MADAM NIPE KIDOGO BASI 10
Nilihisi kuchanganyikiwa, na sio siri katika kipindi ambacho nilijihisi mzembe wa mwisho nikipindi hicho, yaan nimekutana na mwanaume kwenye mahafali na nikajiamin kabisa na kwenda kulala nae, bila hata kumjua vizuri, nikaanza kujilaumu, maana sikuwa na namna yoyote ile ya kumpata…
Nilikaa nikalia, nikatafakari, maana tayari nilikuwa nina mtoto mmoja, ambae nilimpata kwenye ndoa yangu ya nyuma, alafu nakuja kupata mtoto mwingine kizembe kabisa…
Kwa kuwa nilikuwa nina kazi na nina uhakika kwa kumlisha mtoto, nikaona sio shidA sana, maana naweza kumlea mwanangu kwa namna yoyote ile, nikaamua kuacha maisha mengine yaendelee…
Siku moja, nakumbuka ilikuwa ni mwisho wa mwezi, nikashangaa shillin laki moja inaingia kwenye account yangu, kisha nikashangaa na ujumbe unaingia unasema “ hongera sana kwa kubeba mimba yangu, nakuahidi sitakuacha pekee yako kwenye kipindi hichi kigumu, naomba jitunze na mtunze mtoto wetu, na nikuambie tu kuwa sina kingi, ila kidogo nitakachpokipata nakuahidi kuwa niotashare na wewe…
Ilikuwa ni namna mpya, nikaanza kujiuliza ni nani, ila sikupata majibu, nikasema nghoja nikaangalie usajili, nikashangaa nakuta jina la kike, moja kwa moja nikahisi mwenye ile namba sio ambae amenitumia ule ujumbe mfupi…….
Nikatuma sms na kuuliza nani mwenzangu, ila sms haikwenda, na nilipojaribu kupiga pia haikupatikana, basi kuanzia mwezi huo, kila mwezi nikawa natumiwa laki moja na jumbe mbali mbali za kunifariuji, kwa akili zangu za haraka haraka nikajua kuwa ni Yule mwanaume ambae nilikutana nae kwenye mahafali, hivyo sikuwa na shaka kwa kubeba mimba ya mtu anaejua thamani yangu na anaejitambua kama huyo, licha ya kuwa na mambo yake mengine……
Basi muda ukaenda na mimba ikawa inaendelea kukua, kama mnavyojua kuwa mnazi haupandwi uani, ndivyo ambavyo minbva haiwezi kufochika, mimba ikafikisha miezi sita, tumbo likaanza kutoka, sikujali na hakuna mtu hata ambae aliniuliza maana nilikuwa mtu mzima, na kama nikitaka kubeba mimba, basi ni nimebeba mimba kwa kuwa nataka….
Siku moja nipo zangu kwangu hapo tumbo limenichosha balaa na wakati huo nilikuwa nafua kwa tabu tabu, mara simu yangu ikaita, ila hata kabla sijapokea ikawa imekata na wakati huo huo ikaingia sms inasema “ baby daddy wako nimesharudi, je upo tayar kuniona…
Sijui ni kwanini nilijisikia vizuri baada ya kuona hio sms, na kwa sura ya bashasha nikaandika sms kwa shauku kubwa kuwa, “ ndio nimekumiss sana, na mtoto wetu amekumiss mno, naomba nikuone tafadhali…….
Mara ikaingia sms nyingine ikawa inasema “ nataman shauku yako niendelee kuwa juu hivyo hivyo hata kama ukiniona, maana huenda usipende kuniona kama kawaida yako, ila angalau mungu ametafuta sababu ya mimi kuwa na wewe…
Hio sms sikuielewa, ila nikajibu tu njoo please hata kama utakuwa ni jini, mimi nipo tayar kuwa na wewe, kikubwa mwanetu alelewe kwa mapenzi ya baba na mama wote na nisimlee pekee yangu…
Baada ya sms kuandika kuwa imefika nikashangaa nashikwa bega, si ndio nikasema nigeuke nyuma, nashangaa nakutana uso kwa uso na kendric, alikuwa na sura ya bashasha kisha kwa upole akasema “ mimi ndio baba wa mwanao…….
Maswali ambayo wewe unajiuliza na mimi na jiuliza hay ohayo, inakuwaje, kendric awe ndio amempa mimba madam, na wakati hatukumbuki kama ameshawah kulala nae, sio sisi tu, hata madam nae anashangaa maana haelewi ni lini alilala na Kendrick mpaka akambebesha mimba…………..
ITAENDELEA……….
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi












Maoni