πΏππ£πππ‘πππ¦.....: ππππ ππππ ππ ππππππ ππ πππππ ππππ (ππππ£ππ πππͺπ£π€π£π) π©ππππ ππ πΊπππππππ SEHEMU YA 12
Siku moja baadaye
Upande wa jijii Dar es Salaam, Karimu alikuwa mjini amesimama njiani anaongea na simu, hata hivyo Karimu alikuwa anamsubiri Rose ili ampatie funguo za geto la Ray. Hata hivyo alikata simu na kutembea tembea mpaka pale alipoweza kufika maeneo fulani, ndipo alipomuona Rose akiwa amesimama kajibanza kwenye kona.
Alimsogelea kwa karibu βShem vipi?βalimsalimia
βSafi kwema?β alimuuliza
βKwema, nimekusubiri sana ujueβ alisema Karimu
βJamani samahani sana, nilikuwa niko mbali, si unajua siku hizi naishi vingunguti?β
βVingunguti? Tangu liniβ aliuliza Karimu kama vile hajui
βNdio, jamani mwenzako hajakuambia?β Rose aliuliza
βHapanaβ
βOk nambie Karimuβ alisema na kuvuta pumzi
βAhβ¦mh ninaomba ufunguo kuna vitu kaniagiza niweze kwenda kuvichukua mule ndani tafadhaliβ alisema Karimu lakini binti alishika kiuno na kumtazama tu
βVitu gani?β aliuliza mtoto wa kike
βAhsh, we nipe ufunguoβ alisema Karimu huku akiwa anatabasamu, lakini bado binti alikaza
βtwende woteβ Rose aliongea huku akiwa ameshaanza kutembea kuelekea mitaa ya getoni kwa Ray
Kwa kifupi haikuwa mbali walitembea huku wakibishana
βIna maana Rose hauniamini kwamba amenituma au?β aliuliza
βNajua amekutuma, sawa, lakini nataka nikajue alichokutuma humo ndani maana mh, mimi simuamini sana yule mwanaumeβ alisema binti
βDooohβ Karimu alisema
Hata hivyo binti walifanikiwa kufika, wakasalimia majirani na kufungua mlango, binti alipomaliza kufungua mlango hivi, alichomoa ufunguo akaweza kuingia nao ndani kisha akaketi kwenye sofa
βIngia Karimuβ alisema binti, na Karimu aliingia akiwa anafikiria atamdanganya binti kwamba ametumwa nini hata hivyo alipata wazo βNiambie kwamba ni kitu gani amekutuma hapaβ alisema binti kwa hasira huku akionyesha kutokuamini kabisa kinachoendelea
βMh, ni hii sabufa, amenituma hapaβ¦niende nayo nyumbaniβ alisema jamaa
βSamahani sana, kwani wewe hauna ya kwako?β aliuliza
βsina, iliharibika, sasa hii nikasikilize kabla hajarudiβ
βOk powa chukuaβ alisema mtoto wa kike
βOk powa, lakini sasa shem?β aliita Karimu
βNambieβ
βWewe umehamia vingunguti kote kule, ili nisiwe nakusumbua kuja kunipa ufunguo siku nikitaka kuirudisha, basi ungeniachia ufunguoβ alisema
βHahaaaaβ¦β¦Karimu nimeshaujua mpango wenu, Ray anataka aniache, jamani khaa, sasa si aseme tu?β alisema binti huku machozi kama vile yalikuwa yanamlenga lenga hivi
βHamna shemu sio hivoβ
βNajua. Ila inauma jamani sawaβ¦.kama ananiachaβ alisema huku akiinama na kufuta machozi halafu akainua macho na kumtazama, βMi ufunguo sikupi, akitaka aje kuchukua mwenyeweβ alisema binti na kuinuka akatazama kule na huku
βSasa Rose ok basi sawa nitampigia simu ntamwambia umekataa kunipa vitu vyakeβ alisema Karimu
βmwambie tu, ila mimi ufunguo sitakupa, mpaka aje nimpe mwenyewe ndo nione imekuwajeβ
βOk powa mi nasepaβ alisema Karimu na kusogea mlangoni hata radio hakuchukua tena
βsepa tu, ila ndo hivyo mwambie akitaka ufunguo aje anitafute mimi mwenyeweβ¦..kama ana wasiwasi na mimi basi sikupi atajua mwenyeweβ alisema binti.
Karimu aliishiwa pozi, akatoka huku akijicheka na kutoa simu mfukoni akaandika message kwa Jamaa
βDAAAH TRICK YETU IMEGONGA MWAMBA, AMESHTUKA AISEEEβ¦.AMEKATAA KUNIKABIDHI UFUNGUO AKIDAI KWAMBA UNA NIA YA KUMUACHAβ alimtumia Ray
***
Kwa kawaida Ray alikuwa anachelewa sana kuamka, hivyo, ikiwa ni mida ya saa tano asubuhi ndipo alipojishusha kitandani na kuishika simu yake akakutana na message ya Karimu ila akaipuuzia na kuinuka akachukua mswaki halafu akaenda mpaka nje ya chumba.
Alipifika nje ya chumba alipata wazo la kurudi chumbani aweze kuchukua taulo, akaoge kabisa bafuni, alichukua taulo, sabuni ya kuogea kisha akatoka akipiga mswaki na kuzama bafuni, alimaliza kusawaki akaweka mswaki kwenye kadirisha kadogo ka bafuni, kisha akavua bukta na boxer zote akaziweka kwenye misumari nyuma ya mlango.
Hata hivyo alijisogeza pembeni mwa bomba la mvua akaanza kuoga taratiiibu huku akikumbuka tukio la nyuma. Alimkumbuka Rose jinsi alivyokuwa akiinjoy naye, akakumbuka ahadi nyingi ambazo pia alikuwa ameahidiana naye ahadi kama vile alikuwa an ampango wa kuoana na binti, lakin vivyo hivyo alikuwa amekula naye raha nyingi sana jijini Dar wakati yeye akiwa anafanya kazi ya kuuza katika duka la nguo la baba mmoja hivi.
βahahaaβ alitabasamu Ray alivyokumbuka kwamba kumbe binti alikuwa ana-date na boss wake kichwani alikumbuka mambo mengi ya maisha yake na Rose
Kumbe upande wa pili Naa alikuwa ameshaweka chakula jikoni, ilikuwa ni mseto amebandika, halafu akatoa kuni moto ukawa unawaka kwa mbalii, ndipo akatoka jikoni na kwenda mpaka chumbani kwake, kisha akalishika gauni akalivua na kubaki na chupi.
Alipomaliza kufanya hivyo, alichukua khanga na kujifungia kifuani mpaka mapajani halafu akatoka na kuingia katika chumba ambacho ndani kiligawanywa mara mbili, yaani kulikuwa na choo pamoja na bafu, vyote vikiwa na milango tofauti.
Alishika kitasa cha bafu akakizungusha bila kujua kuna mtu maana maji yalikuwa hayamiminiki, alipofungua hivi, alisikia sauti βWEWEEE. KUNA MTUβ yaani mpaka sentensi ile inaisha, ni kwamba mlango ushafunguliwa, binti hakuamini macho yake, alimuona live jamaa akiwa uchi, kabisa, amejipaka sabuni mwili mzima na maji alikuwa amefunga.
Jicho lisivyokuwa na nidhamu lilitangulia kuona ile sehemu kuu, ilikuwa imeinuka kidogo. Alibaki mdomo wazi, na kugeuza uso haraka akatoka akikimbia, huku akitetemeka na kuilaumu nafsi yake.
Aliogopa akaingia chumbani na kujilaza kitandani βHeee kumbe ameshaamka jamani khaaβ aliwaza mtoto wa kike huku akiifungua kanga yake akalala chali na kuanza kuwazia kile alichokionaβ¦β¦β¦β¦
Muendelezo ni 1000
Njoo WhatsApp 0743433005
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni