Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

KIUTANI NIMEINGIZWA UKUBWANI* *1---2* *_______________________________________* *SEHEMU YA KWANZA* Jimmy ni mwanaume wa miaka 38 kutoka nchi ya Marekani

11th Sep, 2025 Views 35

alikuwa akifanya biashara zake kubwa nchni Tanzanian pia alifungua kampuni kubwa sana. Licha ya kuwa na huo mri Jimmy hakutaka kabisa swala la kuowa yeye alikuwa Bize na biashara zake hata kama alikuwa na mambo yake mengine ilikuwa kwa siri sana hakuwa anapenda skendo za ajabu ajabu.

Katika mipango yake ya kutaka kutimiza mambo yake alitakiwa kufunga ndoa yani awe na cheti cha ndoa na wakati huo hakuwa na mpango wa kuwa na mke..

Jioni moja jimmy alikuwa amekaa na rafiki yake Patrick rais wa Tanzania, mfanya biashara mkubwa pia. Jimmy akaamua kumshirikisha swala lake ili aweze kumpa msaada.

"Kama nilivyokwambia bado nataka kuwa hapa na ili mipango yangu kutimia natakiwa kuowa.

Patrick akitabasamu kidogo kisha akanyanyua grass na kunywa fundi moja kisha akarudisha grass mezani.

Hatimae umeamua sasa.

"Hilo ni swala dogo sana jimmy hapa wasichana

Kumbuka nataka cheti na sio ndoa.

warembo wako wengi sana na wakila aina sema unataka mwanamke wa aina gani, toa sifa zake.

"Haujanielewa vizuri Patrick.

Mimi sitaki mke nataka cheti cha ndoa.

Nimekuelewa vizuri sana Jimmy Kila unachokitaka utakipata kikubwa ni pesa tu. Unajua pesa kwangu sio tatizo nataka jambo

liende haraka sana.

"Sawa nipe siku ya leo, kesho nitapata jibu.

Iwe uhakika tafadhali.

Ondoa shaka nina kijana wangu mmoja hajawahi kuniangusha.

Baada ya mazungumzo waliachana Patrick alimtafuta kijana mmoja wa chuo Mike na

kumuelezea shida ya jimmy.

"Mike najua wewe Mjanja na haushindwi nataka unitafute msicha mrembo, smart na Mjanja. "Hiyo imeisha bro nakuletwa mtoto mbichi

kwenye sifa ulizotaja. Patrick alitoa kiasi cha pesa na kumpa yule

kijana. "Kesho mapema sana mlete kwangu.

"Usijali kaka hili limeisha, mapema nitakupigia simu.

Poa.

Patrick aliondoka na kumuacha Mike akiwa bado kasimama

Mike alipiga mahesabu na mahesabu yake yakaangukia kwa binti mrembo mwenye

kujiamini na Mjanja prisca. Muda huohuo alitoa simu yake na kumpigia

Prisca "Hey Puko wapi?

"Nipo chuo.

"Vizuri nipo hapa maeneo ya getini njoo chapu kuna mchongo wa maana.

"Poa nakuja hapo sasa hivi.

Mike alikaa sehemu akimsubiri mara akamuona Prisca akiwa anaelekea maeneo ya getini.

"Hey Prisca. Prisca aligeuka kumuangalia. "Njoo hapa mrembo tujue tuyajenge

Mike usinipotezee muda nataka unipe

mchongo wa maana sio michango isiyo na hela Ni mambo ya pesa ndefu mama Prisca

aliposikia mambo ya pesa ndefu alisogea karibu zaidi.

"Mmmh niambie.

"Kuna mchango wa hela kama utakuwa tayari kesho nikupeleke maeneo "Wapi?

" Maeneo flani ya watu wakubwa huko.

"Kwanza mchongo wenyewe ni mchongo gani?

"Kuna jamaa anataka cheti cha ndoa.....

Sasa mimi na cheti cha ndoa wapi na wapi? "Tulia basi nikupange.

"Eheeee

"Huyo jamaa ni raia Marekani yupo hapa ana biashara zake ukisikia biashara ni biashara kweli sio biashara ya mitumba ni makampuni makubwa, muwekuzaji wa maana kabisa.

"Nenda kwenye point tafadhali.

Ndio nakuja huko, sasa kuna mambo yake yanataka cheti kwahiyo anataka mrembo wa kufunganae ndoa ya mkataba baada ya muda

flani ndoa inakufa. Na unajua talaka ikitoka lazima upate chochote kitu.

Acha hizo wewe ukiniangalia mimi nataka ndoa ?

"Hiyo sio ndoa yani akifunga ndoa akipata cheti wewe unasepa zako unamuachia vyeti vyake.

Prisca alitulia kidogo huku akiwa kashika kidevu chake.

"Mbona kama nakuelewa hivi.

"Huu mchongo wa maana sana mara kesho unaingia chuo na ndinga yako.

Unajua kushawishi. Poa kesho tutaenda huu mchongo usimpe mtu

mwingine. "Nitampa nani wakati wewe ndio Mjanja hapa.

Kwahiyo fanya maandalizi kesho asubuhi na

mapema nakupeleka mjengoni. Poa hilo limeisha.

Usisahau kupigilia mapigo flani, yani gauni moja matata yani utoke kwaajili ya ndoa. "Naelewa.

Kesho yake mapema sana Mike alikuwa nje ya geti la chuo akimsubiri Prisca.

Pia alionekana akiwa anaongea na simu mara

kwa mara. Baada ya muda kidogo Prisca alifika huku akiwa amevalia gauni lake safi la lango ya

off white na nywele zake alikuwa amevaa vizuri. Mike alimuangalia huku akitabasamu.

"Safi sana yani umepita kulekule.

Acha maneno mengi, tunafanya je sasa? "Hakuna kupoteza muda moboss wanalisubiri

huko na wanasumbua hatari.

Walikodi tax na kuelekea kwenye kampuni ya Patrick. Wakati huo Patrick na jimmy walikuwa wakiwasubiri kwa ham

Chapter 2

Jimmy na Patrick wakiwa ofisini Jimmy alikuwa anaangalia saa ya mkononi kwake.

"Una uhakika watafika?

Kuwa mpole kaka huyu kijana hajawahi kuniangusha wapo njiani. Muda sio mrefu watakuwa hapa.

Prisca na Mike walifika ndani ya jengo la ofisi Prisca akawa anashangaa. Mike hii ni sehemu kubwa sana mpaka napata

uwoga

Tulia mtoto nilikwambia hili ni kubwa sio maadili ya kitoto kama ulivyozoea. Mike alipiga simu kwa Patrick kumjulisha kuwa. wameshafika

Niambie Mike

Nipo mjengoni na mtoto mkali.

Sawa pita ofisini kwangu.

Poa

Mike alikata simu akamuangalia priscz ambae alikuwa na hofu kidogo.

*Twende zetu.

Walielekea kwenye lift kisha wakaenda mpaka ghorofa ya tatu. Walifika kwenye mlango wa ofisi ya Patrick

Hebu subiri kwanza.

Alisema Prisca.

Vipi tena.

Huyo mtu yupoje?

Wa kawaida tu punguza wasiwasi. Prisca karibu kwenye safari ya mamilioni Hakuna kurudi nyuma.

Mike aligonga mlango.

Fungua mlango. Baada ya kukaribishwa mike alifungua mlango

wakaingia ndani Waliingia ndani ya ofisi macho ya jimmy na

Patrick yalikuwa kwao. Waoooo karibuni sana.

Asante.

Walienda kukaa kwenye sofa alimuangalia Jimmy ambae Patrick alikuwa

akimuangalia Prisca huku akimthaminisha. Bro muhusika wetu ni huyu mrembo anaitwa Prisca. Mike akimtambulisha.

Karibu Prisc

Asante. Bila shaka unajua sababu ya wewe kuwepo hapa.

Ndio

Upo tayari

Ndio maana nipo hapa. Safi, huyu ni mr Jimmy, ndio mtu ambae

mtafunga ndoa ya mkataba

Prisca alimuangalia Jimmy na kuamini kuwa ni mtu kutoka nje maana hata kiswahili chake hakikuwa kizuri akichanganya kiswahili na

kiingereza.

"Kwahiyo huyu ndio huyo msichana? Ndio, smart and Sharo kama yule uliokuwa.

unataka.

Jimmy alimuangalia tena prisca.

Nitakulipa milioni 10.

Endapo utafanya kile ninachokitaka

Prisca alishituka maana hela alivyotakiwa hakutegemea wala hakuwahi kuishika U. Una unauhakika?

Mike na Patrick walitabasamu.

Ni pesa ndogo sana kwangu.

Sawa lakini kumbuka sio ndoa kweli ni dill hakuna MAPENZI hakuna uhusiano ni cheti tu

Jimmy akitabasamu kwa mara ya kwanza kisha akasema.

Good then lets proceed.

Vipi kuhusu malipo yangu

Cheki imeisha andaliwa.

Sawa tunaweza kwenda.

Wakiongozana wote wanne wakaenda kwenye ofisi ya msajili wa ndoa.

Jimmy na Prisca walikaa kwenye viti huku mashahidi wakiwa wamesimama nyuma yao.

Je mpo hapa kwa hiari yenu? Afisa msajili

aliuliza. Prisca alimuangalia Jimmy kwa sekunde kisha

akajibu. "Ndio Jimmy nae akajibu

Ndio

Baada ya kukubali kila mmoja alisaini upande wake, vyeti vikagongwa muhuli na kukabidhiwa

vyeti vyao vya ndoa.

Jimmy alijiangalia kile cheti huku akitabasamu. Mr and mrs Jimmy hongereni sana. Asante.

Baada ya kutoka nje ya jengo jimmy alimpatia Prisca cheki ambayo ilikuwa imeisha sainiwa

"Haya ni malipo yako. Prisca alipokea kwa bashaha huku akiwa na

tabasamu pana.

Asante hapa kila mtu aende na njia yake. Baada ya hapo kila mtu alishika njia yake, Huku nyuma mike nae alipewa fungu lake

Mida ya saa kumi Prisca akiwa nyumbani kwao na furaha zake mara simu yake ilita alipoangalia alikutana na namba ya Mike

Huyu anataka nini tena na kazi imeisha? Lakini hakuacha kupokea, alipokea ile simu.

Niambie Mike. Prisca kuna jambo la dharula limejitokeza

unatakiwa kukutana tena na Jimmy Kuna nini tena wakati tumeshamakizana.

Inasemekana wafanyakazi wake wameandaa sherehe ya kum surprise hivyo unatakiwa

kuwepo kwenye hiyo sherehe.

Unasemaje wewe? Mbona kama mnaenda kunitania?

Kabia Mike hajajibu ilisikika sauti ya Jimmy. Kubaki kuja nitakupa milio mbili. Baada ya Prisca kusikia hela alitoa macho hakuwa na ta

kusema Prisca alikaa kimnya hakujua akubali hiyo ofa au

akatae. Hey lady... Sauti ya Jimmy alimshitus

Sawa lakini sijajiandaa kwa chochote, unajua kwenye sherehe natakiwa kupendeza.

"Hilo sio tatizo tukutane MAYA FASHION. "Sawa nakuja hapo sasa hivi,

Prisca alingia ndani haraka akachukua kibegi chake kidogo na kukiweka mgongoni. Wakati anaondoka mama yake alimuona.

Wapi saizi na vunegi vyako?

Naenda kujisomea na wenzangu.

Prisca unamjua vizuri sana kaka yako. Aaaah mama, hivi mtanichunga mpaka lini? Mimi nimeshskuwa mkubwa bwana na isitoshe

siendi kufanya kitu kibaya naenda kujisomea na wenzangu.

Shauku yako.

Prisca alitoka hivyo hivyo kigumu alichukua usafiri wa pikipiki mpaka Maya fashion. Alikuta gari ya kifahari imepaki nje ya duka na

muda huohuo jimmy alishuka akiwa kwenye suti moja kali alikuwa amependeza sana kuliko alivyomuona asubuhi

Jimmy alipiga hatua kumfuata Prisca alipofika

karibu alisalimia.

Ingia hapo ndani kila kitu kipo tayari ni wewe tu unasubiriwa

Ok

Prisca aliingia dukani na kuchagua nguo na viatu pamoja na vito vya thamani. Na kila kitu alikuwa amelipa Jimmy.

Baada ya hapo waliondoka na kwenda saloon

huko Prisca alitengenezewa haswa na kuvaa nguo zake, alitoka saloon akiwa kapendeza mno mpaka Jimmy alikuwa anamshangaa huku akiwa kashika kiuno.

Prisca alipiga hatua ndogo kumfuata alifika karibu yake na kusimama mbele yake. Waoooo umekuwa mrembo sana.

Asante.

Jimmy alifungua mlango wa gari na Prisca akapanda Jimmy aliweka vizuri gauni kisha

akafunga mlango nae akaenda kupanda na kuwasha gari wakaelekea ukumbini.

Walipokuwa nje ya ukumbi wakiwa bado wapo

ndani ya gari Jimmy alitoa pete. Naomba nikuvalishe hii pete

Kuna pete tena? Na hii si ni pete ya ndoa? Ndio inabidi

Prisca alinyoosha mkono na jimmy akaingia pete kwenye kidole.

Baada ya hapo akavaa na yeye kisha akashuka kwenye gari na kwenda kumfungulia mlango, Prisca alishuka

Naomba tuingize kama mume na mke kweli. Sawa

Jimmy aliweka mkono wake na Prisca aliingiza mkono wake katikati kisha wakaanza kutembea taratibu kuelekea ukumbini

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KIUTANI NIMEINGIZWA UKUBWANI* *1---2* *_______________________________________* *SEHEMU YA KWANZA* Jimmy ni mwanaume wa miaka 38 kutoka nchi ya Marekani  >>> https://gonga94.com/semajambo/kiutani-nimeingizwa-ukubwani-1-2-_______________________________________-sehemu-ya-kwanza-jimmy-ni-m

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest