Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

Nilikuwa nimelala fofofo, mpaka mke wangu akaanza kunipigia kelele akisema: “Amka ukapokee simu… tangu muda inaita haikati!”

9th Sep, 2025 Views 28



Nikafumbua macho kwa tabu nikamuuliza:
“Saa ngapi sasa hivi?”

Akasema:
“Bado alfajiri haijatoka.”

Nikakasirika nikasema:
“Ni nani asiye na adabu kupiga simu muda kama huu?”

Akasema:
“Ni namba ya ajabu, lakini imeita zaidi ya mara ishirini!”

Nikajibu:
“Hakika hao ni vijana wajinga wanaocheza na namba za simu wakitarajia kwamba atapokea msichana… lakini naapa nitamkomesha!”

Nikashika simu nikiwa tayari kumtukana, nikasikia sauti ninayoijua ikisema:
“Asubuhi njema rafiki yangu, samahani kwa kukuamsha, lakini nahitaji msaada wako katika jambo muhimu lisiloweza kusubiri.”

Nikamuuliza:
“Asubuhi njema, lakini wewe ni nani? Namba hii siijui.”

Akasema:
“Mimi ni fulani.”

Nikasema:
“Pole sana ndugu yangu, samahani, mimi nilikuwa na namba yako ya zamani tu… Kheri gani?”

Akanijibu:
“Mama yangu aliumwa jana, na madaktari wamesema lazima afanyiwe upasuaji haraka. Mimi hali yangu ni mbaya, nahitaji uniwekee mkopo kidogo hadi nipate fedha za chama mwezi ujao.”

Nikamwambia:
“Pole sana, na Mwenyezi Mungu amponye. Lakini kwa kweli sina pesa taslimu sasa hivi nyumbani.”

Akasema:
“Hakuna tatizo, Mwenyezi Mungu ni mkubwa. Samahani tena kwa kukuamsha.”

Akakata simu.

Mke wangu akanigeukia na kuniuliza:
“Huyo alikuwa nani?”

Nikamjibu:
“Ni fulani.”

Akasema:
“Na alikuwa anataka nini?”

Nikasema:
“Anataka mkopo, lakini nikamwambia sina, kwa sababu ukweli ni kwamba yeye hunikumbuka mimi tu pale anapokuwa na shida.”

Mke wangu akanitazama kwa huzuni kisha akasema:
“Ni nini sasa! Watu tumeumbwa kusaidiana, na anayekutafuta katika shida yake ni neema kutoka kwa Mungu kwako, siyo balaa.”

Kisha akaendelea kusema maneno mazuri:
“Ibn ‘Abbās (RadhiyaLlahu ‘Anhu) alisema: Kuna watu wanne huwezi kuwalipa jema lao.

Mtu anayekutangulia kwa salamu.

Mtu anayekupa nafasi katika kikao.

Mtu anayejitaabisha ili akusaidie katika jambo.
Na wa nne, thawabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu peke yake – naye ni yule aliyepatwa na shida, hakupata yeyote ila wewe, akakuamini na kuweka siri yake kwako.”

Wakati huo nilihisi maneno yake ni ya kweli. Nikampigia tena rafiki yangu, nikamwambia:
“Nimepata kiasi kidogo kwa mke wangu, chukua unachohitaji na Mwenyezi Mungu akupanulie.”

Naye akajibu huku sauti yake ikikwaruza kwa kulia:
“Wallahi ndugu yangu, mara tu nilipokata simu na wewe nilihisi kama dunia imenifunga. Nikainua mikono yangu juu nikasema: Rabbī innī massaniyaḍ-ḍhurru wa Anta Arḥamur-Rāḥimīn (Mola wangu, hakika nimeguswa na dhiki, nawe Ndiwe Mwenye rehema kuliko wote). Sikumaliza hata dua yangu ila nikakupokea tena ukinipigia… Nikajua kuwa Mungu amejibu maombi yangu kabla hata sijakufungulia.”

Mafunzo ya hadithi hii.

1.Msaada kwa mwenye dhiki ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu – Wakati mtu anakutafuta katika shida yake, usimchukulie kuwa ni kero, bali ni fursa ya wewe kuwa sababu ya kheri.

2.Maneno ya hekima yanaweza kubadilisha mtazamo – Ushauri wa mke ulimsaidia mume kuona ukweli na kugundua thamani ya kusaidia wenzake.

3.Dua hupokelewa haraka zaidi ya tunavyodhani – Wakati mwingine msaada unakuja kwa ghafla kama jibu la dua, na hiyo ni alama ya rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake.

✨Mara nyingi, anayekutafuta kwa ajili ya kukuomba umsaidie katika dhiki yake hiyo siyo kero kwako, bali ni ishara kwamba Mwenyezi Mungu amekuchagua kuwa sababu ya kheri kwake.

Allah atupe nyoyo za huruma za kuwasaidia wengine, aamiin🤲🤲🤲 #MzimbiriTv

Sufian Mzimbiri.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Nilikuwa nimelala fofofo, mpaka mke wangu akaanza kunipigia kelele akisema: “Amka ukapokee simu… tangu muda inaita haikati!”  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilikuwa-nimelala-fofofo-mpaka-mke-wangu-akaanza-kunipigia-kelele-akisema-amka-ukapokee-simu-tangu-m

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest