Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

UMENIBADILISHA WEWE 01___05 Mpendwa msomaji Leo na kuletea kisa hiki kinachokwenda kwa jina /Umenibadilisha wewe)

18th Sep, 2025 Views 13

hiki ni kisa ambacho kitakufunza mengi ukiwa Kama kijana, binti, mzazi na mlezi,.....wewe uliye kwenye ndoa na hata wewe unaetarajia kuingia katika ndoa.. ......... karibu tujifunze pamoja na kufurahi pamoja

UMENIBADILISHA WEWE

Sehemu ya 1

Katika nyumba moja alionekana kijana akipanga nguo kwenye begi alipomaliza alichukua begi hilo akatoka nje na kuliweka kwenye gari kisha na akaingia kwenye gari na kuondoka.

"Hallo Joel make sure nafika hapo nikute uko tayari"

Aliongea kijana yule na kukata sm

Aliendesha kwa mda wa dakika 30 akawa amefika sehemu husika , geti lilifungulia akaingia na kupark gari akashuka na kwenda moja kwa moja ndani

JOEL:"aa time keeper kama kawaida yako ushafika on time"

"Utaendelea kuongea tupoteze mda au utaweka vifurushi vyako tuondoke"

"Bro taratibu basi kwani tunaenda kwenye misa ya ndoa kwamba tukichelewa utakuta padri kaondoka"

Chris aliona kama joel anamchelewesha alichukua mizigo yake na kuweka kwenye gari wakaingia na safari ikaanza..........

msomaji /msikilizaji CHRIS NA JOEL ni marafiki walioshibana toka enzi hizo za utotoni hadi hivi leo,
siku hii ya leo
walikuwa katika safari ya kuelekea mkoani mwanza ambapo ndio nyumbani kwao, Waliamua kutumia usafiri binafsi kwa sababu zao wenyewe.

Kwakuwa walikuwa wawili ilikuwa ni story na music kwenda mbele .......mida ya saa mbili usiku Joel akiwa anaendesha waliona gari limepaki pembeni huku mdada asimama karibu na bara bara akisimamisha magari lakin yalikuwa yanapita kama yamuoni .

"Oya huyu demu au jini kulikon saizi amepaki na anapungia mkono magari yasimame au traffic sikuhizi wanavaa kiraia"aliongea Joel

"Mimi nadhani atakuwa anashida labda gari lake limehariba"

"Mmmmh sidhani mambo ya bara barani huwa hayaeleweki "

"Embu mpite alafu ukasimame mbele "

"Nisimame ili tufanyeje"

"Tujue huenda anatatizo"

"Oya Chris achana naye kama ni jambazi je"

"Aaaa jambazi awe yule"

"Umeanza ubishi wako mimi sisimami kama anashida atasaidiwa na wengine sio sisi"

"Oya Joel simamisha gari "

"Chris tunawezaje kusimamisha gari kwa mtu tusie mjua"

"Uliambiwa usaidie unaowajua tu? Hembu simama ".........

Joel baada ya kuona Chris amekazana kumwambia asimame alisimama Kisha Chris akashuka

"Baki kwenye gari" aliongea Chris na kuondoka kuelekea kwa yule dada.

Dada yule alipomuoan Chris akataka kuvuka bara bara Ila Chris alimuonesha ishara abaki pale pale atamfuata.

"Mambo" alisalimia baada ta kufika

"Poa kaka "

"Vp unatatizo"

"Ndio gari limenizimikia na kama unavyoona hapa niporini kibaya zaidi sm yangu imezima yaani nimechanganyikiwa sijui hata nifanye nn "

"Okay pole sana aaa ngoja tuone Kama nitaweza kukusaidia"..

"Asante sana kaka yangu Mungu akubariki Sana"

"Haha hahaha unabariki hata kabla sijatengeneza kama nikishindwa je"

"No naamini utaweza "

"Haya ngoja tuone "

Alisogea kwenye gari na kuanza kukagua ili kujua nn shida mda huo Joel Bado yuko kwenye gari .

Chris alihangaika karibu nusu saa nzima bila kujua shida ni nini akaamua kumuita Joel ajae wasaidizane ili wawahi kumaliza hata hivyo Joel alikuwa mtalamu sana kuliko Chris

"Oya yaani umelala kwa amani kabisa mtu wangu"

"Sasa ulitaka nilale kwa ugomvi au'"

"Sasa unalalaje wakati mimi sipo"

"Acha zako siumeenda mwenyewe ulitaka nifanye nin "

"Okay tuachane na hayo twende tukamsaidie kutengeneza gari "

"Tushakuwa mafundi tena "

"Joel bwana acha hizo mtu anahitaji masaada sana tumsaidie then tuondoke "

"Bro hizi huruma zako zitakuja kukuponza ujue, hivi ni mjinga gani anaweza kusafiri safari ya mbali kiasi hiki bila kucheki gari lake kam liko sawa"

"Mistake zinatokea bhn we tumsaidie basi "

Ilichukua mda Joel kukubari lakin mwisho alikubari walimrekebishia gari lake hatimae lilikaa sawa

" asanteni sana kaka zangu sijui bila nyie ningefanya nn, Mungu awabariki sana "

"Urudie siku nyingine ee"
Joel alimjibu na kuondoka

Chris:"Usijali ila next time uwe makini sawa ee"

"Sawa kaka yangu asante sana"

"Haya safari njema"

"Na nyie pia"

Baada ya kuagana Kila mtu aliendelea na safari yake


Baada ya safari ya mda mrefu hatimae waliingia jijini mwanza kwakua ilikuwa ni usiku sana na hawa kuwapa taarifu nyumbani waliamua kulala hotelin.

UPANDE WA PILI

Yule binti alifika nje ya nyumba na kupiga honi

Geti likifunguliwa Kaingia na kupaki gari akashuka na kuingia ndani

Aliwakuta watu wamekaa seblen akawapita na kwenda moja kwa moja na chumbani kwake bila hat kuwasalimia

"Unaona mwanao alivyo na dharau yaani tumekaa hapa na presha juu kwasababu yake alafu anapita kama hajaona mtu "

Alilalamika binti mmoja aliyekuwa amekaa na mmama wa makamo

"Atakuwa kashavurugwa kichwa chake si unakijua vizuri "

Waliinuka na kwenda chumbani kwa binti yule

"We Nanah ndio tabia gani hii unayotuonesha, na ilikuwaje ukawa hupatikani kwenye sm"

"Mom please naombeni mniache yaani hapa nimechoka hadi naona kero kuongea kwaiyo hayo maswali yenu ya hifadhini vizuri mtaniuliza kesho"

Aliongea Nana na kujifunika shuka mwili mzima

"Hahahahahaha mwana kulitafuta mwanakulipata ulikuwa unaona kuendesha kutoka mwanza hadi hapa ni kama temeke na kigamboni eee, alafu ukawa unajisnap mwenyewe raha kama zote ukome"

"Bella niache nipumzike basi "

"Fine usiku mwema "

"Zima taa"

Itaendelea.....

UMENIBADILISHA WEWE

SEHEMU YA 02


Nana aliamka asubuhi akachukua sm yake na kumpigia Dada wakazi amletee chai


Nana ni mtoto wa pili wa mzee Leonard huku dada yake wa kwanza alikuwa anaitwa Nora

Familia ya mzee Leonard ilikuwa ni familia yenye uwezo mkubwa kifedha
Katika familia hiyo walijaliwa watoto wawili tu

"Ingia " Nana alimruhusu dada kuingia

"Za asubuhi dada"

"Nzuri "

"Karibu chai"
"Haya weka hapo kwenye meza alafu ukatoe begi la nguo liko kwenye gari ukimaliza unipasie nataka kutoka ".

"Sawa dada"
Mda huo huo akaingia Bella(binamu yake)

Bella: "Dada wa taifa naona umeshaamka "

"Wewe tena Nilijua tu lazima utakuja asubuhi asubuhi "

Bella: ""Ulitaka nije usiku usiku, hembu tuachane na hizi mh nambie ilikuwaje Jana ukakosekana ghafla alafu umefika mda umeenda kuliko tulivyo tegemea "

" Subiri kwanza ninywe chai ili nipate nguvu za kukueleza vizuri "

Alichukua chupa na kufungua akamimina "huyu mpuuzi leo tena hajaniwekea mdalasini hivi ngoja magee we mageeee"

Mage alikuja akikimbia"abee da" hata kabla hajamaliza kuongea Nana alimmwagia ile chai usoni

"Aaaaaa" mage alipiga kelele na kujishika usoni

"Huu ni upuuzi gani kwanzia lini mm nikanywa chai isiyokuwa na mdalasini "

Bella: ", Nana pun"

"Kaa kimya Bella huyu mjinga hasikii hii ni mara ya pili ananiletea chai isiyokuwa na mdalasini wakati anajua ni lazima kuweka mdalasini kwenye chai yangu"

Mage: "Nisamehe dada ila baba ndio alisema leo nisiweke ndio maana sijaiweka"

"Kwaiyo kama amesema usiwe ngoja " aliinuka na kutoka chumbani kwake akaenda chumbani kwa wazazi wake .

Bella :"Pole sana nenda kapake asali mapema " mage aliondoka na kuacha vyombo mle chumbani

Nana alifika chumbani kwa wazazi wake hakutaka hata kugonga alifungua mlango na kumkuta baba yake akifunga vifungo vya shati

"Baba ndio umefanya nn kwann umemwambia Mage asiweke mdalasini kwenye chai"

"Nimemwambia asiweke kwenye chai yangu siyo ya kwenu"

"Sasa kajifanya mjinga kachemsha ya wote"

"Ooo nasikia jana umerudi saa nane"

"NDIO naondoka kwenda kunywa chai nina njaa"

Alitoka na kumuacha baba yake akimuangalia, alifika chumbani na kukuta mrafiki zake wamekuja

"Nyie vp mbona mnavamia chumbani kwangu mapema yote hii"

Lizzy: "Wewe tena ulitaka tukae makwetu wakati umetulaza tumbo joto,kwanza ilikuwaje ukawa hupatikani"

"Eee nyie yaani Kila mtu yuko roho juu kama vile mimi ni mkuu wa nchi embu mniache nipumue kwanza khaa"

Nancy: "Bwana Nana Acha matani Sema ilikuwaje"

"Khaa nyie embu tulizeni makwomwe yenu kwanza, Mage we mageee embu njoo hapa '"

Bella: "Mh unavyomuita huyo mage kazi anayo"

"Bella usinichokonoe we kaa kwa kutulia"

Mage :"Abee Dada "

"Chai yangu iko wapi alafu mbona umefua nguo nusu na hizo chupi unamwachia nani afue ,na nilikwambia ukatoe begi kwenye gari silioni hapa inamaana hujatoa sio "

Mage; "Ndio dada nilikuwa na"

"Hembu toa hizo chupi haraka na ufanye haraka kuniletea chai uwaletee na wengine Kwanza nguo zangu umeshapasi?"

Mage: "Hapana dada "

"Hivi humu ndani unafanya kazi gani paka wewe maana Kila kitu hadi ukumbushwe mbona kula hukumbushwi
Sasa ole wako ifike saa nne hujamaliza kazi zangu utarudi huko usukumani kwenu ukachunge ng'ombe mjinga sana mfyuuu"

"Sa"

"Mageeee"

"Nenda huko mama anakuita ,Enhe sasa niwape ubuyu wa kilichotokea Jana "

Lizzy:"Embu subiri kwanza hivi Nana unawezaje kumfulisha mtoto wawatu michupi yako kwamba wewe hujui kufua"

"Lizzy umeanza mambo yako embu niache sitaki ugomvi saizi, enhe Jana saa moja jioni nikiwa katikat ya pori sangp gari lisiharibike na kibaya zaidi sm ikazima chaji"

"Haaaaa๐Ÿ˜ฎ ikawaje "waliongea wote kwa pamoja

"Si ndio naeleza jamani watu macho yamewatoka kama mna tunga Uzi kwenye sindano nyie tulizeni vishundu vyenu niwaambie, sasa bwana nilisimamisha magari lakin hakuna gari lililo simama hadi inafika saa mbili ndio gari moja hivi lika simama, embu ngoja ninywe maji kwanza mageeeee niletee maji yakunywa,
Aaaaa sasa hapa Koo liko vizuri , naomba mnipe masikio yenu maana hili ninalolisema linauzito aswaaa,

Nancy: "Shoga we ongea tunakusikiliza"

"Basi kwenye lile gari alishuka mkaka nyie gonja nikae vizuri yaani hapa kama namuona vile ๐Ÿค— Iko hivi alishuka mkaka mmoja hivi yuko hot hivi mnajua hot, mtu asimfananishe sijui na jux au Frank wa jua Kali no yule nimoto nyie mkaka ni mzuri hadi anakera kwaza yuko smart alafu nimrefu mweusi kidogo mweupe kidogo mwili wake sasa uwiiiii


Nitarudi ngojeni kidogo

UMENIBADILISHA WEWE.

SEHEMU YA 03

"ana mwili hivi amazing alafu kilichoni changanya kuliko vyote sauti dah jamani huyo mkaka anasauti tamu nyie yaani alivyoongea tu nikahisi hadi kinembe kinacheza "

Bella: "Aaaa huo ni umalaya sasa khaa yaani mtu anaongea tu alafu unanyegeka"

"Bella na wewe funga bakuri lako mimi Bado naongea alafu unanikatisha muone sura yake cheeeefu๐Ÿ˜"

Bella: "Haya ongea"

"Alafu ananukia sio poa kiufupi ngoja niishie hapo nisije kujimaliza ila mkaka yuko poa sana "

Bella: "Ujimalize mara ngapi "

Nancy: "Bella na wewe Acha zako bhn, mh kwaiyo ikawaje "

"Alikuja akaangalia gari langu then akaenda kumuita rafiki yake wakatengeneza walipomaliza wakaondoka tena hata bila kuomba no kimeniuma basi"

Lizzy : "Wewe tena kwaiyo ulitaka namba yake ya nn wakati una bwana wako "

Bella : "ana bwana au mabwana ?"

"Bella na Lizzy mmeanza naomba msinitibue sawa eee"

"Haya dada"waliongea kwa pamoja na kukaa kimya

Nancy: "Mimi nahisi huyo kaka atakuwa anafanana na hemed maaana unamsifia kama yeye vile"

"Hemed gani yule mwenye sura nzito kama wimbi la uji"

Bella: "Khaaaa leo hii Kawa na sura nzito kama wimbi la uji wakati juzi juzi tu ulikuwa lunakufa kufa kwa ajili yake"..

Lizzy: "Mimi nikiwambiaga huyu ni rahabu mnakasirika haya leo kaka wawatu Kawa wimbi la uji ๐Ÿ˜‚"Lizzy aliongea wote

Nancy: "Nyooo we mwenyewe Hawa kuangusha watoto wawatu dhambini"........

Bella: "Kwani Hawa na Rahabu si ndio wale wale yaani wote mbuzi tu sema wametofautiana viungo Hawa ni kichwa Rahabu ni mkia ๐Ÿ˜‚" Bella aliongea na wote wakacheka ..


"Nyie zimepita dakika 10 huyu mpuuzi hajaleta chai, weee Mageee "

Mage: "Abee Dada "

"Shenzi wewe hiyo chai unatoa kijijini kwenu au"

Mage: "Naleta "

Lizzy: "Ila Nana hii tambia ya kumtukana mdada wawatu sio nzuri kwani huwezi kuongea nae kwa upole jamani."

"Weee Lizzy unikome hapa ni kwetu na yeye nikijakazi kwaiyo hizo swaga zako peleka kwenu ukija hapa tuliza komwe"

Lizzy: "Haya bhn,mh leo tunaenda wapi'"

"Nawasikiliza nyie "

Bella: "Naona leo twende shopping siunajua tunatakiwa kumsindikiza G kununua vitu na harusi yenyewe inakaribia"

"Weee tena umenikumbusha,ngoja nimuwahi huyu mzee Leonard kabla hajaondoka "

Nana Aliinuka na kwenda chumbani kwa wazazi wake

"Baba naomba Hela ya shopping "

"Shingap "

"Million 4"

"Nakutumia sasaiv "

"Haya"

aliondoka na kurudi chumbani kwake

"Usiniambie umetoka kuomba hela" Lizzy aliuza

"Sasa ulitaka nikaombe vuzi we vp "

Nancy: "Ila Lizzy unamwaswali ya kijinga mda mwingine"

Lizzy: "Heeee ya kijinga kivip mimi nimeuliza kwasababu najua anapesa ya kutosha kwenye account yake sasa nikosa
au"

"Aaaaa bwana hta kama Hela Iko kwenye account muhimu kuomba siunajua watu wenyewe wameshazeeka hapo wanasubiri kudanja tu kwaiyo lazima tutumie fulsa "

Lizzy: "Hongera sana"

Nancy: "Asante ila Lizzy punguza shobo rafiki yang yani kitu hakikupiti"

Lizzy. : "Heee kinipite hiyo kwema "


Mage: "Dada baba amesema nikupe hii"

Nana alipokea na kupiga kelele za furaha

"Weweeeeeeee this is my Daddy,yaani nimemuomba million 4 kanipa hundi ya million 7 just imagine eeee "

Nancy: "Wee hembu leta tuaone,
waooo hongera bestie ""

"Thanks guys,sasa tunywe chai chap alafu tuondoke "

Lizzy: "Ila Nana wazazi wako wanakulea vibaya sana kwa mtindo huu sijui labda wakutengenezee mwanaume wao ila sio kwenye hii Dunia "

Nancy: "Hivi Lizzy we unashida gani yaani Kila kitu kwako kibaya "

"Nancy mkaushie kwani humjui Lizzy wewe yeye Kila kitu kwake kiko hivyo,labda nikwambie kitu kimoja Lizzy kama wewe wazazi wako hawakupi vitu kama hivi pole yako ila sitaki Kila muda kuongea kitu chochote kinachuhusu wazazi wangu "

Lizzy: "Haya bhn sorry "

Walikunywa chai Kisha wakaondoka


Itaelendea

UMENIBADILISHA WEWE


SEHEMU YA 04


Ilipita wiki moja siku hiyo walitoka Nana na Lizzy

Wakaenda kupata chakula Cha jioni moja kati ya hotel flani hivi

Wakiwa wanasubiri chakula Nana alimuona Chris akiwa amekaa upande wa pili huku akiwa na watu kadhaa

"Wewe yule kaka alie nitengenezea gari yule pale"

Lizzy aligeuka na kuangalia
"Yupi"

"Yule alievaa shati la dark blue "

"Mr Chris?"

"Unamfahamu?"

"Ndio kwani nani asie mfahamu si ni CEO wa kampuni Ya HPL

"Weeee huyu ndio mmiliki wa ile kampuni"

"Acha kuniigizia bhn kwani ulikuwa hujui"

"Lizzy mimi ningejuaje"

"Basi ndio hivyo alafu nasikia pia ameajiliwa serikalini kwenye sehemu flan hivi nyeti"

"Usiniambie kumbe yuko na maokoto ya kutosha alafu anajiweka kawaida tu"

"Umesema wewe huyu kaka anapendwa na Kila mdada hapa mjini sasa jichanganye Kam hatujakuzika"

"Mfyuuu eti nizikwe wakuzikwa niwe mie"

"Haya Sema ni gentleman alafu yuko humble sana "

" huyo ndio mzuri sasa'"

"Wewe ten una hitaji maombi sio bure "

Wakati wakiwa wanongea waliona Chris akiamka na kuondoka

"Wewe bye tutaonana kesho"

"Unaenda wap sasa "

"Namfata Chris "

"Unawazimu wewe "

"Sawa tu unataka nikae hapa ili iweje"

Nana aliongea na kuondoka haraka

Alifika nje na kumuona Chris akiwa bz kuongea na sm haraka akapata wazo

Alienda na kujifanya anampamia bahati mbaya

"Ooo sorry sorry "

"It's ok niko sawa'"

"Chris aaa wewe nice to meet again"

Chris alikunja ndita kidogo huku akijaribu kukumbuka kama amewahi kumuona sehemu yoyote

"Aaa samahani tumeshawahi kuonana "

"Yes mimi ni yule msichana ulie nitengenezea gari wiki kama moja hivi iliyopita

"Ooo sorry nimeshahau,vp unaendeleaje"

" Namshukuru Mungu naendelea vizuri vp wew"

"Niko poa,aa! kama hutojali naweza kwenda Kuna mahari nawahi mara moja"

"Haina shida, unaenda njia Ipi maana nilikuwa naomba lift"

"Aaa sorry ninakoenda ni mbali kidogo alafu nina haraka sana"

"Okay haina shida asante "

Chris aliingia mfukoni akatoa not 5 za elfu kumi akampa na kusema

"Unaweza kuchukua Uber "

"Aaa no Haina shida nitachukua mwenyewe tu"

"Okay bye"alirudisha Hela yake na kuondoka

"Vp mbona umerudi "

"Mpango wangu umefell ila nimefurahia kumuona "

"Ngoja nile zangu maana nikiongea hapa kuna mtu atashindwa kula"

"Tena Bora ukae kimya tu"

Walikula Kisha wakarudi nyumbani

Chris alifika nyumbani akawa anaongea kwenye sm na Joel

"Bro hivi unaweza kufikilia kuwa leo nimekutana na yule msichana tuliemtengenezea gari "

"Msichana gani tena"

"Yule kipindi tunaenda mwanza si wiki tu imeisha"

"Aaa nimemkumbuka umekutana nae wapi"

"Nimekutana nae hotel wakati nimetoka kwenye kikao".

"Imekuwaje sasa"

"Alitaka nimpe lift ila nimemkwepa na kumdanganya kuwa kuna mahari nawahi "

"Hahahhaha ungempa tu "

"Watu wako kazin ๐Ÿ˜€,sikia basi kesho utaenda kwenye mkutano"

"Yeah nitaenda "

"Okay poa tutaonana huko basi"

"Poa usiku mwema "..

Alikata sm na kuwasha tv

Upande wa Nana

Alikuwa akiongea na rafiki zake

"Sasa jamani kesho situtaenda kwenye mkutano au" aliuliza groly

"Wewe tena na mikutano yako kama mtakatifu vile kumbe" Nana alimjib

"Nyie nijibuni kama hamtaki nitaenda mwenyewe "

"Twendeni bhn ili tukitoka huko tutapita dinner alafu Kila mmoja ataenda anakojua au Kuna mtu ana chimbo la kwenda " aliongea Bella

Lizzy alijibu na kusema"kwaiyo mnataka kwenda kwenye mkutano wa injili kwakuwa hamna chimbo la kwenda kama ni hivyo simlale tu"

Nancy alijibu na kusema"tutaenda "

Basi walikubaliana wote kuwa watenda


Kesho yake jion saa kumi wote walikuwa jangwani
Ambako ndiko kulikuwa kunafanyika mkutano wa injili

Walifika na kukaa kwa pamoja mkutano ulinza muhubiri alisimama na kuanza kufundisha baada ya mafundisho aliwaita vijana wote ambao hawajaoa Wala kuolewa wapite mbele kwaajili ya maombi maalumu

Nana na kundi lake lote waliinuka na kupita mbele na Chris nae alikuwa katika mkutano huo akiwa pamoja na rafiki yake Joel

Nao walikuwa hawajaoa hivyo nao wakapita mbele

Wakati wakiwa pale mbele Chris alimuoana Nana japo nana hakumuona

Muhubiri aliwaombea Kisha akawaruhusu kurudi
Mda huo wote Nana alikuwa Bado hajamuona Chris

Mkutano uliisha wakaondoka Chris aliondoka na Joel huku Nana nae akaondoka na rafiki zake

Chris alionekana kuwaza kitu

" Vp kaka mbona kama unamawazo"

"Hapana kunakitu nafikilia"

"Kitu gani hicho"

"Achana nacho sio cha muhimu"

Itaelendea

UMENIBADILISHA WEWE NO 05

SEHEMU YA 05

Chris na Joel walifika nyumbani

Chris alimuacha Joel seblen akaingia kuoga

Sura ya Nana alikuwa kikijirudia rudia kichwani alishindwa kuelewa kwann sura ya binti yule ilikuwa inajirudia rudia kichwani mwake

Upande wa Nana alikuwa kajilaza kitandan kwke huku akiwa bize na sm yake

"Mageeee"

"Abee"

"Nichagulie nguo ya kuvaa kesho alafu uinyoshe kabisa "

"Sasaivi au baadae"

"Mwakani nyoko wewe yaani nakwambia unichagulie kwaajili ya kesho alafu unauliza muone sura ilivyomshuka utafikili paka shume mxuuuu embu nitolee Iko komwe lako hapa"

Akiwa anaendelea kuchezea sm yake Nancy alinitumia picha ya Chris

"Umeuona moyo wako'" ulikuwa ni ujumbe ulioambatanishwa na picha

"We Nancy hii picha umeitoa wapi"

"Kwenye account yake ya Instagram"

"Embu fanya unitumie jina analotumia sasaiv"

"Poa"

Sekunde chache alitumiwa jina analotumia Chris

Akaingia insta chap namwenda kumtumia text inbox

"Mambo"

Alituma Kisha akaanza kulike na kucomment kwenye Kila picha aliyopost Chris

Alifanya hivyo ili kutafuta ukaribu nae akakaa kusubiri huenda akajibiwa ila hadi inafika saa sita usiku hakujibiwa mwishoni akaamua kulala


Kesho yake asubuhi Chris akiwa njian kuelekea kazini aliingia mtandaoni na kuona message ya Nana

Hakujibu badala yake alizima data na kuendelea kupiga story na Joel ambae ndio alikuwa akiendesha

Nana hadi asubuhi alikuwa akichungulia kama Chris kamjibu ila ola

Jioni Chris aliamua kujibu ile message
"Poa habari yako"

Nana alipoona amejibiwa anipiga kelele za furaha

"Aaaaaaaaaaa hatimae umeingia line karibu kwenye Dunia ya Nana"aliongea Nana na kujibu message

"Poa tu mzima wewe"

"Yeah niko poa"

"Haya nilikuwa napia hi tu"

"Okay thanks "

Chris Baada ya kuzima data alikaa na kujifikilia kwann huyu msichana amemkaa kichwani hivi
Aliwaza bila hakupata majibu

Siku zilienda huku Nana akimtumia Chris message Kila siku na Chris akawa hajibu anaishia kusoma tu na kuondoka

"Nyie hivi huyu mkaka anajionaje sijui "

"Mkaka gani"alijibu Lizzy

"Chris"
"Hahahaha usiniambie kuwa hadi leo Bado unamfuatilia tu "

"Ndio yaani Kila siku natuma message ila hajibu mwezi umekata "

"Kwani unamuomba uzazi au nini yaani unamtumia mtu message mwezi mzima hajibu hata moja alafu unaendelea tu"

"Lizzy we hujui ni kiasi gani nampenda huyu kaka yaani natamani hata leo awe mume wangu "

"๐Ÿ˜ณ Heeee wewe huyo unaitamani ndoa?'"

"Eee Kwan mimi sio mwanamke mpaka nisitamani kuwa na ndoa"

"Kuna wanawake lakin sio wewe abeg achana na hayo mambo"

"Lizzy umeanza mambo yako "

"Sasa nimeanza nn kwani uongo wakuolewa awe wewe au unataka ukamuue kaka wawatu"..

"Unataka kusema kwamba sifai kuolewa au"

"Labda unafaa ila sio kwa Chris kwa hemed sawa maana vichwa vyenu vinaendana"

"Mfyuuu Kama umetumwa useme kenge wewe"

"Hahhahahahaa kenge mwenyewe ,sijui unapata wapi nguvu za kumtumia mtu text mwezi mzima hakujibu na sio kwamba ni mpenzi wako au rafiki yangu ni mtu tu wakawaida naisi Kuna mtu kashakunuia maana sio kawaida yako"

"Hata sikulaumu maana mtu mwenyewe hujui hata kitu kinaitwa kupenda"

"Hahaha makubwa wakujua kupenda uwe wewe ,mtu uko kama kinyonga Kila mda unabadili rangi sishangai kesho ukisema unampenda mlinzi wenu"

"Eeee Lizzy unikome kama umetafuta tusi la kunitukana ukakosa basi funga bakuri lako "

"Sawa mama wakupenda"


Upande wa Chris alikuwa amekaa huku kupitia message zote alizotuma Nana huku uso wake ikiwa na tabasamu nono

"Nataka nione utatuma message hadi lini'" aliongea Chris na kuweka sm pembeni


Siku zilienda Nana hakukata tamaa , aliendelea kumtumia text mwendo ukawa ni ule ule hakuwa akijibiwa

"Hivi Nana huyo kaka unaemtafuta Kila siku hakujibu unahangaika yanin kwani unatafuta nini haswa "

"Bella we hujui njinsi gani navyompenda Chris "

"Na Hemed je"

"Aaaa usinitajie hiyo mbuzi mi na yeye tushamalizana"

"Makubwa mtu uliekuwa unamlilia Kila siku leo Kawa mbuzi ๐Ÿคฃ, sasa nikwambie tu mpendwa wangu huyo mtu unaemtumia text hivyo na hajibu anakuona unajipendekeza we muache akikuhitaji atakutafuta mwenyewe kwanza usikute ana mtu wake alafu wewe uko bz kupoteza mda wako ooh amka shauri yako"

"Akiwa na mtu inanihusu nini mi ninachotaka niwe wake basi hayo mengine sitaki kujua"

"Haya kazana huenda ukafanikiwa "

Itaelendea
Pata Muendelezo kwa sh 1000
๐‘ต๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ ๐’š๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’๐’Š๐’‘๐’ ๐‘ฝ๐’๐’…๐’‚๐’„๐’๐’Ž ๐‘ด ๐’‘๐’†๐’”๐’‚ 0743433005 ๐’‹๐’Š๐’๐’‚ ๐‘จ๐‘ฎ๐‘ถ๐‘บ๐‘ป๐‘ฐ๐‘ต๐‘ถ
๐‘ผ๐’Œ๐’Š๐’๐’Š๐’‘๐’‚ ๐’๐’Š๐’„๐’‰๐’†๐’Œ๐’Š ๐‘พ๐’‰๐’‚๐’•๐’”๐‘จ๐’‘๐’‘ ๐’Œ๐’–๐’‘๐’Š๐’•๐’Š๐’‚ ๐’๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ +255743433005 ๐’๐’Š๐’Œ๐’–๐’‰๐’–๐’…๐’–๐’Ž๐’Š๐’†.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

UMENIBADILISHA WEWE 01___05 Mpendwa msomaji Leo na kuletea kisa hiki kinachokwenda kwa jina /Umenibadilisha wewe)   >>> https://gonga94.com/semajambo/umenibadilisha-wewe-01___05-mpendwa-msomaji-leo-na-kuletea-kisa-hiki-kinachokwenda-kwa-jina-umenibad

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest