MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 12 Kwanza nilishtuka sana na kujiuliza huyu ni Nani na Kwanini anaingilia ugomvi gafla hivyo pasi na kuuliza kitu chochote kile .
Ukiachana na hivyo jamani huu Sijui ni umalaya au ni kitu gani nilijikuta nikiganda na kuangalia uzuri wa mkaka huyo ambaye alionekana Kuwa serious sana kwa wakati huo.
Hamad alinyanyuka akiwa na hasira sana na pasi na kuzungumza kitu chochote kile akapanda gari na kuondoka.
Mimi sasa 😂 nilibaki nikiwa nimeachia domon tu na kumshangaa mkaka huyo ambaye alinipatia msaada.
“Au malaika huyu ?”
Nilibaki nikiendelea kujiuliza tu.
“Ingia Ndani “
Aghaaaaah huyu mkaka jamani hii sauti Mbona nzito hivi ananichanganya mjue 🥹 Yaani ananivukuga kabisa Mtoto wa shekhe.
KWa mwendo wa ki gentlemen mkaka huyo akasogea kwenye gari yake akapanda na kuondoka.
“Haya na wewe Ndani uko “
Mama yangu alinifokea baada ya kuona Kuwa nimeganda tu, hapo ndio nikashtuka na kWa haraka nikaingia Ndani na moja kwa moja nikataka kuingia chumbani kwangu lakini mama yangu alinisimamisha na kuniuliza.
“Yule mwanaume ni Nani ??”
Muda huo mama yangu alikuwa amechukia sana Yaani acheki na yeyote Yule, Yaani mama alikuwa anaona Kama nawaletea ma drama hivi.
“Simjui mama “
Nilijibu.
“Shamsa nitakupiga ujue, Yule mwanaume ni Nani ? Yaani hatujamalizana na huyu jambazi wako unataka kutuletea jambazi lingine si ndio “
Nyieeeh mama yangu alinichekesha na nikajikuta nikicheka tu Walahi 😂, kwa hasira mama akavua kiatu chake na kunirushia, kwakuwa nimecheza sana rede nikakwepa na kukimbilia chumbani.
Siku iliyofuata nilijiandaa mapema sana na Kuwai kazini kwangu mama anajua kabisa wazazi wangu wangeniweka kikaangoni kwajili ya Yule mkaka ambaye alikuja kunisaidia usiku.
Nilifika kazini na moja kwa moja nikaenda upande wa majukumu yangu, nikiwa naendelea na majukumu yangu nikasikia salamu kutoka nyuma yangu.
“Za asubuhi Shamsa”
Ilikuwa sauti moja nzito sana lakini pia haikuwa ngeni masikioni mwangu haraka nikageuka na kuangalia ni Nani, uwiiiih uso kwa uso na mkaka ambaye alinisaidia usiku uliopita.
“Wewe”
Nilimuita kwa mshangao wa hali ya juu sana.
“Ni mimi, Unaendeleaje ??”
Aliniuliza Kana kwamba Mimi na yeye tunajuana.
“Wewe Naani sasa ??”
Nilimuuliza.
Mkaka huyo akatabasamu na kujitambulisha.
“Am MAX “
Walahi siikuelewa kabisa, kiufupi muonekano wake ulinichanganya mpaka nikawa nahisi Kama anaongea kikorea hivi 😂🙌.
“Ndio nini sasa ??”
Nilimuuliza.
Mkaka huyo akanisogelea Karibu kabisa na kunishika mabegani kisha kwa sauti ya kusisitiza akaniambia.
“Naitwa Max “
“Aaaah “
Niliishia kuitikia tu uku nikiendelea kumkazia macho tu na vile alinisogelea Karibu kabisa na kunishika mabega yangu ndio kabisa, kwanza mapigo yangu ya moyo yaliongeza kasi yakawa yanadunda mfululizo.
“Aaah, aaaah am aaah “
Sikuwa najua natakiwa kuzungumza nini Yaani alichanganya akili yangu kwa muda mfupi sana.
“Mmmmmh “
Ilikuwa ni sauti ya kike ambayo iliguna na kutushtua sana haraka tukageuka na kuangalia.
“Oooh Neha “
Nilijichekesha baada ya kuona Kuwa ni Neha, kwa haraka nikajitoa Karibu na huyo kaka na kwenda kusimama Karibu na Neha.
“Nawaona wenyewe “
Alizungumza Neha kwa sauti ya chini sana ambapo ni Mimi tu ndio nilimsikia.
“Una ona nini nawe”
Nilijibu uku nikijichekesha maana ni aibu wlaahi, Yaani kwa haraka haraka mtu anaweza kusema Kuwa Mimi na huyo mkaka tunamahusiano.
“Neha tuonane uku “
Alizungumza huyo mkaka ambaye alijitambulisha Kama Max kisha akashika njia akielekea ofisini kwa boss wangu, kwa haraka nikazungumza.
“Hakujafunguliwa uko boss bado hajafika”
Neha akaniangalia kWa muda kisha akacheka sana na kusema.
“Njoo uku Binti “
Mie Tena nimeitwa Kwanini nisiende, kwa mwendo wa haraka nikaenda na Sijui ata funguo walitoa wapi wawili hawa haraka wakafungua na kWa pamoja tukaingia Ndani.
“Funguo mmetoa wapi
Jamani ??”
Niliamua kuuliza tu maana naona ma Picha Picha tu.
“Binti Tulia nawe Mbona Una wasiwasi sana, relax babe kula ndizi kwanza nyama Zipo chini”
Kiukweli nilikuwa na wasiwasi sana maana boss wangu aliniambia Kuwa ofisi hiyo ni Mimi na yeye tu halafu nashangaa hawa wanaingia na funguo wanazo.
“Aaah Shamsa, huyu mbele yako ni max, lakini pia ndio mmiliki halali wa hii gym”
Alizungumza Neha baada ya kuona Kuwa Nimekuwa mtu wa wasiwasi sana.
“Na Yule mwingine je ?”
Niliuliza.
“Yule pia ni boss wako lakini huyu ndio mmiliki, Yule na huyu ni mtu na kaka yake , Bwana max alikuwa uko kwenye nchi za wenyewe na amerudi juzi usiku, na Jana tukaja Nyumbani kwenu usiku ili kukuambia Kuwa kWa sasa Utakuwa na max hapa ofisini lakini tulikuta hali sio Shwari kabisa”
Hapo sasa ndio nilielewa Kuwa usiku wa Jana max alifika pale Nyumbani akiwa na Neha.
Maisha yaliendelea na niseme Kuwa max alikuwa ni Rafiki yangu sana, yaani ni mkaka mzuri sana, ana Pesa Ndefu lakini pia ni kwenye utu sana, Sijui Niwaambie nini but huyu kaka jamani, Mungu akinipa Kama huyu nitakuwa wife material zaidi ya nilivyokuwa kwa hamad.
Miezi ilipita na niliweza kutunza Pesa baadhi na moja kwa moja nikaamua kufungua mashtaka kwaajili ya taraka lakini pia kwaajili ya kupata haki ya kulea watoto wangu ambao walikuwa wakinyanyasika sana kwenye mikono ya Khadija.
Nikiwa kazini bize kabisa na kazi zangu, mmoja kati ya wafanyakazi wenzangu akaja na kuniambia.
“Kuna mgeni wako hapo chini dear “
“Sawa “
Nilijibu kisha nikajiweka Sawa na kutoka nje, kwanza nilishangaa sana baada ya kukutana na dada wa hamad Yaani sabra.
“Sabra!“
Nilimuita kwa mshangao maana ni gafla halafu ni mtu ambaye kila
Siku tunagombana na kutupiana Maneno na Kama mnakumbuka Mara ya mwisho nilimpiga kibao mbele ya mama yake
Lakini pia mbele ya hamad.
“Wifi yanngu Mwenyewe huyo “
Alizungumza sabra na kutaka kunikumbatia, aaah sinaga huo Unafiki kwakweli, waziwazi nikakataa kumbato lake na kumuuliza.
“Una shida gani ??”
“Wwwh Wifi yangu jamani, ata unikaribishe nije uko juu nikaone unakofanyia kazi na Tupate wasaa mzuri kabisa wa kuzungumza na wewe”
Nilimuangalia kwa muda na kumwambia.
“Una Uhakika umekuja hapa kwaajili yangu au ??”
“Yaaah Nimekuja kwako Wifi yangu mrembo wakati wote”
“Sabra unaweza kwenda sasa muda wa drama uliishia kule kwa kaka yako “
Nilizungumza na kutaka kuondoka lakini gafla sabra akazungumza.
“Ni kuhusu kupata haki ya watoto wako”
Eeeh hapo ni Kama alinigusa hivi nikasimama na kugeuka nyuma.
HIVI AMEKUJA NA LENGO GANİ HUYU JAMANI ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO….
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni
SEHEMU YA : 12
Kwanza nilishtuka sana na kujiuliza huyu ni Nani na Kwanini anaingilia ugomvi gafla hivyo pasi na kuuliza kitu chochote kile .