Kiukweli kwa hali halisi ya maisha ni kwamba watu ambao maisha yao ni duni wanaogopaga sana kutoka na watu ambao wana maisha mazuri, hii ni kwa sababu ya kushindwa kulinganisha hadhi, hivyo basi Nasma alivyokuwa anawaza kuhusu kija Raymond aliona kama vile anapoteza muda wake.
Ray alimaliza kupiga mswaki akaenda chumbani na kuchukua taulo halafu akazama bafuni akioga โMh yaani Rose atahisi nimesusa jamani wakati ninampenda sanaโ aliwaza akiwa bafuni anajipaka sabuni taratibu. Maana tangu jana usiku alikuwa hajamtakia hali mpenzi wake wa jijini Dar aitwaye Rose.
Ray alioga haraka haraka na kuweza kurudi chumbani, muda huo bado mama yake alikuwa amelala, ila mzee alikuwa akichunga mbuzi wake mitaa ya jirani kidogo kutoka pale nyumbani.
Ray alitoka nje akiwa ananukia, hasa, halafu akasimama mlangoni na kumuangalia binti aliyekuwa anamalizia kufagia uwanja โHeeeh kakaโ Nasma alianza mazoea
โNiniโ aliuliza Ray
โUnaoga kila saa?โ alimuuliza
โKawaida, nimezoea, kule Dar kulivyo na joto lazima mtu uoge mara 3 mpaka 4 kwa sikuโ
โMungu wangu ni nyingi sanaโ alisema Nasma
โVipi wewe umeoga kweli tangu jana, maana nguo zilikuwa hizo hizoโ Ray aliuliza
โHamna, nimeoga, sema tu, nguo mimi ninazo mbili tu, hii ya kufanyia kazi, ila nikishaoga navaa hiyo nyingine nzuri nzuriโ
โMungu wangu, nguo mbili? Unalipwaga mshahara?โ alimuuliza
โNalipwa, ila hivyo nyumbani kuna maisha magumu, mimi ndo mtoto ninayetegemewa na wazazi mshahara wangu huwa unatumwa kwao woteโ
โpole sanaโ alisema Ray binti akatikisa kichwa na kuinama kuendelea kufagia uwanja wake โUtaratibu wa chai vipi?โ aliuliza Ray
โngoja namalizia usafi halafu nitatengenezaโ alisema binti
โvitafunwa je?โ aliuliza
โKuna kiporo cha makandeโ
โHahahaaaโฆ..kwa huu mjengo nilijua maisha yamebadilika lakini kumbe wapi, embu niacheni kidogo bwana mimi ngoja nikalete vitafunwa nje huko.โ Alisema Ray na kurudi ndani akachukua pochi pamoja na simu yake akatoka nayo mpaka njiani.
Alitembea tembea, kutafuta sehemu yakununulia chapati au vitafunwa vingine vitramu vitramu, akaona kama vile pale kijijini hakuna, ndipo akaanza kuelekea katika duka moja kununua mkate. Kabla hajafika akasikia sauti
โWe, Raymondโ ilitokea sauti nyuma yake, akatazama, ni Elinami pamoja na Doto walikuwa na mizigo ya majani wanapeleka nyumbani.
โNaaamโ aliitika na kusimama kuwasubiri mpaka wakafika pale
โHeh, ni wewe unanukia barabara nzima jamani?โ Elinami alianza kumpamba lakini Ray alimtazama kwa aibu kidogo
โkawaida mbona?โ alisema Ray na kumgeukia Doto aliyekuwa pembeni mwa Elinami
โShikamooโ alisema Doto huku akimkagua kuanzia juu mpaka chini
โMarahaba wewe ni yupi tena?โ aliuliza
โDotoโ alisema binti
โDoto yupiโฆ.wale niliwaacha vidonchi juzi juzi wa kwa mama Saumu?โ aliuliza
โndioโ
โDuuuh mnakuwa sanaโ alisema na kumgeukia Elinami โVipi natafuta sehemu wanayouza chapati chapati ntapata kweli humu kijijini?โ aliuliza
โDah, ni mbali, karibia na sokoni muleโฆ.ina maana umeshasahau mitaa hii miaka michache tu mhโ alimuuliza binti
โHamna, maisha yamebadilika, mimi kipindi natoka huku kulikuwa hamna maendeleo hivi, nyumba kama hizi hapa, zote hazikuwepoโ alisema akizungusha mikono angani kuonyesha nyumba zilizokuwa zimejaa maeneo yale
โNdo hivyo lakini, wewe nyoosha na hii barabara, utapaona kumechangamka kidogo kuna kabango kameandika Rukia Foodโ alisema Elinami
โOk powa asanteโ Ray alisema, ndipo Elinami akamkonyeza kwa style fulani kwamba watawasiliana kwenye simu, halafu jamaa aliondoka zake akiwa anatabasamu.
Alimtext Rose, Good morning babeโ alitum text kwa furaha lakini kwa bahati mbaya Rose hakujibu kabisa ile message akajua labda yuko bize na kazi yeye akaendelea na mishe zake
Kweli alifikia maeneo fulani akaona bango dogo limeandikwa Rukia Food, akatazama, akamuona mama mmoja mweusi mweusi akisukuma chapati
โShikamooโ alisilimia ikabidi yule mama atabasamu bila kuitikia salamu yake โVipi mbona unatabasamuโ aliuliza
โHahaaaโฆ..hivi Ray, wewe ni wa kunipa shikamoo mimi?โ mama yule alimfahamu
โmhโฆ..mbona sijaelewa hapo kumbe najulikanaโ
โEmbu kwenda bwana,โฆ.yani mkishatoka mjini ndo zenu, mnasalimia hadi wadogo zenu, au kisa tumezeeshwa na maisha sisi?โ aliuliza
โMmmmh hapana, sister sorry sijakujua fulani hiviโ
โHumkumbuki dada mkuu wako ee?โ aliuliza huku akimkazia macho, ndipo Ray akakumbuka na kucheka
โHahahaaaaaaโฆโฆSawa bana, jina la Rukia likanichanganya kumbe Mwanaidiโฆok sorry sana nimezeeka mpaka kumbukumbu zimeenda mbali
โAchana na mimiโ alisema huyo dada kwa jeuri, halafu akainuka โEmbu nipe zawadi yangu kutoka huko mjini, au ndo umemletea mama yako peke yakeโ alisema mwanamke yule
โHamna cha zawadi wala nini, sikia, nifungie chapati 3 mara 4, nikale raha mimiโ alisema Ray
โMh yaani chapati kumi na mbili?โ aliuliza mwanaidi
โYaaapโ Ray alisema na kutoa noti ya 5000 kwenye pochi akamkabidhi, na yule dada alifanya hivyo โShilingi ngapi inakuwaโ aliuliza
โ3600โ alisema huyo dada maana chapati moja ilikuwa sh 300 tu
โOk iliyobaki kunywa sodaโ
โHayo ndo maneno, lakini kabla ya yote uoeeโ alisema mama huyo
Wote walibaki wakicheka huku akizidi kumuwekea chapati kwenye gazet. Akiwa anasubiri chapati pale ziwekwe vizuri, Doto alitokea akikimbia na kusimama pale, akamtazama Ray na kumuongelesha kwa sauti ndogo โUnisubiriโ alisema hivyo ili muuzaji asielewe kinachoendelea
Hata hivyo mwanamke huyo alimaliza akamuwekea vizuri na kumkabidhi Ray, wakaagana Ray aliondoka kwa mwendo wa taratibu huku akimsubiri Doto taratibu alikuwa anataka asikie kwamba ataambiwa nini
โDoto leo umekujua huku?โaliuliza
โNdio,naomba unipe chapati mbili haraka ninawahiโ alisema Doto
โsasa mbona kuna moja tu imebaki hizo zingine ni za kusubiriโ alisema mwanaidi
โBasi nipe hiyo hiyo, inatoshaโ aliongea kama vile ni mtu anawahi sana, kumbe alichokuwa anawahi ni kwenda kuongea na Ray.
๐ฟ๐๐ฃ๐๐๐ก๐๐๐ฆ.....: ๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐
(๐๐๐๐ฃ๐๐ ๐๐๐ช๐ฃ๐ค๐ฃ๐)
๐ฉ๐๐๐๐
๐๐ ๐บ๐๐๐๐๐๐๐
SEHEMU YA 08
Alipatiwa chapati moja na kuondoka akikimbia akamuwahi Ray, huku akicheka na kuhema sana
โWe kaka, shikamooโ alimuamkia
โKila saa??โ Ray aliuliza
โHamna jamaniโฆsi lazima nikuamkie kila saa kukuheshimu au hupendi?โ aliuliza
โOk marahaba, shule vipi?โ Ray alijifanya kukaza asijeonekana mrahisi
โShule nzuri, naona umeamua kuja kututembelea huku kijijiniโ alisema
โHahaaโฆ.nimekimbia maisha magumu Dar weweโ alisema Ray
โMmmh muongo, maisha magumu upendeze hivi?โ aliuliza dotto
Ray alicheka kisha akamuambia โBy the way sitakaa sana, nitaondoka siku sio nyingiโ
โUnawahi nini? Au ndo wifi? Eeh naona, ila sawa kweli hawezi kuwa wifiโ alisema mtoto huyo aliyekuwa na uchangamfu uliozidi kipimo
โKwanini asiwe wifi?โ Ray aliuliza
โHahaa.. wanaume wa Dar hizo mambo mh, kwani mnakuwaga nazo?โ alimuuliza ikabidi Ray asimame na kumshangaa kidogo
โHiv wewe ni Doto au nakufananisha, mbona unaongea sana?โ alimuuliza โMtoto wa juzi una maneno mengi hivi, kwanza wewe una miaka mingapi?โ aliuliza
โkumi na sabaโ
โKumi na saba ndo uongee hivyo?โ embu acha mambo yako, nambie kwanza mambo mazuri mazuri
โMazuri ni yapi kaka? Embu kwanza, kwani hayo niliyoongea sio mazuri? Mbona jamani watu wanayangโangโania wanasema ni matramuโ
โShitโฆโฆโฆ. Dotoโฆ.kimbia uende nyumbaniโ alisema Rayโ
โHaya sawa, basi nipe namba yako kakaโ
โElinami anayo kamuombeโ alisema Ray
โPoa byeโ
Binti alianza kukimbia mpaka akaenda nyumbani kwa Elinami huku akiwa ameificha chapati ili Elinami asishtuke kwamba alimfukuzia Raymond kule kibandani.
โEliiiโ alimuita mwenzake
โNini dogo?โ alimwambia kwa kejeli
โUna message unisaidie nimtumie mtu?โ aliuliza binti
Elinami alitoka na simu mkononi kisha akampatia binti mkononi โzipo chacheโ alisema na kuingia ndani kwake alikuwa anafanya fanya usafi kidogo
Kumbe ili ilikuwa ni gia ya binti kuiba namba ya Ray alitaka anagalao aibe namba ya Ray kwenye simu ya Elinami, hata hivyo bahati kama bahati ni kwamba Elinami alikuwa amesevu namba ya Ray hivyo hivyo kwa jina la Ray hivyo basi haikumpa taabu kuipata na kuiiba akaweka kwenye kisimu chake kidogo lakini kalikuwa ka-smartphone ka Samsung ambako ni version ya zamani halafu akamuita Elinami
โShogaaaโ alimuita โMi naenda kufua simu yako niweke hapa?โ alimuambia
โNyooo, uweke simu yangu hapo? Je wakiibaโ alisema mtoto wa kike huku akitoka ndani na kuipokea simu yake
โAsante eeโ alisema Doto halafu akakimbia kuelekea nyumbani alipofika nyumbani hivi alikunywa kwanza chai na ile chapati yake
*
Upande wa Ray yeye muda huo alikuwa yuko mezani anakunywa chai na mama yake baba bado alikuwa anachungua mbuzi na kondoo wake, Ray alikula chapati mbili halafu akawa hoi na kuachana nazo halafu akatoka nje ya nyumba akamkuta Nasma akiwa ameketi kwenye ndoo akabaki anamshangaa
โHivi wewe mbona hauna raha muda wote?โ alimuuliza
โSamahani kaka, ndo hivi nilivyo mimi nina raha sanaโ
โHaya kale chapati huko ndani halafu leo kwani una kazi ngumu sana?โ alimuuliza
โhapana ninafua nguo za baba na mama, halafu nitapikaโ alimuambia
โOk basi, wewe nenda kanywe chai pale kuna chapati, ukishamaliza oga vizuri nikuone na nguo nyingine hiyo ni chafu sanaโ aliongea akimnyooshea kidole maana alijua uchafu tu ndo kilichokuwa kinamponza mpaka wazazi wakawa wanamdharau
โSawa kakaโฆ.nilikuwa na mpango huo piaโ alijitetea baada ya kuhisi amedharaulika.
โSio kwamba nimesema hauogagi lakini nimekuambia uvae nyingine, wewe mbona mzuri ukiwa kila saa msafi basi utavutia saaanaaโฆhujioni ulivyo mweupe?โ alimuuliza, Nasma alitabasamu kwa furaha kwani mwanamke anapenda kusifiwa sana
Alitazama chini kichwa mwake wakiwa anawaza kwamba mh kanipenda au? Lakini ni kwamba jamaa alikuwa anamsaidia tu kimawazo, sio mapenzi.
Hata hivyo baada ya maneno hayo, Ray aliondoka akaenda mpaka pale baba yake alipokuwa anachunga mbuzi โMzee umeamkaje?โ alimsalimia
โsalama umeamkaje wewe?โ alimuuliza
โsijambo, emb niachie mbuzi hapa ukanywe chai kidogoโ alisema Ray na kusogea kwenye jiwe akaketi
โHuh, kuna chai na nini viporo mimi sili bwanaโ alisema
โHahaha, mzee unaringaโฆ kule nimeleta chapati za kutoshaโ alisema kijana huyo
โHapo sawaโ mzee alisema akitabasamu na kuanza kuondoka kuelekea nyumbani.
Sasa alipomuacha Ray pale na mbuzi Ray alipata muda wa kupiga selfie za kutosha, halafu aliwatumia marafiki zake aliokuwa akifanya nao kazi huko jijini Dar.
Lakini pia alimtumia Rose na kuweka captions โUkwen kuko hivi utakuja kweli wewe mtoto mayai?โ alisema na kumtumia, akaona imefika na kusomwa tayari, lakini haikujibiwa ikabidi ampigie simu aelewe labda ni ubize ama
โhallow Roseโ aliongea baada ya binti kupokea simu
โUsiniite tafadhali niache na maisha yanguโ Rose aliongea kwa hasira na kukata simu
Hilo suala lilimpa taabu sana Ray maana alimpenda yule mwanamke japo alikuwa akimsaliti mara kwa mara. Alimpigia simu tena na binti hakupokea simu kabisa ikabidi jamaa abaki akicheka maana hakuelewa kosa lake liko wapi โni hasira kisa sijamtafuta asubuhi atakuwa powa tuโ alijisemea Ray na kuchukua jiwe akamrushia kondoo aliyetaka kuondoka eneo lile.
Baada ya kumrushia jiwe, alisikia ujumbe umetumwa akaufungua ni namba mpya
โHello, uko pouwa?โ
โNiko powa, nani?โ alimuuliza
โMi Doto, ingia WhatsApp kuna kitu nimekutumiaโ alisema Doto
โOkโ Ray alijibu na kuingia WhatsApp moja kwa moja, alipongia hivi aliona ametumiwa ujumbe na Doto, akaingia kwenye msururu, alichokiona kutoka kwa Doto wala hakuaminiโฆโฆโฆโฆ..JE KAONA NINI?
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments