Jasmine alinyanyua begi la Leon kwa utulivu, akitembea huku akimfuata .
Leon akatembea haraka kuelekea kwenye gari lake la kifahari. Akafungua mlango, kisha akamkodolea macho Jasmine ambae alikuwa kasimama.
“Ingilia haraka tunachelewa.
Jasmine alipanda akakaa kwenye kiti cha pembeni ya dereva, leon akafunga mlango kisha bar akaenda kupanda na kuwasha gari.
Safari yote ndani ya gari, kimya kilitawala. Leon alishika usukani kwa nguvu, macho yake yakiwa barabarani lakini akili yake ilikuwa ikisumbuliwa na kitu kimoja busu la Jasmine. Kila alipojaribu kulisahau alishindwa hasa alipokuwa akimuona yupo karibu yake.
Jasmine, kwa upande wake, alikaa akimuanga Leon taratibu, macho yake yakiwa na uhakika wa ushindi. Aliinua mdomo wake na kusema kwa sauti nyororo:
“Boss… unajua leo umependeza sana. Nikisema hujui kuvaa, nitakuwa mnafiki. Lakini nikisema hujui kupenda… nitakuwa sahihi kabisa.
Leon akamgeukia akimkazia macho kwa hasira.
“Jasmine, nakushauri uache huu mchezo wako. Kuna mambo ya kitoto na kuna maisha ya kweli. Mimi siyo mwanaume wa hiyo michezo yako.
Jasmine akatabasamu, akavuta pumzi kwa utulivu kisha akajisogeza kidogo karibu naye.
“Mimi pia sichezi, Boss. Nataka tu nikufanye ukubali kitu ambacho tayari moyo wako unaamini. Unaweza kunidanganya kwa maneno, lakini macho yako kila mara yananiambia ukweli.
Leon alijisikia damu zikimchemka. Alitaka kumfokea lakini badala yake, akajikuta akishika usukani kwa nguvu zaidi kana kwamba anapigana na nafsi yake.
Walipofika kwenye hoteli kubwa ya kifahari walishuka wote.
" Hii ndio sehemu ya mkutano?
" Ndio . Jasmine nakuomba kwa mara nyingine tena usije ukanifanya michezo yako ya ajabu huku kuna watu wa heshima.
" Kweli leo upo serious yani mpaka imetangulia neno samahani! Basi boss wangu wala usijali nitakulinda heshima yako kama boss wangu.
Walipoingia ukumbini, kulikuwa na watu wa heshima pia walionekana kwenda na masecretary wao, Jasmine akatembea pembeni yake kwa ujasiri, kana kwamba ana haki ya kuwa pale. Walifika sehemu kuna dada mmoja mrembo alimfuata leon wakakubaliana huku Leon aliachia tabasamu ambalo Jasmine hakuwahi kuliona .
" Jamani leon nilikumiss sana.
" Nilikumiss pia miss Leyna, vipi hali yako ipo sawa.
" Nipe imara sana hofu yangu ni kwako mr handsome.
Leon akicheka kidogo
" Niko poa sana , nimefurahi kukuona tena.
Walishikana mikono wakawa wanatembea kuelekea kwenye meza iliyoandaliwa kwaajili ya mkutano .
Kitendo kili kilimuumiza na kumvunja moyo Jasmine aliamini kuwa haba thamani ya kuwa na Leon kile alichokuwa anaongea kila siku ilikuwa anamaanisha.
Alibaki nyuma huku akiwa kabeba begi la pc .
Leyna aligeuka nyuma akamuangalia Jasmine alafu akauliza.
" Huyu ni nani?
" Secretary mpya anaitwa Jasmine.
" Ok.
Waliendelea kutembea mpaka walipofika kwenye meza kubwa ya duara Leon alivuta kiti akakaa na yule mwanamke akakaa pembeni yake huku akiwa inasimamiwa na binti mmoja ambae alionekana kama security wake
Na Jasmine alisimama kando ya Leon.
Alifungua mkoba na kutoa laptop ya Leon na kuiweka mezani.
Kikao kilianza watu walikuwa makini kufuatilia .
Jasmine alipokuwa kasimama kuna mwanaume mmoja alikuwa anamuangalia sana na walipokutana macho aliachia tabasamu na Jasmine hakuwa na hayana alimuonyesha tabasamu ndogo.
Baada ya mkutano kuisha huyo
Mwanaume aliyejulikana kama Mr. Gilbert mfanyabiashara kijana tajiri na anayejiamini alinyanyuka na kutembea moja kwa moja kwenye meza ya Leon. Akiwa na tabasamu la kujiamini, akampa Jasmine mkono.
" Habari mrembo.
" Salama.
" Naitwa Mr Girbet nitafurahi kama utapenda tufahamiane.
Jasmine akatabasamu alafu akajitambulisha.
" Naitwa Jasmine.
" Waoooo jina zuri sana kinaendana na jinsi ulivyo . Wewe ni mzuri Jasmine.
Jasmine alikuwa anatabasamu tu wakati huo leon alikuwa akimuangalia kwa hasira.
" Samahani Jasmine tunaweza kuungana pamoja kwenye chakula cha mchana?
" Sasha nipo na boss wangu Mr Leon.
Girbet alimuangalia Leon alafu akasema.
" Tafadhali mr Leon naomba ruhusa ya kupata chakula na secretary wako.
Kabla Leon hajajibu Leyna akamjibia.
" Kwakuwa hakuna kazi kwa sasa mruhusu aende naye na mimi nitakupa chakula cha mchana na wewe.
Jasmine hakuona haja ya kukataa aliona bora akabadilishane mawazo na watu wengine kuliko kukaa kuona Leon akitoa tabasamu la upendo kwa mwanamke mwingine.
Walipotaka kuondoka Leon alimshika mkono Jasmine.
“Hapana. Leon alisema kwa sauti ya chini l macho yake yakimkazia Gilbert kwa ukali wa simba.
“Huyu ni secretary wangu. Yuko hapa kwa ajili ya kazi, siyo kwa ajili ya starehe au kwenda kula.
Jasmine akamkodolea macho Leon, moyo wake ukicheza kwa furaha ya siri. Tabasamu dogo likatokeza midomoni mwake
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments