Sikutaka kumjibu maana sikuona busara kukaa kujibizana na mama wa mtu, maana ni kama kumvunjia heshima mume wangu…
Yule mama alipoona sijibizani nae, akaanza kulia na kusema “ mchawi, sikuwa najua kama huyu mwanamke ni mchawi kiasi hichi, mwanangu tuondoke tusije kumalizwa kama alivyomalizwa kijana wangu, nikashangaa wanaondoka kwa taharuki kisha Yule dada akaniangalia na kusema “ nitahakikisha namtoa mwanangu kwako, maana hatutaki uchawi kwenye familia yetu…
Nilishangaa sana ila nikaona ni bora wameondoka maana wakiendelea kukaa pale ni lazima watapoteza amani ya moyo na maisha yangu kwa ujumla…
Nikashangaa baada ya kama wiki mbili dada wa kazi anataka kuondoka, yaan sikugombana nae na nimekaa nae miaka miwili, kwanini ghafla hivyo anataka kuondoka, nikamuomba akae kae mpaka angalau mwanangu akue kue, ila alikataa nikaona isiwe kesi nikamuacha aondoke zake…….
Basi nikawa kama nimechanganyikiwa mume wangu akanambia kuwa nisiwe na mashaka maana watoto wameshakuwa hivyo tutatengeneza mazingira mazuri kuwa wakitoka shule kuna kitu wafanye, basi nikakubaliana na mume wangu kuwa hatuhitaji dada wa kazi tena na kama ni kazi basi tutakaa na kusaidiana kuzifanya pamoja mimi nay eye……..
Basi maisha yakawa yanaendelea, yaan asubuh nikiamka nikianza kuosha vyombo yeye anadeki, au unapika chai, au anaandaa watoto, hivyo tukawa tunafanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu, yaan mpaka nikaona maana halisi ya familia kupitia yenye umoja na mshikamano kama ya kwangu, ni kweli nilikuwa ni mwanamke mwenye bahati sana kuwa na mwanaume kama Kendrick na vile mimi ndio nimemtoa uvulana wake, nikawa najiaminisha kuwa alikuwa wa kwangu pekee yangu……..
Basi tumekaa kama miezi miwili tunaishi maisha ya kusaidiana, sasa siku moja ilikuwa ni jumapili, mama yake Kendrick alikuja na mwanamke , alikuwa anaonekana kama mwanamke flani hivi mashamba mshamba sana, mama yake akasema kuwa ametuletea dada wa kazi……..
Kendrick hakutaka ila mama yake akasisitiza sana, nikaona nimshawishi akubali tu, basi baada ya Kendrick kumkubali huyo mwanamke mama yake akaondoka, na tukaanza kuishi nae, Yule mwanamke alikuwa mshapu sana, yaan anafanya kazi dakika mbili ameshamaliza, kwlei akikaa hivyo kwa kama miezi miwili, na baada ya hapo nikashangaa anaamka mapema kisha anabandika maji jikon anamfata mume wangu na kumuambia kwa sauti ya mideko kuwa “ maji tayar baba…
Ingawa mume wangu alikuwa ni kijana mdogo ila hakuwa anaonekana kuvutiwa kabisa na namna ambavyo Yule mwanamke alivyokuwa anafanya, alikuwa haongei nae, mpaka siku moja akamfata na kumuambia “usipobadilika ndani ya siku chache, nakuahidi kuwa hii nyumba utaanza kuiona kama kituo cha polisi, kisha mume wangu akaondoka na kwenda zake kazni…
Yule binti aliona kama utani vile, akaanza kunikunjia mdomo na kuninyali kama hana akili, siku moja nikamsikia anaongea na simu, alikuwa anasema kuwa “ mama huyu mwanamke kweli kamloga mwanao, manaa kila nilalofanya bado naonekana mbaya, na ile dawa ulionipa amekataa kula, maana anasema anataka kula chakula ambacho amepikiwa na mke wake wa ndoa, na sio changu, mama tunatakiwa kufanya namna tumuondoe huyu mwanamke mchawi….
Nilijisikia vibaya sana, maana ni kweli mume wangu ananipenda sana, ila sikuwah kufikiria hata mara moja kama mama yake ananichukia kiasi kile shida ni umri au anasababu zake nyingine tu, sikumuambia mume wangu na wala sikutakja ajue, nilijiambia kuwa kama ni ukweli ni bora aje kuujua mwenyewe kuliko nianze kufarakanisha familia za watu, niliona kama sio sawa kabisa yaan….
ITAENDELEA………..
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments