Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

CEO NISAMEHE SIRUDII TENA ❀ SEHEMU YA KUMI NA TATU*

13th Sep, 2025 Views 47




Wakakuta kimya kuuliza wanaambiwa mganga kafariki ni wiki sasa, walichoka, wakauliza kama kuna mganga mwingine wakaelekezwa kijiji cha tatu kutokea hapo, ilibidi warudi kwanza mjini wakajipange, walirudi kila mtu anamawazo, walianza kupata mashaka, na hali zao pia hazikuwa nzuri, walikuwa wanatoa harufu mno, wakaamua kumpigia doctor wao, akaja na kuwaambia, wanatakiwa kusafishwa hali sio nzuri na huwa ni kwaida yao kupigwa bomba lakini wanarudia, awamu hii hali ilikuwa mbaya zaidi, na gharama ilikuwa kubwa mno, walipiga hesabu kuipata inahitaji akili....

Ilibidi wapambane kwanza kwa mganga ili wampate ya Naseer awape pesa matibabu, upande wetu huku pia Hali ya Naseer ilikuwa mbaya milija yake ilikutwa na uchafu mno, ilibidi tumpeleke nje kwenye matibabu ya uhakika zaidi, niliondoka na mwanangu Elham kwa kuwa alikuwa likizo sikutaka kuamini mtu kabisa, niliondoka nikaenda kumuuguza mpaka akakaa sawa, ilichukua miezi mitatu, ilibidi mwanangu nimtafutie mwalimu huko huko awe anasoma ili asiwe nyuma...

Huku kina Najma hali ilikuwa mbaya mno, mganga aliwalia pesa walikutana na tapeli, awakupata msaada wowote, Najma akaamua kwenda kwenye kampuni ya Naseer ili akadai ata talaka apate pesa, kufika anaambiwa kampuni sasa hivi ni ya mama mtu, alishtuka akajua apa anaweza asipate hata kijiko, sasa ni bora akaitishe vyombo vya habari kulalamika CEO mkubwa lakini hamhudumii mke wake...

Wakati anaenda kwenye vyombo vya habari, akadondoka njiani, alipata msaada, akapigiwa Husna akaenda, wakapata wazo wampigie mama ake Najma make nae pesa ipo, mama ake alivyofika alilia kwa uchungu, akauliza shida nini, walificha nakula njama na doctor, mama alitoa pesa lakini hali ikawa tete ikabidi wasafilishwe wote kwenda kutibiwa hoptal ya rufaa mama ndo akajua ukweli aisee alilia yule mama kama mtoto, aliamua kushughulikia mtoto wake tu, akamuacha Husna peke yake akiwa amepoteza fahamu...

Mpaka akafariki, walitafutwa ndugu zake, kupitia simu yake, wakambahatisha mama ake mdogo, ndio akaja wakachukua mwili, wakaenda kuzika sisi hatukuwa na habari yoyote, tulirudi, nyumbani mme wangu akaanza majukumu yake, na akaacha kabisa kufanya vikao kwenye mahotel, ni kazini kwake alitengeneza ukumbi kwa ajili ya watu maalumu, aliogopa hata kucheka na wanawake, wala kula chochote nje,aliniomba niwe nampa tu chakula chake bora ale kiporo lakini kula chakula au maji nje na kwake amekoma...

Alinunua jiko la umeme,kwa ajili ya kupashia chakula chake, akawa anatembea nalo dogo dogo tu kwenye beg lake, na chakula chake bila kusahau maji, yakimuishia, alikuwa ananipigia nimpeleke, hatukujua taarifa za Najma, mpaka siku moja mama ake Najma alipiga simu, nakumuuliza Naseer mkewe yuko wapi, Naseer aliomba waonane, mama Najma aligoma nakuanza kugomba, alitaka kupambana ili mtoto waje abaki na Naseer...

Naseer aligoma nakusema yuko tayari kwa lolote atampa talaka hamhitaji, vita ikaanza, hapo Najma alikuwa kapona, mama Najma akawaza akaamua kutafuta plan B...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CEO NISAMEHE SIRUDII TENA ❀ SEHEMU YA KUMI NA TATU*  >>> https://gonga94.com/semajambo/ceo-nisamehe-sirudii-tena-sehemu-ya-kumi-na-tatu

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest