Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

BABA KWA NINI ULIMUUA MAMA YANGU?😭 ----- (01) (Kama una Machozi ya Karibu Usisome πŸ₯Ί)

17th Sep, 2025 Views 16



Naitwa Magreth (Mage) kumbuka nilikuwa kidato cha pili kipindi hicho najiandaa na mitihani ya Taifa katika shule ya sekondari Tambaza, ilikuwa jioni ya saa kumi na mbili ikielekea saa moja giza likiwa limeshaanza kuingia tayari, ingawa huwa ninatoka mapema saa tisa lakini siku hiyo tulichelewa kwa ajili ya watu wa mazingira waliokuwa wametutembelea shuleni kwetu.

Kichwani sikuwa haba, nilikuwa nina akili za darasani na ndiyo maana nikachaguliwa kujiunga na shule hiyo maarufu ya Wasichana pekee ambayo ilikuwa miongoni mwa shule kumi bora zinazochukua watu wanaofaulu kwa maksi za juu kipindi hicho, zikiwemo Jangwani, Kisutu Girls, Zanaki na zingine za wanaume pekee kama Azania na za jinsia zote...

Nilifika nyumbani nikiwa nimechoka sana kutokana na purukushani za usafiri wa mjini, nikiwa hoi na kabla ya kufika kabisa mbele ya nyumba nilikaa kwenye baraza moja ya nyumba ya jirani kwa sekunde kadhaa mguu mmoja ukiwa unaniuma kutokana na kusimama kwa muda mrefu ndani ya daladala kutokana na foleni kubwa.

"Wewe mama naniliu umejikalisha huku unapitwa na mambo" nilisikia sauti ya mmoja wa wapangaji akimwambia mwenzake ndani ya nyumba hiyo.

"Mambo gani shoga yangu tena?"
"Ngumi huko nyumba ya pili"
"Nyumba ya pili wapi, ndo mambo ninayoyapenda mie hayo uuuwiii"
"Kwa kina Mage huko"
"Mage huyu anaepitaga pitaga na uniform za shule?" Waliongea, walipotaja jina langu moyo ukafanya paa!!

"Nyumbani kuna ngumi, haiwezekani" niliongea mwenyewe na kutupa begi langu la shule chini bila kulijali tena nikakimbia mbio kama nilivyo mpaka nyumbani ambapo nilikuta majirani mbele ya nyumba yetu wananong'ona nong'ona huku ndani nikisikia sauti ya mama akipiga makelele na baba akimgombeza

"Nitakuua wewe mwanamke, nitakuua" baba aliongea kwa hasira huku vikisikika vishindo ikionekana anampiga mama
"Niue tu niue tu, ndivyo ulivyozoea niue" mama alijibu huku akilia nami nikaufuata mlango na kujaribu kuufungua lakini ulifungwa kwa ndani nisingeweza kuufungua

"Baba muache mama Yangu" nilipiga makelele kama kichaa huku nikilia
"Mage binti yangu uuwii baba yako ananiua" mama alilia aliponisikia napiga kelele mlangoni.

"Jamani nisaidieni nifungue mlango tumsaidie mama" niliwaomba majirani.

"Mh nani anataka kesi, aku" mmoja aliongea huku wakitawanyika kila mmoja na kuniacha nje pale mimi mwenyewe nikiangua kilio baada ya kushindwa kumsaidia mama....

Kwa Simulizi zingine Tamu ingia hapaπŸ‘‰ Hadithi Za Chumbani

ITAENDELEA!!.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BABA KWA NINI ULIMUUA MAMA YANGU?😭 ----- (01) (Kama una Machozi ya Karibu Usisome πŸ₯Ί)  >>> https://gonga94.com/semajambo/baba-kwa-nini-ulimuua-mama-yangu-01-kama-una-machozi-ya-karibu-usisome

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest