MADAM NIPE KIDOGO BASI 13
Basi mahusiano yetu yakawa yanaendelea ila ni kwa siri sana, na mimi ndio niliekuwa natraka usiri, kwa sababu nilikua naona aibu sana kuonekana kuwa nina mahusiano wa kimapenzi na aliekuwa mwanafunzi wake..
Maisha yakaenda na kiukwlei yalikuwa ni mapenzi mujarabu, yaan mubashara, laity kama watu wangekuwa wanajua namna ambavyo nilikuwa napendwa na Kendrick basi wangenionea wivu…
Alikuwa anawapenda wanangu wote kama watoto wake wa kuwazaa kabisa, yaan wote wanakuwa wanamuita baba na hio ndio ilikuwa fahar yake, basi akaenda zake chuo, sijui hata alikuwa anafanyaga kazi gani, maana alikuwa anapambana sana kuhudumia familia yake…
Alikuwa anasoma engeniariang, na akasoma miaka minne, na nwakati wote huo mapenzi ni bam bam, nitake nini nisipewe, yaan sikohoi ameshafika…
Mtoto wangu mkubwa alikuwa ana miaka kumi na moja, na mdogo alikuwa ana miaka mitano na wote walikuwa wanasoma, na walikuwa wanasomeshwa na Kendrick…
Alimaliza kusoma na Mungu alikuwa upande wake, maana baada ya kumaliza tu chuo akapata kazi dar es salam, nikajikuta nakuwa na wasiwasi, ila alikuwa anapambana kuniaminisha kuwa hakuna mwanamke hata mmoja duniani ambae ameshawah kumpenda kama ambavyo alikuwa ananipenda mimi, na alikuwa ana thibitisha hilo kwa vitendo kabisa yaan…
Maisha yakaenda na akaanza harakati za kutafuta uhamisho, ingawa ilikuwa ngumu ila nilihamia dar pamoja na familia yangu ili niweze kukaa na mume wangu mtarajiwa Kendrick, na baada ya swala la uhamisho kukamilika, akataka akapeleke posa kwetu, nikakubali…
Akawapanga ndugu zake na kweli posa ikapelekwa nyumban, na wazaz wangu walipomuona kendirck ni kama walishtuka, maana alikuwa kwenye miaka ishirini naa na mimi nilikuwa nina thelathin na kitu maana tulikuwa tumepishana miaka kama kumi, hivyo ukiangalia tu haraka haraka utajua kabisa kuwa mimi nilikuwa mkubwa, ila kwakuwa nilimpenda wazaz wangu hawakuwa na shida na mimi, issue ikaja kuwa kwao sasa…
Baada ya wazaz wake kuniona walishtuka maana nkwanza walikuwa wananijua, maana nimeshawah kukutana nao shule, na wanajua kabisa kuwa nilikuwa mwalimu wa kijana wao…
“ kama unataka kumuoa huyu sisi hatumtaki, umekosa wanawake wa rika lako, unbakuja kutuletea mzee mwenzetu, sasa n hivi hauwezi kumuoa huyu mwanamke hata iweje, na hautakaa uwe nae, labda kama mimi sio mama yako, akasema mama yake na Kendrick nikashangaa Kendrick anatabasamu kisha akasema “ ni kwlei mimi najua nimewekewa libwata mama, maana hizi sio akili zangu, nakupenda na nakuheshimu sana mama yangu, ila nikuambie tu ukweli kuwa, nimekuja kumtambulisha na sio kumuomba ushauri mtu kuwa niwe nae au laa, maana moyo wangu umeshamchagua na hakuna ambae anaweza kunitenganisha nae hata kwa bahati mbaya…………
Kisha akanishika mkono akaanza kuondoka na mimi, mama yake akaanza kusema “ ukiutoa mguu wako ukiwa na huyo mwanamke, nakuahidi mimi sio mama yako tena…
“ nakupenda sana mama yangu ila nasikitika kusema kuwa hakuna laana za namna hio………….
Kisha hao tukaondoka zetu, tulipofika nje ikabidi na mimi nimuulize maana hata mimi sikuwa namuelewa kabisa yaan..
“ kwa nini haujafata uamuzi wa wazaz wako?...
“ victoria hata nani aseme nini mimi siwez kukuacha, maana najua mateso na mapito ambyo nimepitia kukupata hivyo siwez kuruhusu mtu aje kututenganisha kirahisi namna hii…
Kwakuwa posa ilishakubaliwa nyumban kwetu, basi harakat za ndoa zikaanza baada ya muda kupita nikafunga ndoa na hatimae nikawa mke halali wa Kendrick….amba
Hakuna ambae aliamini kuwa nimeolewa na kendrick ila wakati wote Kendrick alikuwa ananitoa
Wasiwasi na kunionesha kuwa, hajali maneno ya watu na anachokiangalia ni furahja yangu mimi nay eye pamoja na familia yetu…
Siku moja nilikuwa nimetoka zangu kazini, nafika nyumban nashangaa namkuta mama yangu mkwe pamoja na dada yake Kendrick wakufiukia, ni kama binamu tu, waliponiona tu wakaanza kucheka vile vicheko vya kinafki, nikawasalimia kisha nikapitiliza moja kwa moja mpaka chumban kwangu, ila kabla sijaingia ndani nikashangaa mama mkwe anakuja na kuingia chumban kwangu kisha akalala kitandani kwangu na kusema “ embi tuambie umetumia dawa gani mpaka umemfanya mwanangu akuoe bibi kizee kama wewe, tena ulieolewa ukaachika na una mtoto, ni kwamba unataka kumuambukiza mwanangu uzee au…
ITAENDELEA…………..
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi












Maoni