Nikajiangusha chini na kujifanya Kuwa nimepoteza fahamu π.
βWe mnuka jasho wa kimasikini nipe funguo niondokeβ
Alizungumza mume wangu uku akinitikisa kWa miguu.
βShamsa, sitaki drama mimi Sawa, na unanichelewesha ujue β
Alizungumza Hamad akiwa na hasira ya Mbogo.
βNitakupiga ujue β
Hamad aliendelea kulalamika na Mimi niliendelea kujifanya Kuwa nimezimia, gafla tu Hamad akavuta mkanda wake wa suruali na pasi na Kuwa na huruma yoyote ile juu yangu akanitandika nao mgongoni.
Nyieeeeh ππ mkanda shikamoo, nilifurukuta pale chini Kama samaki aliyetolewa kwenye maji na kutupiwa nchi kavu Tena kwenye jua kali π.
βNiue sasa, nimesema Niue β
Nilianza kulalamika na kulia, eeeh mume Angu ajui ata mambo ya kudekeza nyie π nilipigwa mikanda mfululizo mwisho huyo nikakaa wima Mwenyewe na kutoa funguo ambayo niliificha kwenye manyonyo.
βNikirudi nisikute hizi takataka zako umu Ndani β
Kisha Hamad akafungua mlango na kuondoka zake.
Kwa unyonge kabisa nikanyanyuka na kutoka zangu nje na kuwaamsha wanangu, nilihakikisha Kuwa watoto wangu wamekula wameshiba kisha nikawapeleka Nyumbani kwetu na Mimi nikarudi kuendelea na Mishe zangu.
Majila ya Kama Saa 4 hivi, familia ya mume wangu na mke huyo Khadija walifika wakiwa na kigoma kile cha uswahilini Yaani ndio wanamkaribisha mkwe wao.
βUmeshatoa takataka zako kule Ndani ??β
Hamad aliniuliza kwa sauti ya chini sana ili watu wengine wasiweze kusikia.
βSijaona takataka yoyote kule Ndani β
Nilijibu kWa sauti ya jeuri kwani nilijua kabisa Awezi kunifanya kitu chochote kile ikiwa kuna watu wengi sana.
βShamsa katoe takataka zako, halafu hakikisha unapanga vitu vya mke wangu β
βWe kichwa chako sasa hivi Kina wadudu Walahi, Yaani Mimi ndio nifanye huo ujinga ? β
Nilijibu kisha huyo nikaingia zangu jikoni na kuchukua juice kisha moja kwa moja nikaenda zangu chumbani kwangu na kutulia.
Nikiwa chumbani gafla mama Angu mkwe na Wifi zangu wawili wakaingia na kuanza kutoa nguo zangu kabatini, Tena walizitoa uku wakitupa tupa uku na uku.
βMama ni kitu gani hiki mnanifanyia lakini ??β
Niliuliza kWa sauti ya huzuni sana π₯Ή.
βKoma wewe me naweza Kuwa na Mtoto Kama wewe, Ebu kusanya hivi vi sepe vyako haraka tuweke nguo za mtu na nusu β
βMama Una watoto wa kike ujue β
Nilizungumza uku nikiwalenga Mawifi zangu hao wawili ambao walikuwa bado awajaolewa yaani ni wakubwa kuliko Mimi lakini mpaka muda huo hawakuwa waneolewa.
Aaah kila mtu alinipuuza zaidi wakaongeza nguvu na kuanza kutupia nguo zangu nje, nilibaki Nikilia na kuwaomba waweze kunihurumia lakini haikusaiidia kabisa zaidi baba mkwe nae akaja kuwaongezea nguvu.
Baada ya muda kila kitu kilikaa vizuri uku vitu vyangu vikizagaa kwenye chumba cha watoto wangu, kWa hali ya utulivu kabisa nikaanza kukusanya kila kitu na kuweka kwenye chumba cha wageni, Kiukweli kila kitu kilikuwa kΔ±nanΔ± umuza sana lakini sikuwai kutamani watoto wangu wajue maisha ambayo yanaendelea kati yangu Mimi na baba Yao.
Majila ya Saa 1 usiku, nikachukua usafiri na kwenda kuwafuata watoto wangu Nyumbani kwetu kwani siku inayofuata wanatakiwa kwenda shuleni kuendelea na masomo.
Kuna muda nilitamani sana watoto wangu Wakasome shule ya kukaa uko uko ili tu waepukane na hizi hekaheka lakini ilikuwa kazi nzito sana kwani kila kitu ni juu ya baba Yao.
Majila ya Saa 3 usiku Mimi na watoto wangu tukiwasili Nyumbani na muda huo tulimkuta Hamad akiwa na huyo mwanamke wake Khadija hapo sebule wakitomasana tu utazani wanaishi peke Yao.
βAntieeeh β
Watoto wangu walimuita Khadija kWa furaha sana na kwa bashasha wakamkumbatia ni wazi Kuwa wanamjua na yeye anawajua vizuri sana.
βNiliwamisi sanaβ
Alizungumza Khadija uku akiwashikashika watoto wangu mashavu, Walahi Kama mama nilijikuta nikiumia sana lakini ndio hivyo Tena ni mke wa pili wa baba Yao.
Sikuona sababu ya Mimi kuendelea Kuwa hapo kwa haraka nikashtuka njia nikitaka kuelekea chumbani kwa watoto wangu ili kuwategea net gafla hamad akanisimamisha.
βUnaenda wapi ? Tunamaongezo hapa β
Niligeuka kwa utulivu kabisa kisha nikazungumza.
βNaenda kuwawekea watoto net wapate kupumzika kesho wanaenda shuleniβ
βMama Yao ameshaweka kila kitu Sawa mpaka nguo za shule ameshanyoosha amekusaidia wewe usiyejua majukumu ya Kuwa mama bora β
Alizungumza hamad mbele ya watoto wangu.
Unajua Bwana mpaka sasa ukiniuliza nilimkosea nini mume wangu wlaahi sina jibu, siku zote Nimekuwa mkimya sana, siku zote Nimekuwa nikijishusha naa kujiweka mbali sana na ugomvi lakini wapi, Nimekuwa nikiomba mpaka msamaha kwenye makosa ambayo siyajui lakini wapi yaaani Sijui ata sababu ya ugomvi wangu na mume wangu.
βHaya mkalale sasa Antie mtaongea nae kesho β
Niliwaambia watoto wangu uku nikijichekesha tu.
βUsiku Mwema daddy β
Kwa pamoja wakamuaga baba Yao na kukimbilia chumbani mwao, polepole nikasogea mpaka alipokuwa amekaa mume wangu kisha nikakaa pembeni na kWa sauti ya chini nikamuuliza.
βNikuombe kitu mume wangu ??β
βNiite hamad inatosha sana, mtu wa kuniita mume kwenye hii Nyumba ni Khadija tu β
βNi Sawa, lakini Naomba sana sana weka mipaka kwenye maneno yako aswa wakati ambao watoto wapo, siitaji waathirike na chochote kile kinachoendelea baina yetu β
Hamad akamgeukia Khadija na kucheka sana akazungumza.
βBabe unamsikia huyu mpuuzi lakini, Yaani ananifundisha mimi jinsi ya Kuwa baba bora kwa watoto wangu ambao Mimi nahusika na kila kitu kwenye maisha Yao β
Kiukweli kila kitu kimeshanichosha nilibaki Kuwa kimya tu, Basi utambulisho mfupi ukashika nafasi kisha kila mtu akaenda kulala.
*******
Maisha yaliendelea kwenda uku kWa upande wangu maisha yakizidi Kuwa magumu sana, Yaani matatizo yaliongezeka sana kwaajili ya uwepo wa Khadija, nilijitaidi sana Kuwa Mtulivu lakini Hamadi alikuwa makini kuhakikisha Kuwa makosa amani.
Ikiwa ni Majila ya Saa 5 usiku nikiwa chumbani kwangu, muda huo nilikuwa naswali zangu na kumuelezea Mungu wangu magumu yangu gafla hamad akaingia na kuzuungumza.
βNimefata haki yangu na nimebanwa sana β
Sikuweza kuitika Wala kujibu kitu zaidi niliendelea na swala yangu.
βUnisikii au ??β
Hamad aliniuliza kwa hasira sana.
Baada ya hamad kuona Kuwa Nipo kimya sana alishikwa na hasira sana, sasa wakati na inama kwajili ya sujudu hamad akanichota teke na nikajikuta nikipiga beki bila kupenda ππ nacheka Kama mazuri lakini ameharibu swala yangu.
ITAENDELEAβ¦.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments