. Hakuna aliyemshika mkono, hakuna aliyemtongoza, wala kumsifia hata siku moja. Kila mtu alimuona kama kichekesho.
Yeye mwenyewe alishazoea kuitwa majina ya ajabu, lakini moyoni kwake kulikuwa na maumivu ya kisirisiri. Aliwaza, Mbona mimi pia ni binadamu, mbona wao wanafurahia maisha yao na mapenzi yao, mimi nikibaki tu kama kipande cha sofa? Duh.
Siku moja, demu akajikaza kiume, akasema apate presha ya maisha. Akajitosa kwenda kuogelea kwenye swimming pool ya mtaa wa mabazu, akijua pengine maji yangeosha maumivu yake.
Lakini mbona? Balaa lilimkuta. Kundi la madada wa kisela, wenye roho za shetani, wakamnyemelea. Wakaanza kumrekodi live huku wakimcheka, kumshusha, wakimwambia hafai, wakimwita Titanic iliyojaa maji.
Cha ajabu zaidi, walimchukulia nguo zake zote. Yaani demu kabaki mtupu katikati ya umati, na video tayari ipo TikTok, watu wanacomment bila huruma.
Sara alijikuta anazidi kuvunjika moyo, lakini kilichowashangaza wengi, kulikuwa na jamaa mmoja pembeni, alishuhudia yote. Jamaa huyo hakucheka kama wengine. Alimuangalia Sara kwa jicho la tofauti, kama vile alikuwa anaona almasi kwenye vumbi..
Baada ya lile tukio la pool, Sara alitoroka fasta kwa taulo moja tu alilokuwa kapewa na mlinzi wa eneo. Huku machozi yakimtoka, alijisemea:
Mbona watu wana roho za paka? Mimi nimewakosea nini hadi wanifanyie hivi?”.
Akafika home, akajifungia ndani kama wiki nzima. Hakutaka kuongea na mtu, hata wazazi wake waliona kabisa mtoto wao anadidimia kisaikolojia. Lakini usiku mmoja, akatumiwa meseji isiyo na jina,
Nimeona yote. Usijione uko peke yako. Kuna mtu anakutazama tofauti.
Sara akaanza kuchanganyikiwa. Moyo ukamdanganya kuwa labda kuna jamaa kavutiwa na uchungu wake, lakini akajikaza: “Haya mambo ya mapenzi kwa mtu kama mimi ni kama kutamani mwezi.
Siku ya pili, akiwa anatoka kidogo kwenda duka la jirani, yule jamaa akajitokeza. Jamaa alikuwa mpole, anavyoongea haongei kama wanaume wasiwo wa mtaa.:
“Mimi naitwa Max, na tangu siku ile nakuona, sijakupoteza akilini. Hawa wanaokucheka hawajui dhahabu wanayotupa.”
Sara akashtuka lakini moyo ukamshtua. Kwa mara ya kwanza akaona kuna mtu anamwangalia bila huruma wala dharau. Wakaanza kuonana mara kwa mara, na polepole Sara akaanza kurudi kwenye furaha.
Sara akiwa hajui kinachoendelea, bado alikuwa anaamini Max ni msaada pekee alioumbiwa na Mungu. Jamaa alimpa faraja, akamrekebishia hata self-esteem iliyokuwa imesambaratika kama kioo kilichodondoshwa.
Follow channel zetu watssap
https://whatsapp.com/channel/0029VbAynWb7IUYY5Bfgwj2j.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments