MIMBA YA DHARURA 9
Nadia alijaribu kuficha huzuni yake kwa kujaribu kutoa tabasamu mara kwa mara alinyanyu grass ya juice na kunywa kidogo, lakini mikono yake ilikuwa inatetemeka.
Jayden alimwangalia kwa makini, moyo wake ukijaa hofu kana kwamba kuna kitu kinamumiza Nadia.
“Nadia, unajua unaweza kuniambia chochote, sio lazima ipambane na hisia zako mwenyewe,” Jayden aliongea kwa sauti ya upole.
Nadia alitabasamu , halikuwa tabasamu halisi lilikuwa tabasamu la kuigiza.
Nipo Sawa tu, Jayden ni mawazo tu ya kawaida.
Kwa mbali, macho yake yalibaki yakimfuata Kabir na mke wake. Kabir alionekana akicheka, akizungumza na wageni huku wakipeana mikono kwa heshima na furaha. Kila mtu alionekana kusherehekea upendo wao mpya na kumpongeza kwa hatua aliyochukua.
Nadia moyo wake ulilia kimya kimya , haikuwa kwaajili yake ila kwaajili ya Tawakal.
“Kwa nini niliamini kuwa bado ipo nafasi? Kwa nini nilihisi amani jana nilipomuona? Kumbe nafasi yangu kwa Kabir haipo tena, nafasi ya mwanangu Tawakal pia imepotea.”
Alijaribu kugeuza macho yake, lakini moyo wake ulikuwa umekwama kwa kabir.
Kila mara macho yake yalipoangalia uso wa Kabir, hisia za kale zilimrudia Upendo, maumivu, na hofu vikapishana ndani ya nafsi yake.
“Najua kuna kitu kimekugusa hapa ndani…” Jayden aliongea tena kwa sauti ya chini, huku akimshika Nadia begani.
" Punguza wasiwasi jayden kuna baadhi ya mambo yanayofanyika huwa yanakumbusha mambo yaliyopita hivyo hili tukio limenikumbusha jambo flani lililopita.
" Inaonekana kilimuumiza sana.
" Mr J naomba tuachane na hizo mada tuangalie hili lililopo mbele yetu.
Mc akitangaza maharusi waibuke na kwenda kucheza mziki. Kabir na mke wake walisimama na kwenda katikati ya ukumbi , kabir alishika kiuno cha mke wake kwa umakini mkubwa na mke wake aliweka mikono yake mabegani kwa kabir taratibu walianza kucheza huku waliangaliana
Mc akitangaza watu wanyanyzke kwenda kuungana nao.
Jayden hakutaka kupoteza muda alinyanyuka na kumpa mkono Nadia akimaanisha anyanyuke waende kucheza.
Nadia hakupinga alimpa mkono walisomea mbele na kwenda kucheza .
Wakati wanaendelea kucheza Kabir aliangalia upande wake wa kulia alimwona Nadia akiwa anacheza na Jayden Uso wake ulipoteza tabasamu kwa muda mfupi. Lakini hakusema kitu. Aliendelea kumshika mke wake, kana kwamba hakutaka mtu yeyote agundue mawazo yaliyomjia ghafla.
Nadia, akihisi macho ya Kabir yamemgusa, aligeuka haraka na kutabasamu Jayden kana kwamba hana habari na wala hajali kile alichokiona.
Kabir alihisi kike alichokiona ilikuwa ni mawazo yake au alimfananisha . Aliangalia tena huku akijaribu kujisogeza huku akiendelea kucheza alifika karibu na Jayden wakakubaliana na kupeana hongera huku Nadia akiwa anamuangalia kwa makini.
" Huyu ndio shemeji yetu? Aliuliza kabir huku akimuangalia vizuri Nadia.
" Hapana ni mfanyakazi mpya pale kazini anaitwa Nadia.
Hilo jina ilikuwa ni uthibitisho tosha kuwa ndio yule mwanamke alikutana nae miaka iliyopita .
Muda ulienda Nadia alitaka kuondoka .
" Jayden muda wangu wa kuwa hapa umeisha nataka kuondoka.
" Sawa nitakupeleke.
Jayden na Nadia walitoka ukumbini huku wakiwa wameshikana mikono ,wakati huo macho ya kabir yalikuwa yakiwashinikiza .
" Ni yeye , sijui kwanini amekuja tena kwenye maisha yangu. Alijisemea kabir na kuonekana kakosa amani pia kuna hisia za wivu zilimnyemelea aliamini Jayden ndie mwanaume anaemmiliki Nadia.
Nadia alifika nyumbani akiwa amechoka , alivua viatu na kutisha huko.
" Mwenzetu vipi ni uchovu au umeibua kidogo? Amina aliuliza lakini Nadia hakumjibu alienda kujitupa kwenye kochi.
" Nadi upo sawa kweli?
" Mtoto wangu yuko wapi?
" Yupo chumbani kwako Kalala.
" Uuuuh...
" Nadia mbona sikuelewi?
" Amina kichwa changu hakipo sawa nilichokitaka nacho huko kimenivunja moyo wangu nilichokuwa natarajia kimekufa.
" Unamaanisha nini kusema hivyo?
" Nimekutana uso kwa uso na kabir, ndio yule niliemuona jana......
" Ni jambo jema hilo .
" Hakuna wema hata kudogo ile sherehe ilikuwa inamhusu kabir na kabir ameitwa na ana mke mrembo sana .
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi














Maoni