Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MIMBA YA DHARURA 4

27th Aug, 2025 Views 28



Nadia alijifungia chumbani kwake, moyo wake ukiwa na shauku ya kutaka kujua kwenye ile barua kimetandikwa nini.
Alipofika alichukua begi lake akatoa ile barua
alikaa kitandani akafungua ile barua na kuangalia macho yake yalikuwa na hofu pia alikuwa na hamu ya kujua yaliyomo. Kwa sekunde kadhaa aliitazama tu, alishusha pumzi kwa nguvu kisha
Akaanza kusoma:

"Nadia,
Samahani kwa kile kilichotokea. Najua nilikuvunja, niliharibu kitu kisichostahili kuharibiwa ila ni maalumu kwa mtu aliyedhamiria kufanya hivyo.
na kila dakika inayopita moyo wangu unaniuma zaidi Sikukusudia. Usidhani kuwa nilikuchukulia kama mwanamke wa kawaida, la hasha, wewe ni tofauti, ni wa thamani kubwa zaidi. Leo ninapoondoka hapa, natamani ningepata nafasi ya kukuona tena, kuomba msamaha uso kwa uso. Lakini najua huenda hunihitaji tena maishani mwako wala kutamani kuniona Hata hivyo nataka ukumbuke kitu kimoja moyo wangu nimeuachwa mikononi mwako.
Kabir."

Nadia alihisi machozi yakimtiririka mashavuni, siyo kwa hasira tena, bali kwa hisia nzito. Alishindwa kuelewa kama ni huzuni, hasira au upendo wa ghafla uliokuwa inanyemelewa kwenye moyo wake.
Amina aliingia ghafla bila kubisha hodi akamkuta Nadia akifuta machozi.
"Etiiii… umesoma barua yake na unalia? Amina aliuliza huku akimwangalia usoni kwa makini.
Nadia alitikisa kichwa taratibu.
"Unakataa wakati naona unalia .
Nadia alikaa kimya kwa muda, kisha akasema kwa sauti ndogo.
"Najisikia vibaya, Amina… Najisikia kama nimeharibu kila kitu. Nilimkataa vibaya sana, kumbe alihitaji nafasi ya kuzungumza nami."
Amina alimshika mkono.
" Alikuwa anakutaka lakini hakujua thamani yake na sasa hayupo unajiona thamani yake?
" Hapana .
" Kila kitu hapana sasa ukweli wa hili uko wapi?
Nadia alimuangalia usoni alafu akasema.
" Wewe ni rafiki yangu sioni haja ya kukuficha.
Siku ile tuliyopotea usiku nilikutana kimwili na kabir nikitokea kumchukua sana , alijitahidi sana kuomba msamaha lakini sikumuelewa lakini kwa sasa naona hakuwa na kosa sababu hata mimi nilionyesha kutaka kile alichokifanya. Sasa ameondoka na nafsi yangu inanisuta sana nimegundua kuwa hakufanya kwa mukusudi ila ni mihemko yetu ndio sababu .
" Nilihisi kuna kitu kinaendelea kati yangu .
" Najisikia vibaya sana.
"Sikiliza Nadia, hakuna mwanamke anayeweza atamsamehe mwanaume wa aina hiyo kwa urahisi. Lakini kama moyo wako umeamua kusamehe basi msamehe .

Usiku ulipowadia, Nadia alijilaza kitandani akiwa bado na barua mkononi. Alijua kesho wangeondoka hotelini kurudi majumbani kwao. Lakini moyo wake haukuwa na amani. Maneno ya Kabir yalikuwa yamechora alama isiyofutika kichwani mwake.

Asubuhi ilipofika kuandika lako wote walipanda kwenye gari na safari ya kurudi kwao ilianza.
Nadia alikaa kando ya dirisha, akiangalia barabara , alikuwa kimya sana tofauti na marafiki zake waliokuwa wanacheka na kupiga story.
Akili yake ilikuwa kwa Kabir mwanaume ambaye hakujuwa kama atamuona tena. Lakini moyoni mwake aliapa, ikiwa kweli hatma itapanga wakutane tena, basi safari hiyo wataweka mambo sawa.
Akiwa kwenye dimbwi la mawazo Amina alimshika begani, Nadia akageuka kumuangalia.
" Unamfikiria kabir?
Nadia alitingisha kichwa akimaanisha hapana.
" Ila yule kaka ni handsome kama ingekuwa haujachumbiwa na Jawad ningekushsiri uwe nae.
" Acha ujinga yule ni mtu wa kukutana nae kwa bahati mbaya.
" Ni kweli lakini ingekuwa wewe ndio mimi nisinge acha bahati inipite .
" Vipi kama ana mwanamke wake anayempenda?
" Kwa jinsi alivyo anaonekana bado alikuwa anakuhitaji na hata kama ana mwanamke wake huko ingejulikana tu maana ninge mganda zaidi ya ruba.
Kwa maneno ya amina nadia akajikuta anacheka.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MIMBA YA DHARURA 4  >>> https://gonga94.com/semajambo/mimba-ya-dharura-4

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
profile
majario 27 Aug 2025 22:41
MIMBA YA DHARURA 4
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest