Sasha alicheka kwa sauti ya kebehi, akaweka karata mezani kwa nguvu. Alimuangalia tena usoni Jasmine na kuangua kicheko kikubwa.
" Sasa unacheka nini?
โJasmine, hivi kweli unajua unachokisema? Yule Leon siyo mwanaume wa mchezo. Ukicheza na moyo wake unaweza kuumia vibaya.
Jasmine akakunja midomo yake kwa jeuri na kumuangalia rafiki yake.
โSasha, mimi sijawahi kushindwa kwenye mchezo yangu, nakuhakikishia Leon atanibeba kama mtoto mdogo, ni suala la muda tu.
โUsijiamini sana, Jasmine. Wanaume kama Leon mara nyingi ni hatari. Ana pesa, ana sura, na ana jeuri ya kutosha. Ukijaribu kumteka, unaweza kujikuta wewe ndiyo unayejikuta mteka.
Jasmine akatabasamu huku akiinua kikombe cha maziwa na kunywa kidogo.
โSasha, nashukuru kwa tahadhari yako. Lakini moyo wa Leon tayari nimeuona unavunjika taratibu. Ni lazima atakubali kuwa na mimi.
" Sawa na mimi huku najiandaa kubembeleza mtu ambae atatumika na kuachwa vibaya .
" Maneno yako hayatanikatisha tamaa.
" Sawa nipo hapa.
" Wewe jiandae kuwa na shemeji.
" Mimi na ujeuri wake wala sitaweza kumuita shemeji.
" Kwangu mimi atabadilika tu.
" Atabadilika vipi wakati wewe mwenyewe ni jeuri?
" Tulia mama angalia mchezo utakavyoenda.
Kesho yake ofisini, hali ilikuwa tofauti. Leon aliingia akiwa amevalia suti ya navy blue iliyokaa mwilini mwake kwa ukamilifu. Uso wake ulikuwa mkali kama kawaida, lakini kulikuwa na kitu tofauti machoni mwake. Wafanyakazi wote walihisi hali ya hofu ikiwazunguka walipoona Leon akipita.
Jasmine, aliyekaa mezani kwake, alinyanyua macho kwa makusudi na kutabasamu.
โ habari za asubuhi Boss. alisema kwa sauti ya kuvutia.
Leon hakujibu alimuanga kwa sekunde chache, kana kwamba anatafuta maneno ya kumwambia, kisha akasema kwa sauti thabiti:
โ hakutaka Ofisini kwangu sasa hivi.
Jasmine alinyanyuka taratibu, akipiga hatua za kujiamini kuelekea ofisini kwa Leon.
Alipoingia, Leon alimwangalia moja kwa moja, macho yake yakiwa hasira na kitu kingine kisichoweza kufichika.
โJasmine, nataka tuweke mipaka. Hii michezo yako ya utani lazima iishe. Hapa ni kazini, na mimi ni boss wako. Sio mtu wa mchezo wako wa mapenzi.
Jasmine akasogea karibu, akiinamisha kichwa kidogo huku tabasamu la kuvutia.
โBoss, unajua tatizo lako? Unajifanya mkali, lakini ndani yako unaniacha niishi Kila ukiniangalia macho yako yananiambia ukweli tofauti na maneno yako.
Leon alijaribu kugeuka, lakini Jasmine akamsogelea zaidi,
โJasmine, rudi nyuma,โ alisema kwa sauti ya chini .
โKwa nini?โ Jasmine alijibu kwa sauti laini. โAu unaogopa kwamba utanibusu, utakuwa mfungwa wangu rasmi?โ
Kimya kizito kikatawala. Leon alibaki, Miguu yake kana kwamba imeganda sakafuni. Hali ile ilikuwa ya hatari zaidi.
Kwa mara ya kwanza, Leon hakuwa na majibu ya haraka.
Alitaka kuongea kitu lakini alisita.
" Niambie Boss unataka nini kwenye maisha yangu? Kunileta hapa ilikuwa ni kunikomesha au kulikuwa na jambo lingine?
" Tafadhali Jasmine hebu songea huko sitaki kuongelea hayo unavyotaka najua akili yako inachofikiria lakini kusema kweli mimi siwezi kuwa na wewe, sijawahi hata kukutama....
Kabla hajamaliza kuongea alishitukia midomo ya Jasmine imekutana na midomo yake .
Leon alitulia kwa muda , Jasmine alimbusu kisha akarudi nyuma kidogo.
Akatengeneza vizuri suti yake alafu akaongeza kwa sauti ya chini.
" Uwe na kazi njema boss.
Jasmine aligeuka taratibu akapiga hatua ndogo kuelekea mlangoni , alifungua mlango na kutoka bila hata kugeuka nyuma. Baada ya kufunga mlango Leon akijisemea.
" Ni nini hiki anafanya huyu binti ? Anamaanisha nini? Au anachofanya ni moja ya kisasi chake cha kijinga?
Leon alibaki akiwa amesimama huku akiwa anafikiria kile alichofanyiwa na Jasmine.
" Hapana sitakiwi kuamini akili za huyu msichana Mjanja anaweza kucheza na akili yangu ili aje kunidhalilisha .
Leon alianza kuwa na tahadhali kubwa kwa Jasmine aliamua kuacha mazoea kabisa na kuweka utani pembeni alikuwa Bize na mambo yake hata Jasmine alipokuwa akimchokoza na maneno yake ya chokochoko hakumjibu .
Lakini licha ya kufanya yote hayo na kujiepusha na Jasmine hisia za kumtaka bado zilikuwa zinamsumbua.
Siku moja leon alikuwa anataka kutoka kwenda kwenye mkutano alitakiwa kwenda na jasmine.ilimbidi amuite Jasmine na kuongea nae.
" Jasmine leo nitatoka na wewe tunaenda sehemu muhimu yani namaanisha tunaenda kwenye mkutano wenye heshima huo ujinga na kichaa chako naomba uuache hapa hapa.
Aliongea Leon huku akiwa kamtolea macho na Jasmine alikuwa anatabasamu tu.
" Wewe nirembulie macho kama mdoli alafu ukafanye Madudu huko utaona nitakachofanya. Chukua hilo begi langu nifuate.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments