MIMBA YA DHARURA 12
Waliongea huku Jayden wakisisitiza kupewa nafasi ya kumlea Tawakal. Lakini jibu la Nadia lilikuwa
" Muda ukifika kila kitu kitaenda sawa.
Siku zilienda Jayden waliongeza kumjali Tawakal na alionyesha mapenzi ya dhati kwa mtoto alinunua kila kitu kinachohitajika kwaajili ya mtoto.
Siku moja watu wakiwa kwenye ofisi zao wakifanya kazi kiliitishwa kikao .
" Boss wamerudi anataka kukutana na wafanyakazi wote.
Ilikuwa ni sauti ya wafanyakazi.
" Kwani Boss alienda wapi? Mbona kila siku yupo . Aliuliza Nadia.
" Hassan sio boss alikuwa kwa muda boss mwenyewe ndio karudi na anataka kuongea na wafanyakazi wote.
Watu wote waliingia kwenye chumba cha mkutano, kila mmoja akakaa kwenye sehemu yake wakisubiri boss aingie.
Baada ya dakika kadhaa alingia kabir na kwenda kukaa kiti cha mbele na kuwaangalia wote.
Nadia alipomuona kabir moyo wake ulishituka alimtolea macho kama mjusi alibanwa na mlango.
Chumba kizima kilikuwa ukimya wa ghafla. Macho ya wafanyakazi wote yalielekezwa kwa Kabir, lakini moyo wa Nadia ndiyo uliokuwa unadunda kwa kasi isiyo ya kawaida. Alijikuta akishusha pumzi nzito, akitetemeka mikono huku akijizuia kumwangalia moja kwa moja.
“Karibuni nyote. Kabir alianza kwa sauti yake ya kujiamini, akitazama kila mmoja kwa makini.
“Najua muda mrefu nimekuwa mbali, lakini sasa nimerudi rasmi kushika tena nafasi yangu.
Wafanyakazi wakapiga makofi ya furaha. Wengine walibaki kumtazama kwa heshima, wakionekana kufurahia kurejea kwake. Lakini Nadia hakuwa na hata chembe ya furaha badala yake, moyo wake ulikuwa kama unavunjwa vipande vidogo.
Jayden aliyekaa upande wa pili alimgeukia Nadia . Aliona jinsi Nadia alivyokuwa akitetemeka, macho yake yakiwa hayana amani. Alihisi kitu kisicho cha kawaida, lakini hakusema neno.
Baada ya kikao
Wafanyakazi walitoka mmoja baada ya mwingine. Nadia alijaribu kujipenyeza katikati ya wenzake ili asiweze kuonana na Kabir. Lakini ghafla akasikia sauti nzito nyuma yake:
“Nadia… njoo ofisini kwangu, nataka kuongea na wewe.
Mwili mzima wa Nadia ulitetemeka. Wenzake wakamgeukia kwa mshangao, wengine wakaanza kunong’ona. Jayden akabaki akimwangalia kwa macho ya kuuliza, lakini hakuwa na uwezo wa kuuliza chochote.
Nadia aliingia ofisini kwa Kabir alisimama mbele ya meza.
" Kaa kwenye kiti. Alisema kabir huku akimuangalia kwa makini.
Nadia alikaa kwenye kiti mbele yake huku mikono yake ikitetemeka. Kabir alimwangalia kwa makali.
“Nilidhani sitakuona tena, Nadia…” Kabir alianza kwa sauti ya chini .
" Hata mimi sikujua kama tutakuwa kuonana tena. Imekuwa kama ajabu kwangu na tena wewe ni boss wangu.
Nadia aliongea huku akijaribu kujifichahisia zake lakini sauti yake ilitetemeka.
Kabir macho yake kunuangalia Nadia na kujaribu kusoma hisia zake.
“Kwani ulitarajia nini, Nadia?” aliuliza kwa sauti tulivu lakini nzito. “Ulikimbia kana kwamba mimi ni adui yako, kumbe nilikufanyia nini cha kukufanya unitoroke bila kuonana na mimi?
" Nilijaribu sana kutaka kuonana na wewe ili tuweke sawa tofauti zetu lakini hukunipa hiyo nafasi Nadia.
“Kabir mambo mengi yamepita. Sitaki kuyafufua. Maisha yangu yamebadilika sana .
Kabir alinyanyuka pale kwenye akasogea mbele kidogo, akiegemea kwenye meza yake huku macho yake yakimtazama Nadia kwa hali flani.
“Badiliko lolote halitafuta ukweli, Nadia. Na ukweli ni kwamba bado nakukumbuka. Kila siku, kila saa, kila dakika nimekuwa na kufikiria wewe na hasa lile tukio zima lililotokea ule usiku.
Maneno hayo yakamchoma Nadia kama sindano moyoni. Alitamani kusimama na kuondoka, lakini miguu yake ilikuwa mizito.
“Usinifanye nikumbuke mambo ambayo nimehangaika sana kuyafuta kwenye akili yangu,” alisema kwa sauti ya chini, macho yake yakiwa na ukungu wa machozi.
Kabir alinyamaza, alimuangalia kwa muda mrefu kana kwamba alikuwa akisoma nafsi yake. Kisha akainua mkono wake, akashika faili lililokuwa mezani,
“Kwa sasa wewe ni mfanyakazi wangu. Lakini usisahau… hata kabla ya kazi hii, ulikuwa mtu cha thamani zaidi kwangu.”
Nadia alibaki amekaa, moyo wake ukipiga kwa kasi. Maneno ya Kabir yalikuwa yakimvuruga. Na ghafla mlango ukagongwa na Jayden akaingia bila kuruhusiwa, macho yake yakizunguka usoni kwa Nadia na Kabir kama vile anasoma kitu.
“Boss, kuna mambo ya kusaini…” alisema Jayden kwa heshima, lakini akabaki akimtazama Nadia kwa makini.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi














Maoni