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest