MR ARROGANT 17&18*
Baada ya siku ndefu ya kazi, Leon alimwambia Jasmine .
“Usiondoke leo nataka tuwe na usiku wa tofauti mimi na wewe .
Jasmine alitabasamu kwa aibu. Hakujua Leon alikuwa na mipango gani, ila moyoni alitamani kila kitu kizuri kitokee.
" Watu wote wameondoka?
" Ndio hao tumebaki mimi na wewe na mlinzi getini.
" Basi hatuna muda wa kupoteza twende zetu.
Walitoka ofisini huku Leon akiwa kabeba pochi ya Jasmine
Walipofika nje walipanda kwenye gari ya kifahari ya Leon.
Waliondoka na kwenda sehemu moja ambayo ilikuwa ni uwanja kama wakichezea mpira . Gari ilisimama hapo leon akawasha taa full
, akaweka muziki wa romantic ukawa unasikika taratibu ndani yake. Harufu ya air freshener na manukato ya Leon vilitawala kwenye gari .Jasmine alimuangalia Leon aliweka mkono wake juu ya mkono wake, akitabasamu kwa jicho la kimahaba.
" Jasmine niambie unataka nikufanyie nini ili uamini kuwa nakupenda?
" Matendo yako tu yananifanya niamini kuwa unanipenda.
" Upo tayari kuwNzisha familia na mimi?
" Unauhakika na unachosema? Aliuliza jasmini kama vile haamini
" Ndio sitaki tupotezeana muda nataka uwe wangu wa halali kila nitakapokuhutaji basi nikupate kwa urahisi sio kama hivi zimetulia mara Nadia anapiga simu na kutaka urudi nyumbani haraka.
" Mimi nipo tayari hata leo .
Mara simu ya Leon iliingiza ujumbe na Leon alichukua simu yake na kusoma. Kisha akatabasamu.
" Tunatakiwa kwenda sehemu.
" Wapi? Nilijua leo umepanga tuwe hapa.
Leon alicheka
" Yani mtoto mzuri jana wewe nikulete sehemu kama huu? Haiwezekani.
Leon aliwasha gari wakaondoka.
Walifika kwenye ukumbi wa kifahari uliopambwa na taa za bluu na nyeupe, na muziki wa live band ukicheza nyimbo laini za mapenzi. Meza yao ilikuwa karibu na jukwaa, mishumaa ikiwaka na maua mekundu ya waridi yakiwa katikati.
Leon alimsogelea Jasmine, akamwambia kwa sauti ya chini sana kana kwamba ni siri .
“Unajua Jasmine, kila mara nikikuona, moyo wangu unapiga muziki wake wa pekee.
Jasmine alitabasamu. Leon akaendelea kusema
"Leo, nataka ucheze na mimi muziki huo.
Leon alisimama akanyosha mkono kwake. Jasmine akajisikia aibu lakini hakuweza kumpinga. Alimpa mkono wake leon alishika vyema kiganja cha Jasmine wakasogea kwenye uwanja mdogo , mwanga wa taa ukimulika sura yao, Leon alimzungusha taratibu, akimshika kiuno kwa upole. Miili yao ikakaribiana zaidi, pumzi zikigongana, na macho yao kuzungumza zaidi ya maneno.
Muziki ulipokuwa unaimba kwa hisia Jasmine alijikuta akiegemea kifuani mwa Leon, akisikiliza mapigo ya moyo wake. Leon naye, akamshika zaidi kwa nguvu kana kwamba hataki tena kumwachia.
Hakukuwa na maneno mengi vitendo ndio vilipewa kipaombele kwa usiku huo.
Leon alisogea karibu na sikio la Jasmine alimnong’oneza kwa sauti nzito ya kiume iliyokuwa na msisimko fulani, yenye joto la mapenzi:
“Jasmine huu ndio mwanzo wa muziki wetu, na nataka ucheze nami hadi mwisho wa maisha.”
Macho ya Jasmine yalijaa machozi ya furaha, alinyanyua macho akamuangalia na kusema kwa sauti yenye haiba ya kike
“Na mimi sitaki muziki huu uishe kamwe.”
Leon naomba nikuombe kitu.
" Haina haja ya kuomba sema tu mpenzi.
" Leo siwezi kwenda kulala mwenyewe nataka kulala pembeni yako.
Leon akifumba macho alihisi msisimko.
" Sawa mama twende ukanifanye nilale usingizi mzito wenye amani.
Baada ya maneno hayo, kimya kifupi kilitawala. Jasmine alibaki akimtazama Leon kwa macho yaliyojaa upendo na shauku. Leon naye alimwangalia kwa ukimya, moyo wake ukicheza midundo isiyoelezeka.
Alinyanyua mkono wake, akapapasa shavu la Jasmine kwa upole.
“Jasmine… unajua ni mara ngapi nimewaza kuhusu hii siku? Lakini leo nimehisi ndoto yangu imekuwa kweli.”
Jasmine akatabasamu kwa aibu, akainamisha uso wake taratibu. Lakini Leon akainua kidevu chake kwa kidole gumba, macho yao yakakutana tena. Dakika hiyo ikawa kama dunia imesimama kwa ajili yao pekee.
Wakati huo muziki wa live band uliendelea kuimba nyimbo za mapenzi, taa za ukumbi zikizidi kuangaza nyuso zao. Leon hakusubiri tena. Alisogea, akabusu midomo ya Jasmine kwa upole . Jasmine alijibu busu hilo bila kujizuia, mikono yake ikimkumbatia Leon kwa nguvu.
Usiku ule, kila kitu kikawa kimesahaulika mashaka, migongano, na hofu. Kilichokuwepo ni hisia kali za mapenzi.
Baada ya muda, Leon akamnong’oneza tena,
“Twende nyumbani Jasmine… leo nataka nipate joto lako kwa ukaribu zaidi .
Jasmine Alikubali moyo wake ukiwa tayari kwa hatua mpya ya safari yao ya mapenzi.
Offer offer
Soma yote kwa sh 500
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi










Maoni