Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MADAM NIPE KIDOGO BASI 17

13th Sep, 2025 Views 60


Basi baba mkwe na mama mkwe wakaombana misamaha pale na sisi kesho yake tukarudi zetu nyumban na maisha yetu yakawa yanaendelea kama kawaida…

Siku moja mume wangu akanambia kuwa event kazini kwao, anataka nivae nipendeze kwa ajili ya hio event, na sikuwa na namna zaidi ya kukubali, maana mume ndio ameshasema sasa, mimi ni nani nipinge…..
Basi bana siku ikafika na mume wangu kipindi hicho alikuwa tayar ameshanunua gari, hivyo akanipeleka saloon, nikapambwa vizuri na baada ya kupambwa tukaenda zetu kwenye event, mume wangu ni ile aina ya wanaume wanaojali sana, alikuja akanifungulia mlango wa gari, na baada ya hapo akanishika mkono mpaka ndani, hakuwa anajali kabisa kuhusu watu, na kweli watu walikuw wanatuangalia ila hakuwa anajali, alichokuwa anakiangalia ni furaha yangu tu,basi muda wa chakula akaenda kunifatia chakula, kisha akaanza kunilisha, yaan ni kwamba hajali mashabiki, mtajijua wenyewe, kumbe tulisahau kuwa kinachokupa furaha kifiche sisi tukakidhihirisha na kuibua maibilisi wa kibinaadamu wa kutosha bila kujua…

Basi maisha yakawa yanaenda kama kawaida, na baada ya kama wiki mbili kutoka tutoke kwenye ile event, mumewangu akabadilika kabisa, akawa ni mtu ambae ana wasiwasi sana, sikuwa najua ule wasiwasi ulikuwa unatokana na nini, maana alikuwa anaficha simu, alikuwa anaficha kila kitu, mpaka nikajikuta naanza kupatwa na mashaka juu yake…

Ila kila ambapo nilikuwa nafuatulia sikuwah kugundua jambo lolote lile, maana alikuwa bado ni mume na baba mzuri, ila shida ikawa ni hofu kupitiliza na kuficha ficha baadhi ya vitu vyake..
Mwanzo nilikuwa Napata wasiwasi mpaka nilipoona makala moja ya dada yangu ummuh junaynah, akanipa moyo sana na kunambia kuwa “ kama mwanaume haujamfumania basi usimuwazie usaliti, huenda kuna mambo anapitia hataki kukuambia, hivyo muache na umpe utulivu mpaka siku ambayo utamfumania ndio useme kuwa anakusaliti, na kama unahisi kuwa hauwezi kumuacha mtu basi usifuatilie simu yake, watu pekee ambao wanayo mamlaka ya kufuatilia simu za wenza wao ni wale ambao wanauwezo wa kuwaacha, basi nikakaa zangu kwa kutulia na nikaacha kabisa kumfuatilia….

Siku moja ilikuwa ni jumapili, mume wangu alisema kuwa atapika yeye, hivyo mimi nisipike kabisa, nikakubali, nikawa zangu ukumbini naangalia tamthilia, mara simu yake ikaita, hakuisikia maana simu ilikuwa ukumbin na yeye alikuwa jikon, ila haikuwa imesaviwa, sijui ni kitu gani ambacho kiliniambia nipokee, nilkipokelewa na sauti ya kike ya madeko inayosema “ yaan ukishakaaga na mke wako haunikumbuki kabisa mimi, nataka na mimi unifanyie kama unavyomfanyia mke wako bana, acha kunibania bania Kendrick…
“ Kendrick hayupo hapa unaongea na mke wake Kendrick, wakati ambapo Kendrick anampikia mkewe, wewe ni nani mke mwenzangu, nikasema ila hapo roho inaniuma hatar…
“ mimi ni mke mwenzako, na hapa nilipo nina mimba ya Kendrick na ananipenda sana, akaanza kusema Yule mwanamke..
Sijui nilipata wapi nguvu za kujibu, maana nilimuambia kuwa “ mwanamke anaependwa sana hanaga kelele, si unaona namna ambavyo mimi nimetulia na sina kelele na mtu, basin i wazi hata wewe unajua ni nani anapendwa zaidi, nikajibu kisha Yule mwanamke akasonya na kukata simu…

Nilikuwa nahisi kupasuka, maana nilikuwa namuamin sana mume wangu, nilikuwa siamin kama anaweza kunisaliti hata kwa bahati mbaya, nikasimama, ila kabla sijaenda jikon akaleta chakula, alishtuka mara baada ya kuniona nimesimama nikiwa nimeshika simu yake mkononi, na machozi yalikuwa yananitoka kwa hasira……
“mke wangu shida ni nini? Akauliza kwa wasiwasi mkubwa…
ITAENDELEA…..

Offer offer offer
Soma yote kwa sh 800
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MADAM NIPE KIDOGO BASI 17  >>> https://gonga94.com/semajambo/madam-nipe-kidogo-basi-17

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest