Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 π’•π’˜π’ πΏπ‘œπ‘£π‘’π‘†π‘‘π‘œπ‘Ÿπ‘¦.....: 𝐋𝐀𝐒𝐓 ππŽπ‘π 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ π‡πŽπ”π’π„ π†πˆπ‘π‹ (π™‰π™™π™žπ™«π™– π™‰π™œπ™ͺ𝙣𝙙π™ͺ) 𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 π‘Ίπ’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š EP 03

11th Sep, 2025 Views 45


Wale wanawake majirani hawakuweza kujibu Chochote walitoka kimya, Fina alikuwa anacheka ile kinafiki, haijulikani kwanini afanye hivyo

Ray alibaki akiwa na Nasma pale ndani hata hivyo alimtazama kwa mshangao bila kuongea chochote halafu akainuka, Ray akajua hapo kuna tatizo

Ray alitoka hadi nje ya chumba akatembea mpaka getini kisha akamkuta Karimu akiwa anaongea na simu pale nje. Alimsubiri akamaliza kuongea na simu

"Karimu" Aliita Ray

"Ee"

"Nambie ukweli, kipi kilichotokea"

"Mh daah" Karim aliguna kwanza huku akionyesha tabasamu Fulani hivi "Broo" Alisema Karimu

"Nambie mzee mbona unaguna mke wangu kapigwa na nani mbona sielewi?"

"Hama Hapa unapoishi Bro, la sivyo utapitia magumu sana" alisema Karimu

Ray alitazama akapata wazo
"Daaah Kuna kitu nimeelewa" alisema

"Nini" Karimu aliongea

"Rose" aliongea Ray

"Kama ulikuwepo man, Rose kaja na visichana kama nane hivi hapa wamempiga mkeo, tatizo naye ni mpole sana mzee"

"Nikuambie kitu Karimu?" Alimuuliza

"Yap boss"

"Ntamuua Rose" Aliongea kwa hasira macho yakiwa makundu, halafu akaingia ndani ya geti na kusogea mpaka chumbani akaingia, ndipo alipomkuta Nasma amesimama chumbani anawaza sana huku machozi yakiwa yamekaukia kwenye shavu

"Nasma" aliita Ray akamsogelea na kupiga magoti "Nisamehe Nasma" Aliposema hivyo ndo kabisa Naa alilia kabisa kwa uchungu huku akifoka kwa sauti

"Kumbe unalijua kosa lako Ray, kumbe wewe ndo umetuma wanawake wako, ahihiiiih" Alilia kwa uchungu na kuketi kitandani

"Acha kuongea kwa sauti ngoja Nikuambie yule sio mwanamke wangu Nakuambia kweli" Ray alisema huku akimsogelea na kumshika mapajani

"Usinishike" Aliongea binti kwa hasira huku akiishika mikono ya Ray na kutaka kuitoa lakini Ray aliikaza wakabaki wameshikana

"Nasma, yule tuliachana muda sana, ni wivu wake kisa kaona wewe ni mzuri zaidi yake

"We Muongo Ray" Alisema binti

"Nakupenda, na ntahakikisha hili halitotokea tena, umeumia sana?" Ray aliuliza na kuinuka akaketi pembeni mwa binti huku akimkagua majeraha

"Nimeumia kwa sababu yako, nataka twende hospitalini" nikatibiwe

Ray alimtazama usoni "Kweli?" alisema akiwa anatabasamu kwa furaha hakuamini amesamehewa, Naa alitikisa kichwa "Ok Jiandae niko nje na Karimu, ok??"

"Sawa"

Ray aliinuka na kugeuka huku akiitoa simu mfukoni na kuiwasha halafu akatazama kama kuna ujumbe au la, alitembea mpaka mpaka nje huku akiitazama simu yake kwani kulikuwa na jumbe kutoka mtandaoni kwamba mama yake amempigia mara tatu pamoja na dada Anita akiwa anataka kuujua umbea

Ray alikuwa anataka kumcheki Karimu lakini alimkosa pale nje ikiwa ameshaondoka Karimui

Ilibidi Ray ampigie simu lakini Karimu alikuwa bize akiongea na simu nyingine, akaachana na hiyo Mada

"Phina" aliita Ray kwa nguvu "We Phina" aliita tena

"Abee" Phina alitoka chumbani kwake na kusogea getini

"Samahani nikuulize" alisema Ray

"Nini..." aliuliza kwa wasiwasi Fina akijua labda jamaa ameshamshtukia "Usije ukanihisi vibaya mimi sijampiga mkeo" alisema binti

"Najua sio wewe but ni Rafiki yako, I'm sure kwamba ulikuwepo tangu hii ishu ikitokea sasa embu nielezee ilikuwaje"

"nilikuwa ndani, nikasikia kelele tu nje, kutoka hivi, mabinti kibao wanamshambulia mkeo" alisema

"For what now?" aliuliza kwa hasira

"Sijui mimi, embu niache kidogo, mtafute Rose muulize"

"Daah yule mwanamke kumbe ni mbwa, yaani nikimkuta nampigia mamae" alifoka kwa hasira kijana Ray maana alikuwa amekasirika sana "Ok powa Phina" aliongea Ray na kurudi chumbani ambapo alimkuta Naa akiwa anajitizama kwenye kioo cha kabati Majeraha yalikuwa mengi usoni ndipo alipomtazama Ray huku machozi yakimlenga lenga

"Ray"

"Usilie Nasma, aammh unaj...." alisema ila binti akamdakia juu juu

"Unanipenda?" aliuliza

"Yap" Ray alisema akitikisa kichwa kisha akatembea na kumkumbatia kwa nyuma

"Basi kama unanipenda tuhame hapa" alisema binti

"Mmmh, unajua la...."

"Sitaki maelezo mimi kama ndo hivi narudi kwetu" alisema na kujinasua kifuani mwa mtaalam na kuketi kitandani kwa hasira na kushika tama

"Sorry....nisamehe mimi"

"Tuhamee" alisema kwa kiburi maana alijua anapendwa"

"Ok, basi sawa" alisema Ray

Simu ya Ray ilianza kuita na kuitoa mfukoni akatazama hivi ni Da Anita anapiga...ITAENDELEA

𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 π’•π’˜π’
πΏπ‘œπ‘£π‘’π‘†π‘‘π‘œπ‘Ÿπ‘¦.....: 𝐋𝐀𝐒𝐓 ππŽπ‘π 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ π‡πŽπ”π’π„ π†πˆπ‘π‹
(π™‰π™™π™žπ™«π™– π™‰π™œπ™ͺ𝙣𝙙π™ͺ)
𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 π‘Ίπ’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š

EP04
"Huyu Naye anataka kuniambia nini" Ray aliongea kwa sauti ya chini Nasma akachukua jicho lake paap na kulizungusha kutazama kwenye simu kwa ajili ya kuyalinda mahusiano yake, alipokuta imeandikwa Dada Anita, alitulia kimya, Ray akapokea

"hallo"

"Hallo shikamoo Da Anita" aliita

"Marahaba hahahaa Ray hahah" alikuwa anacheka Ray akabaki ameshangaa

"Vipi mbona unacheka" aliuliza

"Mh, Hapana Ray we muhuni sana" alisema Anita

"Uhuni wangu nini?" aliuliza

"Hahaa, yaani ukaamua kutoroka na Housegirl, kweli wewe ni hatariiii"

"Mh" Ray aliongea na kukata simu halafu akamgeukia Nasma, Nasma alishtuka kidogo

"Vipi kuna tatizo?"

"Nope, jiandae twende zetu"

"Hapana, huyo uliyekuwa unaongea naye nani?" Aliuliza Naa

"Da Anita mtoto wa Ma Mkubwa....tuondoke" alisema

"Sawa, but Umekula wapi leo mbona sikuelewi"

"Ah mmh, hivi ulipika ee embu nipe Chakula nile kwanza, sijala"

"Hahahaha, unachekesha" Binti aliongea kwa jeuri fulani hivi, kisa Ray hajala hadi akumbushwe, alipakua chakula mwenyewe kwenye chombo halafu akala pale pale kitandani na kugeukia nje

Aligeuza macho akala haraka haraka halafu akainuka na kuanza kutembea kuelekea mlangoni "Twende Hospitali" aliongea

Cha kushangaza ni kwamba Nasma hadala ainuke kwenda hospitali ndo kabisa alijilaza kitandani na kugeukia ukutani

"Vipi mbona unalala tena"

"Niko sawa, sina Maumivu na siendi popote nalala zangu"

Ray aliposikia maneno hayo alimtazama binti kwa hasira mpaka pua na mdomo vikawa vinacheza cheza kwa hasira kali sana.

Ray alifanya akama anafyonza kiume ile "Dhyaah" halafu akatoka nje bila kuongea chochote.

Alitembea mpaka nje ya Geti ndipo akarudi na kuchukua pesa pamoja na Earphone halafu akatembea kuelekea mtaani kuzurura, alikuwa ana hasira sana

Ray alitembea tembea mpaka Maeneo Victoria, alipofika akasimama na kupata wazo aende kwa Karimu lakini hakutaka kwenda bila kumpigia simu "Oi Kerry" alisema

"Hahahahaaaa" Karimu alicheka kwa nguvu

"Unacheka nini mzee?" aliuliza

"Hiyo Kerry ndo maana yake Karimu sio, basi umenipa bonge la AKA leo man" alisema Karimu

"haha okay naibuka hapo sasa hivi"

"Sipo magetoni"

"Uko wapi?"

"Temeke Mikoroshini"

"Humo humo naibuka mzee baba" aliuliza mtaalam

"Haina noma"

Ray alipanda gari, kama mbili hivi halafu akaenda pale alipokuwa Karimu, alimkuta Karimu akiwa anakunywa Pombe, alipendelea sana kunywa Castle lite, ama Serengeti lite, Ray alikuwa sio mlevi kabisa

Ray alipofika eneo lile aliketi, kulikuwa na washikaji kibao, lakini Ray kwa utoto wake eti alikuwa na Stress zake kuhusiana na Nasma

"Ningekuwa mnywaji leo ningelewa sana" alisema Ray

"Kisa nini, lile tukio ama?" Karimu aliuliza

"Boy bora lile yaani kuishi na mwanamke ni shughuli sana" alisema, Mara muhudumu akamletea Coke baridi

"Kwani vipi"

"Eti kananiletea kiburi kale kademu hakanijui mimi vyema Sio?" aliongea kwa hasira na Kunywa Soda mara moja "Man namuambia tuende hospitali, halafu anajilaza kitandani et 'SIENDI POPOTE MI NIKO SAWA'" Aliongea Ray huku akiwa ameweka kidole kwenye pua kumteta

"Hahaha, Ray" Aliita Karimu huku akiweka mkono mezani kama mwalimu anayeuliza ada ya mtoto "Hilo tu linakupa stress???" alisema "BADO HUJAONA CHOCHOTE.....Utalewa lazima unywe pombe Nakuambia" alisema Karimu

"Daaaah" Ray alipata hasira

"Usiseme Dar, Dar kubwa hii, wewe vunga kama huelewi ila si una miaka 24, we subiri boss" Alisema Karimu na kupiga glass mdomoni akanyonya bia...JE RAY KAONA LOLOTE KWENYE NDOA HAPO?.
Kwa sh 1000 unamaliza season two
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 π’•π’˜π’ πΏπ‘œπ‘£π‘’π‘†π‘‘π‘œπ‘Ÿπ‘¦.....: 𝐋𝐀𝐒𝐓 ππŽπ‘π 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ π‡πŽπ”π’π„ π†πˆπ‘π‹ (π™‰π™™π™žπ™«π™– π™‰π™œπ™ͺ𝙣𝙙π™ͺ) 𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 π‘Ίπ’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š EP 03  >>> https://gonga94.com/semajambo/season-two-lovestory-last-born-na-bikira-ya-house-girl-ndiva-ngundu-burudan-simulizi-ep-03

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest