MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 14 “Yaaah mke wangu, Shamsa Nafikili ungekaa kwanza then ndio tuzungumze”
“Sawa”
Nilijibu kWa sauti ya kutaka kulia kabisa Ila mapenzi nyie me si mke wa mtu jamani 😫.
“Aaah mama yangu Alipata shida ya akili miaka 6 nyuma baada ya baba yetu na Mdogo wetu wa mwisho wa kike kufariki kwenye ajali ya gari, kilikuwa ni kipindi kizito sana kwetu lakini kWa mama ilikuwa ni ngumu zaidi kutokana na umri wake, baada ya muda mama akakaa Sawa na Mimi nikapata kuoa mwanamke ambaye alimpendana sana na mama yangu, walikuwa ni marafiki wa Karibu sana na Nilijibunia wao, lakini tatizo la mama limerudo upya kabisa baada ya mke wangu kufariki”
Hapo max akatulia kwanza na kuangalia chini akizuia nisiyaone machozi yake.
Kiukweli nilijikuta nikimuonea huruma sana max wa watu ambaye alikuwa na huzuni sana.
“Kuna muda najiuliza ni Mungu ndio anataka Nipitie haya au ni kitu Gani 🥹💔 unajua mke wangu Alipoteza maisha akiwa kwenye wodi ya wazazi akipambania Mimi kuitwa baba”
Hapo max alilia kwa sauti kabisa kutokana na maumivu makali ambayo anayo moyoni mwake.
KWa utulivu wa halafu ya juu nikasogea Karibu yake na kumkumbatia kwa nguvu sana na kuruhusu alie kwenye kifua changu.
“Nia maisha mazuri Sawa lakini sina amani, sina furaha kwenye maisha yangu, Shamsa nimeenda mpaka kwenye nchi za watu uko nikiamini Kuwa nitakuwa Sawa lakini wapi Leo hii Nipo hapa, nimeshindwa kupona maumivu makali ambayo ninayo”
“Usijali max Utakuwa sawa dear “
Niliendelea kumtuliza pale mkaka wa watu na ni wazi alikuwa na maumivu sana moyoni mwake.
Sijui ata usingizi ulitupitia muda gani maana mpaka asubuhi yaaani na wa kwanza kuamka ilikuwa ni Mimi Ila Kasheshe lilikuja kwenye kunyanyuka Bwana 😂🙌 Yaani max alikuwa amelala juu yangu Tena kalala usingizi Mzigo kabisa na mikono yake Amezungushia kwenye kiume changu Kama kwamba alikuwa amekumbaatia mto.
“Sijui nimuamshe ?”
Nilijiuliza kimoyomoyo uku nikiendelea kumuangalia vizuri kabisa, my zangu huyu kaka ni mu handsome aswaaah Walahi huyu mama amejua kupata watoto wazuri.
Muda huo huo simu ya max ikaanza kuita na kwakuwa ilikuwa na sauti Kali sana max Aliweza kusikia na kuamka.
Kitendo cha max kufungua macho yake na kukutana uso kWa uso na Mimi lakini pia kwa jinsi alivyokukuwa amenilalia na kunikumbatia alijikuta akishtukaa sana na kwa haraka akanyanyuka na kusimama akishangaa tu mwisho akaniuliza.
“Ni Mimi ndio nimelala hivyo na umeniacha tu ??”
“Unamaanisha nini ??”
Nilimuuliza..
“Namaanisha Yaani ndio nimelala
Juu yako hivyo na nimejiachiia na huu uzito niliokuwa nao halafu umeniacha kweli ? Hivi umeweza ata kulala au ndio nimekutesa Binti wa watu ?”
“Max Bwana relax ata hivyo nimelala vizuri kabisa Yaani nimelala bila wasiwasi ondoa Shaka dear “
“Mmmmh ungenipiga ata konzi tu ningeamka”
Nilijikuta Nikacheka tu na muda huo huo sauti ya mama mzazi wa max ikasikika ikiita.
“Frida, frida, muda wangu wa uku huu ujue “
Nilimuangalia max na kumuuliza.
“Frida ni Nani au ni Mdada wako wa kazi ??”
KWa sauti ya huzuni sana max akajibu.
“Frida ni Jina la mke wangu, Mara nyingi amekuwa akimpikia uji mama kila asubuhi, aaah nilikuwa na dada wa kazi lakini ni siku ya Tatu Leo tangu aache kazi na kuondoka “
“Unaweza kunionesha jiko lilipo ??”
Nilimuuliza max nikiwa nataka kwenda kumuandalia mama yake uji.
“Unataka kufanya nini Shamsa? Kama ni kwaajili ya mama usijali, namtuma tu huyu mlinzi anaenda kumnunulia kwenye hii cafe hapa chini anamletea “
“Haina haha nitafanya hivyo please usikatae “
Basi max wa watu akakubali pale na moja kwa moja aakanionesha jiko lilipo na kila kitu na nikaanza kuandaa uji wa mwanamama huyo.
Nikiwa naandaa uji huo nilijikuta nikiwakumbuka sana watoto wangu ambao walikuwa wakipenda sana uji na Nimekuwa nikiwapikia kila asubuhi.
“Sijui Kama mnapikiwa uji kwa sasa “
Nilizungumza kWa sauti ya huzuni sana.
Baada ya muda kila kitu kulikuwa Sawa kisha Mimi na max tukajuandaa na kutoka na safari ikiwa ni kwenda gym kwaajili ya kuendelea na majukumu yetu ya kila siku.
“Kuna sehemu tutapitia kwanza nataka Kuna vitu nikafatilie”
Alizungumza max muda huo Mimi na yeye tulikuwa Ndani ya gari.
“Wapi Tena naa wewe jamani Mbona tunazulula tu “
Nilianza kujilalamisha Mwenyewe kwa kujidekeza kWa mkaka wa watu 😂🙌.
“Ni sehemu muhimu sana, Yaani hii sehemu anaijua mama yangu, baba yangu, mke wangu na Mdogo wangu tu Yaani ata marafiki zangu wa Karibu sijawai kuwaonesha na wewe ndio wa kwanza “
“Ata Neha ajui?”
Nilimuuliza.
“Yaaah ajui, halafu Neha sio Rafiki yangu Bwana ni shemeji yangu, Mimi na mume wa Neha ndio marafiki sana ila kwakuwa nega ni mcheshi sana na anaupendo wa hali ya juu nimejikuta nimemzoea sana Neha”
Hatimaye gari ikapaki nje ya ghorofa kubwa sana na refu mno, sehemu kubwa ya ghorofa ili ilikuwa ni kioo tu.
“Max subili kwanza ndio unaingia umu Ndani au ?!”
Nilimuuliza.
“Naingia au tunaingia nawe ? Tunaenda Ndani na sio juu sana ni ghorofa ya 14 tu hapo na tunatuma lift”
Nilimuangalia max kwa muda kisha nikaamjibu.
“Wewe nenda tu Mimi utanikuta hapa hapa Nina shida na hizi lift Yaani nikipanda tu Natapika mfululizo “
😂🙌 nicheke kwanza halafu Kuwaambie, kusema zangu za ukweli hizo lift nazisikia tu na kuziona kwennye tv lakini sijawai kupanda ata siku moja 😂🙌.
Kitu kingine haya majumba marefu nayo uwa yananiwazisha sana 😂🙌, Yaani kiufupi nayaogopa.
“Shamsa tutatembea tu wewe ni Rafiki yangu si ndio please usikatae “
Nyie huyu kama anajua kubembeleza Bwana, Mwenyewe nikajikuta nikikubali na kumwambia.
“Shikilia mkono wangu pasi na kuachilia “
“Hakuna Shaka “
Kukaa wa watu akanifungulia na mlango was gari na kwa pamoja tukaingia Ndani, kwa mara ya kwanza nikapanda lift na muda wote nilikuwa nimemkumbatia max nikiwa nimefunika mmacho yangu.
“Tumefika mama “
Alizzungumza max akitaka nimuachiie lakini pia nifungue macho yangu.
Kitendo cha Mimi tu kufungua macho, Yaani ni uso kWa uso na Mume wan hi Hamd ambaye alikuwa anataka kupanda kwenye lift hiyo.
JE NINI KITAJILI ?
TUKUTANE SEHEMU INAYO…..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni