Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 09....10 Nyie nilianza kulia Kama Mtoto Mdogo na kuomba msamaha mfululizo lakini kilio

17th Sep, 2025 Views 22

changu kilikuwa Kama ni sauti za chiliku kwenye masikio ya hamad, hamad hakuweza ata kunihurumia zaidi alinitumia alivyotaka.

Nilijua Kuamka siku nyingine kabisa nikiwa kitandani mtupu kabisa, mwilini nilikuwa Nina maumivu makali sana lakini pia nilikuwa. Na uchovu wa kutosha kutoka na kipigo lakini pia na kazi nzito ya usiku kucha.

Muda huo huo akaingia Hamadi akiwa na trey aliloweka kifungua kinywa.

Nikijikaza na kunyanyuka lakini hamad akawai na kufunga mlango na kuniuliza..

“Unataka kwenda wapi ??”

“ ni muda wa kuwaandaa watoto wangu aendee shule “

Hamad akaniangalia kwa muda kisha akaniuliza.

“Hivi ukiniangalia unaniona Kama baba mjinga sana si ndio ? Ukiniangalia unaniona Kama Mimi siwezi kuwaandaa watoto wangu ? “

“Sijamaanisha hivyo hamad, ata hivyo ni asubuhi sasa siwezi kuendelea kubaki kwenye chumba chako wewe na Khadija”

Hamad akanishika shingo yangu kwa nguvu na kuniambia.

“Sema mume wangu “


Kwa sauti ya tabu sana nikasema.

“Mume wangu “

Hamad akanisukuma kwa nguvu sana nikaanguka chini kama Mzigo Walahi 🥹 Ila huyu mwanaume ni zaidi ya shetani Walahi, Kiukweli siwezi ata kumsamehe.

“Takataka wewe eti hamad mimi ni mume wako Sawa, Tena Shukuru Mungu licha ya umasikini wako na ukoo wako mzima still nimekuoa na kukupatia watoto wazuri ma handsome wa kwenda “

“Please mume wangu Niache nikawaandae watoto “

“Kwa taarifa fupi tu Saa hizi ni Saa 6 kasoro Binti Sawa, watoto wako shule kitambo sana, Mwenyewe unazani sana hizi ni Saa 12 Sijui”


Eeeh macho yalinitoka Kama Fundi Saa aliyepoteza nati Walahi, Yaani siku ya kwanza kazini ambapo natakiwa kufika Saa 12 asubuhi hatimaye Saa 6 mchana inanikuta nikiwa Nyumbani.

“Nifungilie mume wangu “


Hamad akaniangalia na kwa utulivu kabisa uku akivuta vuta mashavu yangu akazungumza.

Kuanzia sasa maisha yako ni umu Ndani, Yaani wewe na Mimi, Mimi na wewe, hao wehu wako waliokuwa wqkikipatia jeuri uko nje watakutafuta kwa Tochi”


Aaaah hamad hakuwa akitania ata kidogo Yaani alihakikisha Kuwa anafanya maisha yangu yanakusa ya tabu sana.


******

Week Mbili ziliisha nikiwa Sigatoka Ndani ya chumba iko jamani 🥹😫 kilikuwa ni mtu wa kukaa sehemu moja, Ndani ya siku zote hizo sikuwai kuona watoto wangu Wala kusikia sauti zao, lakini pia si kujua ata simu yangu iko wapi labda ingenisaidia kwa Namna moja au nyingine.

“Hamad imetosha sasa nataka kutoka nje utanifungia umu Ndani mpaka lini labda ??”

Nilimwambia hamad na muda huo ndio kwanza alikuwa akijiandaa kwenda kazini.

Hamad aliniangalia kwa muda kisha akajibu.

“Yaani wewe kutoka umu Ndani mpaka akili yako ikukae Sawa na ujue Kuwa Mimi ni mume wako na sio hamad, mpaka ujue Kuwa nastahili heshima”

“Nipe taraka yangu hamad nimechoka “

Wlaahi niliamua tu kuomba taraka yangu maana nilianza kukiona kifo changu kabisa, Yaani hamad hakuwa na huruma na Mimi ata kidogo, imagine unafungiwa Ndani Kama hivyo halafu kila siku ni Mli mmoja tu.

Kiukweli nilianza kuchoka mwili na ata AFYA yangu ilianza kudolola.

“Ooooh kuhusu taraka nimeghaili siwezi kulipia taraka “

“Hamad please Naomba taraka yangu me siwezi Tena nimeshindwa “

Nikianza kulia uku nikiwa nimepiga goti na kushikilia miguu yake maana mambo sio mambo kabisa kwa upande wangu.

Hamad alichoka sana na kwa kejeli ya hali ya juu akazungumza.

“Eeeeh shujaa imekuwaje Tena hautapambana kwaajili ya watoto wako ? Wewe si ulisema uwezi kutoka uku kwaajili ya watoto zako nini kimekubadilisha sasa “


Ni kweli naitaji sana kuondoka na watoto zangu lakini siwezi kuendelea naweza nikafa kabisa nikiwa Ndani ya hii Nyumba halafu watoto wangu wakabaki na baba tu hivyo ni bora nikatoka nje halafu nikajua napambanaje kwaajili ya watoto wangu.

“Watoto baki nao wewe ni baba yao najua utawalinda na kuwalea vizuri sana “

Nilijibu kwa utulivu wa hali ya juu ungawaje moyo ulikuwa ukiniuma sana.

“Sawa “

Alijibu hamad kisha akaendelea na shughuli yake ya kujiandaa, hamad alijiandaa alipomaliza akaondoka na kunifungia Tena Ndani.

Siku hii Bwana sikutulia kabisa niliangaika uku na uku kwaajili ya kunisaidia lakini nilishindwa kabisa ukizingatia mwili wangu ulikuwa dhaifu sana.

*******

Majila ya sana 3 usiku gafla mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa na hamad ndio kwanza alikuwa amerudi.

“Kuanzia sasa wewe ni mbwa Huru “
Alizungumza hamad.

Kwanza Nikamuangalia na kwa hasira nikamuuliza.

“Mbwa ??”


“Yaaaaah mbwa unataka uwe Nani ? Nimekufuga vya kutosha na sasa unaweza kwenda, Ila sharti langu ni moja tu Kaa mbali na watoto wangu Shamsa “

Nyieeeej macho yalinitoka Walahi, Ila huyu Jake Bwana ataki kabisa nitokea hapa Nyumbani kwake ni vile tu ajui kuishi na watu maana kila siku anakuja na kikwazo kipya.

“Kingine wewe bado ni mke wangu sitakupa taraka ata ata Mara moja, na ole wako nikuone na wanaume wengine uko nje “


Nilibaki nikitoa macho tu, Kiukweli hamad alijipanga kunikomoa tu hakuna kitu kingine kwake, kwakuwa nilikuwa nikiitaji kutokaa nje nikajikuta nikikubali tu.

Baada ya muda mfupi baadae nilikuwa tayali Nipo nje, nikisema nje Namaanisha nje kweli 😂🙌 Yaani getini kabisa na mabegi yangu, Yaani hamad alinifukuza kabisa na kila kitu changu isipokuwa watoto wangu.

Ila maisha ya Kuwa mama wa Nyumbani yaliniharibia kila kitu, just imagine Sina ata Mia mbovu mfukoni, najua watu watanishaangaa watauliza inamaana haukuwa ukisave katika Pesa ya matumizi ya kila siku, iko hivi hamad ni Yule mwanaume ambaye anaenda sokoni Mwenyewe akupi ata shillingi 50 😁🙌.

Nikaweka begi langu chini na kuanza kutoa vitu uku na uku nikitafuta siku yangu, Mungu Mwema jamani niliweza kuipata simu yangu na ilikuwa na chaji kidogo sana,

Kama kawaida mwaya msaada wangu wa kwanza ni Neha Yaani Sina mtu mwingine zaidi ya Neha, nikampigia na kwa sauti ya kilio Nikamuomba aje Nyumbani kwangu.

Nyieeeeeh bado nitaendelea kusema Kuwa Neha ni zaidi ya Rafiki kwangu, imagine hakujali Kuwa ni usiku sana baada ya muda yeye na mume wake waliwasili pale Nyumbani na kunikuta nikiwa nimejikunyata getini nikijililia Mwenyewe kwani nilikuwa na maumivu makali sana.

“Huyu mume wako anashida ya akili au ? “

Mume wa Neha aliniuliza maana ni mwanaume mwenzie lakini amuelewi kabisa.

Neha akamuangalia mume wake kisha kwa utulivu akajibu.

“Babe relax ni muda wa kumsaidia Shamsa kwanza “

Bado kWa pamoja tukapanda kwenye gari na safari ya kuondoka ikaanza.

Aaaah Walahi kuja watu wanaishi Bwana, hii Nyumba anayoishi Neha ni hatari jamani kwani Pesa wanato wapi hawa watu.

“Karibu snaa Shamsa “

Neha alinikaribisha.

Moja kwa moja nikapelekwa kwenye chumba cha wageni na kukabiziwa kila kitu muhimu na wakaniacha nipumzike.

*******

Hatimaye asubuhi ilishika nafasi nikiwa Sijapata ata leke la usingizi usiku kucha.

Basi nikaoga pale na kutoka nje ili niweze kuwasaidia kazi Mbili Tatu.

“Wewe Tena Mbona umewai kuamka ??”

Neha aliniuliza.

Muda huo yeye na mume wake walikuwa wakifanya usafi wa Nyumba Yao, Walahi nilijikuta nikianza kuwaonea Wivu Walahi kubwa watu wamepata wenza wao.

Nikiwa bado nawaangalia na kutabasamu peke yangu gafla Hodi ilisikika mlangoni na muda huo huo akaingia Khadija, Yaani mke mwenzangu.

JE KUNA UHUSIANO GANI KATI YA HADIJA NA NEHA ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO…..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 09....10 Nyie nilianza kulia Kama Mtoto Mdogo na kuomba msamaha mfululizo lakini kilio  >>> https://gonga94.com/semajambo/mume-wangu-alivyoniolea-mke-wa-pili-sehemu-ya-09-10-nyie-nilianza-kulia-kama-mtoto-mdogo-na-kuomba-m

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest