Siku ikapita, ila Rose alianza kulalamika nikama nimeanza kujitenga kuna siri gani kati yangu na Madam nilimwambia hakuna lolote, ila alionekana kuchukia, sikujali nilikuwa bze kujisomea kwa ajili ya mtihani, hatimae nikahitimu, siku ya kurudi nyumbani ikafika, madam akaomba ruhusa, tukawa tunasubiri usafiri tuijiwe,tukiwa tunasubiri ikaja gari ya bei mbaya afu safi vibaya mno, ikapaki mbele yetu,akashuka Teacher G, kila mtu akawa anamshangaa, Rose akaomba lift, Teacher akakubali tukaambiwa tupande wote, Rose akawahi mbele mimi na madam tukakaa. nyuma...
Tulisalimiana uku gari inatembea, alitupa hongera kwa kuhitimu,muda huo tuliwajulisha nyumbani wasije tuko njiani tayari, ilikuwa ni mwendo wa masaa kama 4 ivi, tulifika nyumbani tukashuka, nikashusha mizigo yangu kwenda kwenye nyumba yetu, mimi na madam, ajabu na Teacher nae akawa anatufata, hee, Rose akamuita, ikabidi aende nae, nilifika nikabadilisha nguo, mama akaja tukamsalimia nakutambulishana apo mama akafurahi, alikuwa ameshatuandalia chakula, akaomba tule yeye akawahudumie huko, tulimruhusu akatoka....
tena Alivyotoka tukaanza kupakua nikacheki kwa pembeni, nikaona kuna chimbo huwa tunaficha soda zipo kama soda 8 ivi nikajiongeza apa zishapigiwa bajet, mpaka siku mgeni anaondoka, nilitoa, tukiwa tumejiachia wenyewe tunacheka tukasikia hodi, ilibidi tutazamane hodi sauti ya kiume kabisa, ilibidi nitoke nakuta ni teacher, niliamua kumkaribisha nje, nikatoa na mkeka na dada madam akatoka, tukapakua, naΠ° yeye tukamletea soda, apo ni nje, tena kwenye mkeka, akaanza kula, kidogo Rose akatoka, akatutizama, akaja na yeye...
Nikafata sahani, tukala, apo story ni Rose na madam ndo wanaongea mimi na Teacher kimya, Rose akamuomba Teacher waende ndani apa panaumiza, "Rose we nenda tu mimi napenda sana kukaa kwenye mkeka kuliko uko ndani, Rose alinikata jicho, akatoka karudi na kaka ake, wakaanza mada za kuonesha mimi nadate na Ronard, nilijiongeza wanataka kumuaminisha Teacher nina mtu, ili kamal ananiwazia avunjike moyo, waliendeleza chokochoko, hakuna anaewasaport, badae Teacher akaniambia nikamuite mama anamaongezi nae kidogo, Rose na Ronard wakatazamana...
Mimi niliinuka nikaenda kumfata mama alikuja, Teacher akawaomba watupishe anashida private, waliondoka kishingo upande, Baada ya kuondoka Teacher aliomba samahani kisha. akaenda kwenye gari akaja na vitu akasomba tukamsaidia, ilikuwa mchele, sukari, mafuta, ngano, vitenge, akaniletea na laptop na simu, kama zawadi ya kuhitimu, kwanza tukatazamana, tukatulia, madam alitoka akaingia ndani, tulibaki wenyewe tu, Teacher akasema, "mama nisamehe kama nitakuwa nimekosea lakini nimekuja hapa kumchumbua binti yako, ukweli nampenda sana nahitaji kumuoa kabla hajaingia chuo, nilikuwa naomba ruhusa yenu nyote, najua hata Gift hajui kama nampenda, lakini huo ndio ukweli,ninampenda sana, niliacha kufundisha kwa ajili yake ili kumlinda amalize kwanza masomo, niliona sitoweza kuvumilia nikiwa karibu yake, nimesubiri amalize ili nifate taratibu zote...
Mama alinitizama mimi nikawa nashangaa, nikakataa mimi sitaki wanaume kabisa, Teacher aliinama kisha akamuomba mama ruhusa atoke na mimi kwanza tuongee kisha tutarudi mama alisema ngoja kwanza, aliingia ndani, akashauliana na binti yake apo kapata wakushauriana nae, wakaamua kuniruhusu, tulipanda gari, wakati mlinzi anataka kutufungulia Rose akaja kuzuia nayeye anataka kupanda, Teacher akasema anajambo muhimu. sana haitaji mtu waziada, Rose alinikata jicho akaondoka,tulitoka tukaenda hotel moja imetulia kweli, Teacher alinitazama sana, nikawa naona tu aibu, akaomba akae karibu yangu, nilikataa akasema hatovuka mipaka, alisogea akaanza kuongea, "G nakupenda, mimi sio mpitaji ndio maana nimekuja moja kwa moja, naomba unipe nafasi, sitamani kukukosa kabisa, na sijui kama nitaweza, ukweli nitaumia sana...
Na nahofia kusubili zaidi nahisi utaniacha, alikuwa anaongea kama anatetemeka, nikawa namshangaa, nikajikaza na kimwambia, Teacher wanaume ni waongo sana nyie, yani wewe jinsi ulivyo uje unipende mimi? Ilihali kuna watu wadada wazuri sana,mmh ata sikuelewi, "G usione hivi napitia wakati mgumu sana, hujui tu, tukiwa pale ghafla hotel ikavamiwa, ile hofu nilijikuta namkumbatia G ziro distance, mtoto wa watu pamoja na kuwa tuko kwenye hatari lakini akuwa akiwaza akawa bze kwenye hisia, alijikuta kaleta mdomo wake kwangu...
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments