Nilishaanza kumuogopa, kwa maana kuanzia namfahamu sijawah hata mara moja kumuona katika hali kama ile, kuna namna nikawa kama naanza kumuogopa maana sikuona kama ni hali ya kawaida, niliona kama anaweza kuja kuniua, nikasimama na kutaka kuondoka, akanifata na kunikumbatia kwa nguvu kisha akasema naomba usiniache mamaa naomba usiniache, wewe ndio dawa yangu nimechoka kunywa dawa, hata kama ukinikasirikia ila hakikisha kuwa hauendi mbali na mimi, nimechoka kunywa dawa kwa miaka mingi, watu wanajua kuwa nina pesa ila mimi ni mpweke sana, na upweke wangu umefanikiwa kuuondoa wewe tu naomba usiniache....
Alikuwa anaongea kama mtoto mdogo ambae hakuwa na cha kufanya, alikuwa anaongea kama mtoto mdogo ambae mama yake alikuwa amemuacha mwenyewe na Amelia sana akimlilia mama yake, nikamshika mkono na kurudi nae kitandani, hapo simu nikaweka pemben maana usalama wa afya yake ni muhimu sana kuliko hata hilo penzi jipya, nikaanza kumchezea nywele huku namuimbia, akatulia kisha akalala lla alikuwa anashtuka kila dakika ananiangalia, nikawa nashangaa huyu vipi,mwisho akashindwa akaenda kuangalia simu yangu ipo wapi, alipoona ipo mbalia akaja akalala vizuri kisha akanambia naomba usiniache shimena wangu...
Ingawa siku hio Edward alilala kwa marue rue sana, ila alilala mpaka asubuh, na asubuh akanambia kuwa jioni ya siku hio kutakuwa na mkutano, ameshaanza kuona kama kelele hazimuathiri sana na kwa kuwa anaenda kukutana na watu wazima huenda akaweza kuhimili, hivyo nisΓtembee nae sana, mwisho nionekane kama mlinzi wake binafsi..
Basi nikakubali, tukajianda atukaenda kazin, na jion ya siku hio tukawa tumeenda kwenye hio shughuli, ni kweli asilimia kubwa walikuwa ni watu wazima hivyo sikuwa na wasiwasi kabisa, kumbe kuna watu nahisi walikuwa wanajua hali ya Edward, kuna muda nimeenda zangu uwani, nikashangaa nasikia disko limeanza, nikatoka uwani mbio, kufika nakuta watu wamejaa ambao hata hawakuwepo na walikuwa wamemzunguka Edward kana kwamba walikuwa wamepania kuona anadhalilika, nikafika nikamuona Edward macho yameshaanza kuwa mekundu na muda sio mrefu ataanza kutetemeka kwa uoga na ni jambo la aibu sana kwa mtu kama yeye, hivyo nikachukua mic kwa mtu mmoja ambae alikuwa anaperform karioki kwa lazima maana hakutaka kunipa kisha nikaanza kuimba taratibu na watu wote waliokuwa pale wakakaa kimya....
Nikaanza kuimba "I found love, for meee Darling just dying by in, and follow my lead I found a boy handsome and sweet I never new your someone, waiting for meee We were just kids when fell in love
not know and what it was, I will not give you up
this time
baby just kiss me slow, you're the one that I owN sasa wakati ambapo nilifika hapo nikawa nimeshamfikia Edward, nikamsogelea na kumuambia kwa sauti ya chini kuwa " siku zote nitakuwa kwa ajili yako...
akashusha pumzi kisha akanikumbatia kwa
nguvu sana, mpaka kuna muda nikawa nahisi kama mioyo yetu imekutana, akaniambia naomba usije ukakaa mbali na mimi shemina... watu sasa wakajua kuwa tunapendana sana kumbe nilikuwa namtibu, maana alishaanza kuchanganywa na zile kelele za pale, hivyo asilimia kubwa ya watu waliokuwa pale hawakushtukia mchezo ulivyokuwa unaenda, basi nikamshika mkono na kuondoka nae hapo hakuna mtu ambae alielewa kuwa Edward alikuwa anaanza kuchanganyikiwa kutokana na kelele ambazo zilikuwa eneo lile....
basi tukafika nyumban nikashangaa Edward ameingia chumban alafu akawa anatetemeka kwa uwaga, mara nyingi huwa anakuwa hivyo pale ambapo kelele zinakuwa zimeshaanza kumdhuru na kumuathiri, nikamsogelea na kumuuliza shida ni nini, nikashangaa anaanza kulia, kisha akasema laity kama usingekuwa pale wakati ule, basi ningedhalilika, ni nani ambae alifanya vile, alitaka kila mtu ajue kuwa mimi nina matatizo ya akili....
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments