Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Nay Wa Mitego X Mtafya - Shida

MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJILI SEHEMU YA 04*

11th Sep, 2025 Views 56



Chakula chake cha usiku nilikuwa nakipikia nyumbani kule mgawahani kwetu hakuna hata umeme pale ni spesheli kwa chakula cha asubuhi na mchana tu😍😍

Basi bwana nilimwelekeza akaniambia anakujaaπŸ™ˆπŸ™ˆ ilibidi sasa nianze kumpakulia msosi wake kwenye hotpot nzuri mteja ni mfalme bwana😍

Ile juice niliitia kwenye kopo fulani hivi naloekea maji yangu ya chuoπŸ™ˆπŸ™ˆni zuri😍😍 Hemed alifika karibia na kwetu akanipigia..

Nilimuomba asije na gari yake mpaka nyumbani majirani wataanza kutudisi hahahaa mi naogopaπŸ™ˆπŸ™ˆ aliegesha gari kwa mbali kidogo kisha akatembea mpaka kwetuπŸ™ˆ

Nilimkaribishia nje kulikuwepo na kiti pale akakaa nikamtolea chakula chake nilikuwa nimekifungasha vizuri akanishukuru baada ya hapo akatutakia usiku mwema akaondoka zake..

Usiku tena wakati najisomea akanipigia😝😝 ilikuwa mida kama ya saa nne hivi nikajiuliza au nimezidisha machumvi huko kwenye chakula hahahaaa

Nilipokea kama kawaida yake akaniambia samahani kwa usumbufu BellaπŸ˜”πŸ˜” bila samahani Hemed karibu nakusikiliza..

Asante sana kwa chakula BellaπŸ₯ΉπŸ₯Ή chakula ni kitamu sana😞😞tangu nizaliwe leo ndo nimekula chakula chenye radha tamu ninayoipenda❀️❀️

Asante sana mama Mungu akubarikiπŸ₯Ήβ€οΈ lolπŸ™ˆπŸ™ˆπŸ™ˆnilijisikia furaha mieeπŸ™ˆnikamwambia asante kwa kushukuru Hemed naomba nikutakie usiku mwema.

Nilikata simu chapuπŸ˜‚πŸ˜‚mi sitaki hizo habari za kuzoeana mwisho yaibuke mengine akuu najiepushaaaa...

Baada ya kukata simu ikaingia msgπŸ€—πŸ€—na that time sijui nilianza kuwajeπŸ™„ simu ikiita tu nawaza ni HemedπŸ˜”πŸ˜”msg ikiingia tu nawaza katuma Hemed..

Nilifungua msg kweli ilitoka kwa Hemed aliniuliza kama niko free anipigie tuongee mmhhh nilimkataliaπŸ™ˆ

Nilimwambia niko bizeπŸ€—πŸ€— bize usiku huu Bella??. Kwani unafanya nini mamaaa...

Uuwww huyu naye kwanini ananiharibu😰😰😰nilishindwa kabisa kuacha kujibu msg zakeπŸ₯ΊπŸ₯Ίkila akituma najibu kila akituma najibu nikajikuta hata madaftari nimeyatelekeza..

Nilimwambia mie usiku mida kama hii nakuwa najisomea maana ndo nakuwa free sina hekaheka..

Oh sorry mama kwa usumbufu so unasoma uko level gani??. Nikamwambia niko chuo...

Chuo gani unasoma unasomea nini??. Nikamwambia niko IFM nasomea course fulani..

Wow hongeraπŸ₯Ίβ€οΈnikamwambia asanteee...hapo nyumbani mnaishi na wazazi wenu???..

Dah😭😭😭hilo swali lilikuja kunikumbusha wazazi wanguπŸ₯ΉπŸ₯ΉπŸ₯Ήnilijikuta tu naanza kulia na sikuweza kumjibu chochote nilizima simu nikaenda chumbani kwanguπŸ˜“

Nilichukua picha ya mama na baba nikawa nawatizama tu naishia kuwaloanisha kwa machozi..

Nililia usiku mzima majukumu niliyonayo ni magumu😭😭😭 kesho yake niliamka macho yamevimba sana...

Sikuweza kulala wala kubakia nyumbani ilibidi nitoke nikahangaike nikilalala nani atanitafutia sina wa kunitafutia😰..

Nilimtuma poppy sokoni mimi nikatangulia kupika vitafunwa bado simu nilikuwa sijaiwasha😰
Wakati napika vitafunwa kwa nje nilisikia muungurumo wa gari nilipochungulia nikamuona Hemed anashuka kwenye gari na vile vyombo alivochukulia chakula usiku..

Nini kitafuata???. Itaendeleaaaaaa

*SEHEMU YA 05*

Hemed alipiga hatua mpaka ndani na mida hiyo sikuwa na mteja yoyote maana ilikuwa asubuhi sana ..

Niliipua nilichokuwa nakipika nikaenda kwanza kumpokeaπŸ˜”πŸ˜” aligundua siko sawa😰😰..

Swali la kwanza aliniuliza Bella are you okay??..

nyieee hiko ndo kitu pekee nilichotamani kuulizwa kwa muda huoπŸ˜­πŸ˜­πŸ™Œ

Nilishitukia tu machozi yananitoka bila kujizuia nilimwambia no I'm not okay HemedπŸ₯ΉπŸ₯Ή..

Aliweka vile vyombo pembeni then akanikumbatiaa😞😞wakati Hemed amenikumbatia kwa bahati mbaya poppy nayeye alirudi kutoka sokoni akawa ametukuta😰😰..

Nilimwachilia Hemed haraka nikarudi nyuma kuendelea na kazi yangu..

Sikuweza kumwelezea chochote naye aliona mazingira siyo rafiki ikabidi aondoke lakini hakuwa okay kwa sababu ya hali aloniacha nayo..

Tulisaidiana na dogo kuandaa chakula kabla wateja hawajaanza kuja..

Mida ya saa nne mimi nilipeleka chakula site kwa Hemed poppy akabaki anahudumia pale ofisini..

Siku hiyo nilienda nikamkuta Hemed kule site alikuwa tu amekaa ndani ya gari lake..

Niliwapa chai mafundi nilipomaliza akaniita kwenye gari mmhhh sikuenda πŸ˜“πŸ˜“ watu wataanza kutujadili wakati hakuna hata kinachoendelea kati yetu..

Alipoona siendi aliamua kutelemka kwenye gari akanifuata pale nilipokaa..

Alikuja akaniomba tuongee mi nikamkatalia nikamwambia hapa siyo sehemu sahihi..

Aliniomba tuzunguke nyuma ya nyumba muda huo mafundi wanakula..

Nilimkubalia tulienda nyuma ya nyumba Hemed akaanza kuniuliza nina shida gani kwanza nimevimba sana macho kama mtu niliyekesha nikilia..

Nilimwambia kuna vitu tu vinanisibu alianza kunibembeleza nimwambie lakini naanzaje kumwambia mtu hata simjui nianze kumwelezea matatizo yangu..

Sikumwambia chochote niliishia kulia tu na baada ya hapo nilichukua vyombo nikaondoka pale..

Hemed alinifuata ofisini mgawahani kwetu pale...alikuja akamuita poppy akaenda kuzungumza naye hata hivo nilishamzuia poppy kusema kitu chochote bila ruksa yangu..

Hemed bado alitaka kujua nasumbuliwa na nini alimuuliza poppy lakini poppy hakuweza kuongea chochote alimwambia tu kuna siku dada mwenyewe atakwambiaπŸ₯ΉπŸ˜žπŸ˜”..

Mkaka wa watu siku hiyo hata hakunywa chai nilimhurumia sanaπŸ™ˆ

Aliondoka ila akaniomba niwashe simuπŸ€—πŸ€—πŸ€—nilifanya hivo ilibidi niwashe simu nione anataka kusema nini...

Baada ya kuwasha simu alinipigia akaniuliza kama nimekula nikamwambia sina appetite ya kula chochote..

Alinibembeleza mno akaniomba nile chakula mmmhhh nilimuitikia tu lakini wala sikula..

Jioni mida ya saa kumi tulifunga mgahawa tukarudi nyumbani kwa vile huwa tunapika chakula cha Hemed nyumbani

basi nasisi tulianza kuwa tunakula uko huko home badala ya mgahawani..

Siku hiyo usiku Hemed alikuja kuchukua chakula akiwa hana Amani kanyong'onyeaπŸ˜”πŸ˜”

Nilimtolea chakula chake lakini alikataa kukipokea aliniambia nirudishe chakula ndani tukale wote maana mpaka muda ule bado nilikuwa sijalaπŸ™ˆ

Nilijaribu kumgomea nayeye akanigomea😝😝akadai haondoki pale kwetu bila mimi kulaπŸ™

Itaendeleaaaaaaaa
Full yote 2000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJILI SEHEMU YA 04*  >>> https://gonga94.com/semajambo/mrembo-yatima-na-kijana-tajili-sehemu-ya-04

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Nay Wa Mitego X Mtafya - Shida
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest