Nadia alifika nyumbani kwao akapokea kwa furaha na wazazi wake.
Baada ya wiki mbili kupita tangu Nadia arudi nyumbani kutoka vacation, maisha yake yalionekana kuendelea kama kawaida. Alijaribu kusahau kilichompata lakini moyoni mwake bado alihisi pengo kubwa maana hata mchumba wake alikuwa anajua yeye ni mwanamwari na hakujua anajibu nini siku alikutwa hana bikra.
Siku moja jioni Nadia alikuwa jikoni akiandaa chakula cha usiku mama yake alimuita sebuleni.
" Nadia mama....
" Abeee...
" Bado haujamaliza kupika?
" Nimemaliza namalizia kufuta futa.
" Fanya uje nina maongezi na wewe .
" Sawa.
Baada ya dakika chache Nadia alienda sebleni alimkuta mama yake
uso wake ukiwa na tabasamu la furaha.
" Kuna nini mama ?
" Njoo ukae hapa. Nadia alikaa pembeni ya mama yake huku akimuangalia usoni kwa makini.
“Nadia mwanangu, kuna habari njema.
" Habari gani?
"Jawad amekuja kuzungumza na baba yako. Anataka mwezi ujao tufanye harusi yenu.
Nadia alibaki ameduwaa, moyo wake ukiganda , alimuangalia mama yake moja kwa moja.
“Mama… mwezi ujao? Mbona haraka sana?” aliuliza kwa sauti ya mshangao.
Mama yake alitikisa kichwa.
“Harusi ni heri, mwanangu. Kwa nini tusubiri tena? Jawad yupo tayari. Familia zote zimekubaliana hivyo .
Nadia alihisi dunia ikizunguka. Moyoni mwake kulikuwa na umesinyaa kwa zile taarifa, lakini kwa uso wake alilazimisha tabasamu dhaifu.
“Mama bado nina mitihani ya chuo. Na pia… nadhani hatujaandaa vya kutosha. Labda tusubiri kidogo.
" Unajua Jawad anakupenda sana na amejichimbia kwa muda mrefu tangia ulipomaliza kidato cha nne na sasa hakuna kipingamizi tena mwanangu.
" Lakini mama
Kwanini msinipe uhuru wa mimi kumaliza masomo yangu na hata nipate kazi ndio hayo mengine yote yaendelee?
Kabla mama yake hajaongea chochote baba yake aliingilia kwenye mazungumzo yao kwa sauti nzito akasema.
“Hapana Nadia, tumeshaamua. Utamaliza mitihani yako baada ya hapo maandalizi yataendelea. Hii ndiyo baraka ya maisha yako.
Hakukuwa na nafasi ya kubishana tena. Nadia alijua mapambano yake ya kujitetea yamefika mwisho kabla hata ya kuanza.
Alinyanyuka na kwenda chumbani kwake.
Alichukua barua ya kabir akirudia kuisoma kwa mara ya nyingine kisha akasema.
" Tangia nikutanie na kabir najikuta sitamani tena kuwa na Jawad nahisi kabir ndio mwanaume sahihi kwangu.
Kesho yake Nadia alienda kukutana na dada yake.
" Hakuona bibi harusi mtarajiwa.
" Dada sitamani hii ndoa .
Zakia alimuangalia huku akiwa kakunja uso wake alafu akauliza.
" Kwanini?
" Unajua sijawahi kuwa na hisia na jawadi ni shinikizo la wazazi wamenichsgulia mwanaume sababu ya kujuana kwao tu na kuendeleza urafiki wao.
" Lakini Jawad anakupenda sana na kumbuka amekuwa akikutunza tangia zamani. Na wewe ulikubali.
" Nilikubali kwakuwa nilikuwa sijui lolote kuhusu mapenzi, kupenda na niliona sawa kwa kila kitu lakini sasa naelewa kila kitu juu ya swala zima la kupenda.
" Nadia usiniambie kuwa unampenda mtu mwingine.
" Sijasema hivyo.
" Naomba uridhie ndoa yako na Jawad usitake kuudhi wazazi.
Nadia alitulia kimnya.
" Hata mimi sipo upande wako na sikuungi mkono kabisa kwenye hayo mawazo yako. Tena mlaani shetani huenda sio akili yako.
Siku zilienda Nadia alifanya mtihani wake wa mwisho .
Baada ya kumaliza mitihani yake ya chuo Nadia alianza maandalizi kwaajili ya harusi yake na Jawad . Alianza kuzunguka madukani na mama yake kutafuta nguo, viatu na mapambo ya harusi. Alijitahidi kucheka na kuonekana mwenye furaha, lakini moyoni mwake kulikuwa na mzigo mzito.
Mara kwa mara walipokuwa kwenye mizunguko Nadia alihisi kuchoka sana, mwili ulipoteza nguvu. Kila alipojaribu kumweleza mama yake, alijibiwa kwa urahisi:
“Ni kawaida mwanangu. Maandalizi ya harusi ni shughuli kubwa, kila msichana hupitia haya hiyo ni hofu tu ya ndoa . Ndoa ikipita utakuwa sawa.
Hata mimi kipindi nataka kufunga ndoa na baba yako nilikuwa na hofu sana mpaka nilikonda.
Nadia akanyamaza, akijifariji kuwa ni kweli. Hakuwahi kufikiria zaidi ya hapo.
💍Hatimaye siku kubwa ilifika. Nyumbni kwa kina Nadia kulipambwa kwa mapambo mazuri, wageni walijaa kila kona, muziki ulipiga kwa shangwe. Nadia alivishwa gauni la kifahari, sura yake ikipambwa kwa tabasamu la bandia huku moyo wake ukiwa na hofu isiyoelezeka.
Marafiki na ndugu walimtia moyo kwa kumwambia hiyo ni kawaida na ajitahidi sana kuficha hofu yake kwa tabasamu.
Baada ya muda magari ya kutoka upande wa bwana harusi yaliingia , watu walichungulia madirishani.
" Mashaallah bwana harusi kapendeza sana yani hii ndoa mbona itafana.
Nadia alivyosikia hivyo moyo wake ulidunda kwa kasi huku kijasho chembamba kikimtoka .
Walifunika na mitandio mwepesi huku akiwa kainama. Watu waliimba na kufurahi.
Kwa upande wa Nadia mambo yalianza kubadilika dakika chache kabla ya kufungishwa ndoa. Nadia alianza kujisikia vibaya ghafla. Jasho jingi lilianza kumtiririka mwilini kana kwamba amemwagiwa maji. Mapigo ya moyo yake yalikuwa yanadunda kwa kasi mno.
“Mama… sijisikii vizuri,” aliongea kwa sauti dhaifu.
Kabla hata hajamaliza maneno, mwili wake ulilegea, macho yakafunga, na akapoteza fahamu mbele ya wageni wote. Sherehe ikasimama ghafla, makelele ya furaha yakabadilika kuwa vilio na mshangao.
" Jamani mwanangu ... Mama Nadia alilia huku akipewa na kanga .
" Nadia, Nadia mwanangu fungua macho....
Wengi walijua huenda Nadia amefariki .
" Mmmmmh kwenye hii dunia kuna ushirikina sana kigagura wameshafanya yao.
Taarifa ziliwafikia wanaume ikabidi zoezi la kufungisha ndoa liahurishwe Jawad alinyanyuka haraka na kukimbilia chumbani kwa bibi harusi wake.
Alimkuta Nadia Kalala huku watu wakiwa wamemzunguka.
" Hebu pisheni , nipeni nafasi...
Nadia, Nadia naomba uamke usijifanye hivyo nilisubiri sana hii siku amka Nadia....
" Jamani pisheni tumuwahishe hospitali.
Alisema mwanaume mmoja wakambeba na kumkimbiza hospitali.
Walifika hospitali walipokelewa na Nadia akakimbizwa wofldini na kuanza kufanyiwa vipimo huku nje kila mtu alikuwa akiomba dua yake, Jawad akili yake haikuwa sawa alihisi kuchanganyikiwa msimamizi wake alikuwa pembeni yake akimfariji.
Baada ya muda mfupi, Nadia alifumbua macho yake akajikuta yupo kwenye kitanda cha hospitali na Mama yake alikuwa pembeni akimshika mkono kwa hofu, baba yake akizunguka huku na kule akiuliza madaktari.
Daktari alifika na kusema kwa sauti tulivu
“Msihofu sana. Nadia yupo salama. Amechoka....
" Uchovu tu ndio awe hivi? Aliuliza baba Wakati huo Nadia alikuwa akimuangalia daktari huku akiwa na hofu
"Tatizo sio hilo pekee. Tumefanya vipimo na tumegundua kuwa ni mjamzito wa mwezi mmoja na wiki kadhaa.
Maneno hayo yalitua kama bomu. Mama yake akashika kichwa, baba yake akakosa nguvu ya kusimama, na Nadia akabaki akitazama dari la hospitali machozi yakimtiririka.
Mimba aliyodhani ni siri moyoni mwake sasa ilikuwa imetangazwa mbele ya kila mtu. Na mbaya zaidi, ilikuwa mimba ya vacation na muhusika ni kabir mwanaume asiejulikana anaishi wapi na atampataje.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments