MIMBA YA DHARURA 7
Siku ile haikuwa ya kawaida kwa Nadia. alikuwa na matumaini makubwa ya kufanikiwa alikuwa na imani anaenda kutafuta mwanga mpya wa maisha yake na ya mwanawe.
Akitoka na kuchukua usafiri wa pikipiki ukampekeka mpaka kwenye kampuni moja ya simu. Alishika kwenye pikipiki akasimama huku akiangalia lile jengo huku akiomba dua aweze kupata kazi baada ya kuzunguka na vyeti vyake kwa muda na bila mafanikio.
Alipiga hatua kwa ujasiri japokuwa ndani yake hofu ilimtafuna.
Alijipa moyo kwa kusema
“Usiogope Nadia kumbuka unatafuta riziki sio kwa ajili yako peke yako bali kwa ajili ya malaika wako mdogo. Hii ni hatua ya mwanzo.
Nadia akavuta pumzi ndefu, wakaingia ofisini. Walikaa kwenye viti vya kungojea zamu ya kuingia chumba cha usaili. Baada ya muda, sekretari akawaita mmoja mmoja.
Nadia akabaki akihisi tumbo linacheza kwa wasiwasi. Wakati anasubiri, kijana mmoja nadhifu, mwenye suti ya kijivu ya heshima na sura ya upole, aliketi karibu naye.
“Habari yako dada?”
Nadia akahema, akajibu kwa heshima:
“Nzuri,
“Umefika kwa ajili ya nafasi ya kazi?” aliuliza kwa upole huku akimtazama kwa macho yenye upendo.
“Ndio, natumai Mungu atanijalia leo.”
Kabla mazungumzo kuendelea, sekretari akaita jina lake:
“Bi. Nadia, tafadhali ingia.”
Moyo wa Nadia ukadunda kwa nguvu. Aliingia ndani ya chumba cha mahojiano. Ndani aliketi jopo la watu watatu mwanaume mmoja mzee, mama wa makamo, na kijana mmoja aliyeonekana kuwa boss mdogo wa kampuni hiyo.
Aliulizwa maswali mengi kuhusu elimu yake, uwezo wake wa kufanya kazi, na ndoto zake za baadae. Ingawa mara nyingi alijikuta akitetemeka, kila mara alipojibu alikumbuka uso wa mtoto wake Tawakal na kupata nguvu mpya.
Mwisho wa mahojiano, yule boss kijana akamuuliza swali moja lililomgusa zaidi:
“Kwa nini unataka hii kazi, Bi. Nadia?”
Alikaa kimya kwa sekunde chache, kisha akajibu kwa ujasiri.
“Kwa sababu nina mtoto mdogo ambaye nataka nisimame kwake kama mama jasiri anayepambana. Sitaki amkute mama dhaifu aliyeachwa na dunia. Nataka amkute mama atakayeweza kumsomesha, kumlisha, na kumfundisha maana ya kupigania maisha.
Chumba kizima ukanyamaza. Maneno yake yaligusa mioyo ya wote waliokuwepo.
" Asante miss Nadia unaweza kwenda tutakutafuta.
Nadia alitoka pale, hakuwa na hakika kama atapewa kazi ama la. Alienda nje akawa amesimama akitafakari afanye nini .
Siku mbili zilizofuata Nadia alikuwa anasubiri kwa hamu. Hatimaye, simu yake ikalia. Ilikuwa kutoka kwa kampuni alivyofanyiwa interview mara ya mwisho.
“miss Nadia, tunafurahi kukujulisha kwamba umepitishwa. Tafadhali fika kesho kuanza kazi rasmi.
" Asante.
Nadia alipiga kelele ya furaha. Amina akakimbia kutoka chumbani:
“Nini tena rafiki yangu?”
Nadia akamkumbatia kwa nguvu huku machozi ya furaha yakimtiririka.
“Amina… nimepata kazi! Hatimaye nimepata kazi!”
Wote walifurahi wakalia na kushangilia. Kwa Nadia, hiyo haikuwa tu kazi bali ilikuwa mwanzo wa hadithi mpya ya matumaini, mapambano.
Kesho yake Nadia alienda kuanza kazi kwenye idara ya masoko alikabidhiwa ofisi yake mpya na kuanza kazi.
Nadia alifanya kazi zake kwa bidii na kwa umakini mkubwa sana.
Mkuu wa kitengo cha idara ya masoko Jayden alitokea kuvutiwa sana na utendaji wake wa kazi pia alihisi kuwa na hisia na Nadia. Alianza kwa kumtoa lunch huku wakiwa wanaongea maswala ya kazi.
Ikafikia muda walizoeana sana wakawa kama marafiki staffment.
Siku moja wakiwa lunch jayden alimwambia.
" Nadia kesho jioni kuna rafiki yangu anafanya sherehe baada ya kutoka Fungate na sina mtu wa kwenda nae, unaonaje kama utanipa kampani.
" Samahani Jayden sitaweza "
" Usijifanye hivyo bwana tafadhali nikubalie ombi langu.
" Huo muda natakiwa kuwa na mtoto wangu .
Jayden alimuangalia usoni kwa makini.
" Usinitanie wewe. Inamaana una mtoto?
" Ndio mimi ni mama wa mtoto wa miezi 8.
" Siamini hauonekani kama una mtoto mdogo.
" Ukweli ndio huo.
" Hongera.
" Asante.
" Kwahiyo wewe ni mke wa mtu?
" Hapana am a single mother.
Jayden alitoa tabasamu ambalo lilimpa matumaini flani. Na pia alitaka kujua mambo zaidi.
" Vipi baba wa mtoto .....
" Mr J naomba tusifukue makaburi ila jua mimi ni mama .
" Ok sawa . Vipi kuhusu ombi langu?
" Nitaongoza na na wewe ila kitachukua muda mrefu nitawahi kurudi kwaajili ya mtoto wangu.
" Sawa.
Walimaliza kupata chakula wakarudi kazini kila mmoja alienda kwenye ofisi yake wakati Nadia anaelekea ofisini kwake akipishana na mwanaume mmoja alikuwa akiongea na simu Nadia alipomuangalia usoni moyo wake ulipuke.
Walipishana na yule mwanaume Nadia aligeuka tena kumuangalia .
" Hapana sitaki kuamini kama ni yeye.
Full 1000
Whats 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi














Maoni