Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

POOR RICHMAN* (Alijifanya amefirisika na Kuwa Masikini ili kuwajua wanafiki kwenye Maisha Sehemu Ya 9

9th Sep, 2025 Views 64



Harakati za kumuwinda mrembo huyo na mtoto pekee Wa Mr Tamir zilianza Huku Jovin akishirikiana vyema na keivo!.
Jovin aliona kuna ugumu kidogo kuifanya ile kazi wawili tu Yeye na Keivo kitu alicho kifanya ni kutafuta baadhi ya vijana walala hoi Wa mtaani aliwapa visenti kidogo na kazi yao ilikuwa ni kumpleleza Binti Huyo Wa Tajiri kila anapo enda!.

Mwezi Mmoja ulipita Huku Bado yule Binti akiwa anafuatiliwa Muno na vibaraka Wa Jovin, na kipindi hicho Jovin na keivo walikuwa wamehama pale walipo kuwa wanakaaa na kuhamia sehemu Nyingine.
Siku Hiyo mida ya Jioni wakiwa magetoni walipokea ujumbe!.

"Leo kwenye ukumbi Wa Millennium kuna tafrija Moja ya rafiki Yake na mtoto Wa Mr Tamir anasherekea Birthday yake, kwa taarifa tulizo zipata Hata mtoto Wa Mr Tamir atakuwepo na hii Ndo fursa pekee!" Huo ulikuwa ni ujumbe ambao Jovin aliupokea kutoka kwa Moja ya kibaraka Wake!.

"Oya keivo jiandae Muda Wa kwenda kufanya tukio! . Ebu mshitue na Saimon, mwambie awe Tayari Muda wowote tutampigia Simu!" Hayo yalikuwa maneno ya Jovin, na Huyo Simon alikuwa Dereva Taxi ambaye walikuwa washampanga Siku Nyingi, Japo kuwa walikuwa hawajamwambia ni Mtu Gani watamteka, ila walikuwa wamemwambia tu watateka mtu na Yeye Ndo itabidi Gari Yake itumike!.

Basi ni kweli kwenye Moja ya ukumbi maarufu palikuwa na sherehe za Moja ya mtoto Wa Tajiri pale Mjini, na mtoto huyo alikuwa rafiki mkubwa Binti Yake na Mr Tamir!.
Sherehe zile zilitamatika Mida ya Saa Sita Ndo Watu walianza kutawanyika! Basi Binti Wa Mr Tamir kama kawaida Yeye na Walinzi Wake Watatu walio Shiba walizama kwenye Gari ya kifahari na kuanza safari ya kurudi nyumbani!.

Walitembea umbali Wa kilomita kadhaa hivi, ilibakia kidogo wafike kwenye mjengo Wa Mr Tamir ambao ulikuwa mkubwa kama hekalu, Baada ya kuchepuka tu Njia Kuu na kukatiza Sasa Njia inayo elekea nyumbani kwa Mr Tamir gafla Gari ilikanyaga kitu chenye ncha kali na Tajiri za mbele zote zilipasuka!.
Ilibidi walinzi washuke kuangalia Nini Shida!.

"Uuuuu naona kuna kitu hapa, tairi zote zimepasuka, Madam kwa Sababu home Siyo mbali ungeshuka ili tutembee, maana naona mazingira Siyo rafiki!" Moja ya Mlinzi alizungumza! Huku akiwa naangaza huku na kule!.
Ni kweli mtoto wakike alishuka na alikuwa anajiamini kwa Sababu aliamini mbele ya mbavu zile hakuna Mtu atamchukua isitoshe ilikuwa ni Karibu na nyumba kwao, yaani ilikuwa ni kama mita mia tu kufia nyumbani kwao.
Walitembea hatua kama Tano hivi gafla waliona ni kama Mtu anakuja kwa mbele!.

"Jitambulishe mwenyewe kuna usalama??" Basi Mlinzi Mkuu ambaye Ndo alikuwa anamiliki Bastola kati ya Wale wote aliuliza Huku akimnyoshea yule Mtu Bastola!.

"Tafadhari wajukuu Zangu Mimi ni Mtu mwema tu!" Basi ilisikika Sauti kama ya Mzee ambayo ilifanya Yule bwana ashushe Bastola Yake akiamini ni raia mwema!.
Lakini Baada ya kusogeleana na Mtu Yule gafla alichomoa kitu kama Spray hivi Baada ya Hapo aliwapulizia walinzi wale kwa kuwashitukiza!, ilikuwa ni kitendo cha sekunde tu walinzi wale walijikuta wanalegea, yule mwenye Bastola akiwa anajitutumua kunyanyua Bastola ili ampige nayo Yule Mtu, gafla kuna Mtu akijitokeza kwa nyuma na kumgonga na kitu kizito!.
Yule Binti mtoto Wa Tajiri alijikuta haelewi afanye nini alianza kukimbia Huku akiwa anapiga kelele, lakini alikimbia hatua Tano tu alikamatwa naye pia alipuliziwa ile Dawa na kumfanya azime!.
Ilikuwa ni Dawa kali muno, maana kitendo chu kunusa harufu Yake ilikuwa unazima hapo Hapo!.

"Keivo Kazi nzuri! Haya tumbebe tuondoke naye!" Basi Jovin aliongea!

"Bro hii Bastola yao tunawaachia!?" Keivo aliuliza, basi ilibidi na ile Bastola waibebe na kuondoka Nayo!.
Masaa yalisogea hatimaye palikucha na kuwa asubuhi!.

Mr Tamir akiwa anapasha asubuhi kuuweka Mwili Sawa kwa kukimbia kimbia kabla ya kwenda kazini, alishangaa kuona walinzi Wa Binti Yake wapo chini hawajitambui kabisa, yaani walikurupuka Baada ya kushituliwa!.

"Heeeee Maiki Vipi Binti Yangu yuko wapi!? Mbona mpo hapa!?" Mr Tamir mapigo ya Moyo yakiwa yameanza kwenda kasi!, aliuliza!.
Vilikuwa ni vigugumizi tu kwa Wale walinzi maana nao walikuwa haelewi ilikuwaje kuwaje, yaani kilicho kuwa kinasikika ni neno Samahani Boss!.

"Nawapatia nusu Saa Binti Yangu awe amefika nyumbani lasivyo! Lasivyo! Hahaaa sielewi hata nitakacho wafanya!" Mr Tamir akiwa kachanganyikiwa aliongea, yaani Hata mudi ya kufanya mazoezi ilikata gafla alirudi nyumbani Mwili mzima ukiwa unatoa jasho kama Ndo kafanya mazoezi kumbe ni presha tu.

"Mume Yangu Mara Hii umefanya mazoezi au umeanza uvivu!?" Basi Baada ya kufika nyumbani alikuta Mkewe Bado kalala!.

"Kipenzi si Hawa wapuuzi akina Maiki nimewakuta wamezimia hapo Barabarani, nawauliza Binti Yangu yuko wapi wananitumbulia tu Macho!" Akiwa kachanganyikiwa Mr Tamir aliongea, kwanza Mke Wake pale pale presha ilimpanda Baada ya maneno Yale!.
Mwanama yule akiwa hajauliza vizuri Mara Simu ya Tamir iliita Namba ikiwa ni Mpya!.

"Mr Tamir Mimi Sina mengi na Sina Cha kupoteza kwenye maisha Yangu, nakupa Siku Moja tu ya Leo Hati Zangu zote na mihuri Yangu yote viwe vimerudi tena vikiwa kwa Jina langu, na cha Pili akaunti Yangu ya benki iwe inafanya kazi, na cha Tatu Sitaki uguse Mali yoyote iliyopo kwenye kampuni kuanzia Sasa mpaka akaunti za kampuni sitaki Ziguswe! Lasivyo kufikia kesho utaikuta maiti ya Binti Yako getini kwako, Sina mengi Mzee Ndo hayo tu! Sehemu ya kurudisha hati nadhani unaijua pale pale ulipo zitoa Ndo kazirudishe, cha Mwisho hii ibaki kuwa Siri Yako la sivyo Bora Wote tukose" Baada ya kupoke Simu Hayo Ndo maneno ambayo Mr Tamir aliyasikia!.
Kwanza Mke Wa Bwana Huyo alianza kutetemeka kwa presha Baada ya kusikia watakuta Mwili Wa Binti yao getini kwao!.

"Mume Wangu! Yote haya umeyataka Wewe na Tamaa Zako, nilikuonya lakini kuchukua Mali Mr Jovin kwa Sababu ni Mtu mwema tu, lakini Tamaa Yako tu, na hukuwa na haja ya kuchukua Mali Zake ikiwa unazo zako tena nyingi zaidi Yake! Ona Sasa Yote Haya! Nasemaje Binti Yangu akifa, Hata Mimi najiua!" Hayo yalikuwa maneno ya Mke Wa Mr Tamir akiwa kajawa na Jaziba na Mwili mzima unatetemeka.

Kwa presha ambayo Mama huyo alikuwa nayo pale pale alizimia, hakika Mr Tamir alihisi Dunia inazunguka, yaani jasho kwenye ukwapa lilimjaa haswa.

Je Jovin atafanikiwa kuzipata Mali Zake!? Je Mr Tamir atakubali kirahisi hivyo!?

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

POOR RICHMAN* (Alijifanya amefirisika na Kuwa Masikini ili kuwajua wanafiki kwenye Maisha Sehemu Ya 9  >>> https://gonga94.com/semajambo/poor-richman-alijifanya-amefirisika-na-kuwa-masikini-ili-kuwajua-wanafiki-kwenye-maisha-sehemu-ya-9

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest