MR. ARROGANT ๐๐ฅ* *1----2* *
*SEHEMU YA KWANZA*
Ilikuwa majira ya saa kumi jioni msichana mrembo (Jasmine) aliye kuwa amevalia gauni lake zuri la rangi ya gold na kikoti cheupe alikuwa anatembea kando ya barabara huku akibinyeza simu yake ni wazi alikuwa akichati na mtu.
Ghafla lilopita gari na kumwagiwa maji ya mvua yaliyokuwa yametuama kwenye dimbwi.
Jasmine alishituka akasimana na kuanza kutoa maneno.
" Hivi nyie wenye magari mna nini lakini ? Anajiona nimemaliza kila kitu kwenye hii dunia ... Aliongea maneno mengi sana lakini ile gari haikusimama.
" Huyu mtu jeuri sana na hawa watu nawapenda mno ipo siku tutaonana tu .
Wakati Jasmine anasema hivyo kumbe alikuwa ameshika namba za ile gari.
Baada ya wiki mbili kupita akiwa kwenye mizunguko yake alipita sehemu akalikuta ile gari imesimama mbele ya super market moja.
Alisoma namba na kuhakikisha ndio ile gari iliyomwagika maji.
Alitabasamu kidogo kisha akasema.
Dawa ya jeuri ni jeuri sasa ngoja nilipize. Aliangalia kila upande akaona watu wapo Bize na mambo yao.
Aliangalia chini akaokota kipande cha chupa alafu akasogea karibu na gari na kuanza kukwambia rangi ya gari huku akiandika.
" Acha ulimbukeni hata sisi tunayo magari ila tuna nidhamu .
Alipomaliza kuandika akasimama na kusoma kwa sauti alafu akasema.
" Pumbavu ujumbe utamfikia.
ile anageuka anakutana na kijana mtanashati ambae alikuwa akimuangalia huku akiwa kakunja uso wake mpaka matuta yakajichora usoni kwake.
kijana huyo hakuwa mwingine ni Leon Maxwell tajiri mwenye sura ya kuvutia na jeuri isiyoelezeka. Alijulikana mjini kama Mr. Arrogant mtu asiyejali hisia za wengine, mwenye dharau na anayeamini kila mtu yuko chini yake.
Leo alimsogelea karibu
" Kwanini umeharibu gari yangu?
" Sijaharibu nilikuwa najaribu kufikisha ujumbe.
" Ujumbe gani wa kipuuzi?
" Upuuzi uliuanza wewe juzi, kwani ilinimwagia maji machafu na ukaisha kuchungulia , ukiniangalia kama takataka kisha ukaendelea na safari yako.
" Unajua hii gari yangu ina thamani gani?
Jasmine alitabasamu kwa jeuri, mikono yake ikiwa kifuani kwake.
โSijui, na sitaki kujua Lakini najua kitu kimoja thamani ya gari lako haiwezi kulipa heshima unayopaswa kuwapa binadamu wengine. Ndio maana niliandika ili nikufundishe nidhamu kila ukisoma hapo utakuwa unakumbuka unatakiwa kuwa na heshima pamoja na utu.
Watu waliokuwa karibu na supermarket wakawa wamesimama, wakifuatilia mrumbano yao kama sinema ya bure.
Leon alicheka kwa dharau, akamuangalia Jasmine juu,chini kisha akasema kwa sauti ya kudharau:
โKwa mara ya kwanza nimekutana na mwanamke mwenye ulimi mrefu kuliko akili yake.
Umejiingiza kwenye matatizo makubwa bila kujua.
Jasmine akamkaribia kwa hatua moja zaidi, macho yake yakimwangalia bila woga.
โNa wewe kwa mara ya kwanza umekutana na mwanamke ambaye hakubali kuonewa hata kidogo. Umenimwagia maji, sasa nimekulipiza. Ni rahisi tu, haki sawa.
Leon hakupenda aliona kama anadhalilishwa. Kwa mara ya kwanza alihisi kuvunjiwa heshima Hakuna aliyewahi kumsimamia kwa ujasiri namna ile, tena mbele za watu.
Aliinama karibu na sikio la Jasmine, akasema kwa sauti ya chini lakini kwa ukali:
โUmeamua kucheza na moto, na moto wangu unachoma vibaya. Nitaona utavumiliaje.
Jasmine akasogea nyuma hatua mbili, lakini tabasamu lake halikupotea usoni mwake
โNami nataka kuona moto wako unachoma kiasi gani, Mr. Arrogant.
Walitazamana kwa sekunde chache, kukawa kimya .
Leon akapanda gari lake, akawasha gari na kuondoka huku vumbi kidogo likitimka
Jasmine alibaki akitabasamu, akipiga makofi kwa kujipongeza.
โLeo nimekutana na jeuri mwenzangu. Huu mchezo utakua tamu sana.โ
Hapo ndipo mchezo wa jeuri dhidi ya jeuri ulipoanza rasm.
MR. ARROGANT ๐๐ฅ 2
Siku zilisogea Jasmine akiwa kwenye duka la shangazi yake wakiwa wanaongea.
" Shangazi sasa inakuwaje kuhusu kupata kazi bado haujaongea na huyo rafiki yako.
" Amesema mpaka mwezi wa sita ndio kutakuwa na nafasi za kazi .
" Kwahiyo nitakaa miezi yote hii bila kazi. Sasa nini maana ya elimu yangu nimesoma kwa bidii changamoto kwenye ajira , daaaah inakatisha tamaa sana.
"Haifai kukata tamaa kabla haujafanikiwa.
Jasmine aliondoka na kwenda kupanga nguo mpya ambazo zilikuwa zimeingia muda sio mrefu na wateja walianza kuja kununua mali mpya maana shangazi yake aliwapigia simu wateja wake.
Muda uleule, akiwa anapanga mizigo ya dukani, ghafla gari jeupe likasimama mbele ya duka, mlango ukafunguliwa na mtu akashuka taratibu.
Hakuwa mwingine, bali ni Leon Maxwell. Aliekuwa amevalia Suruali yake nyeusi iliyokaa fit, shati la kifahari lililofunguliwa kifua, na miwani ya nyeusi iliyositiri macho yake makali. Alitembea kwa kujiamini, kila hatua ikionekana kama inatetemesha dunia.
Jasmine alishika kiuno, akamwangalia moja kwa moja.
Leon alienda kukutana na Nadia shangazi yake Jasmine.
" Habari.
" Salama Leon karibu.
" Nimeshakaribia nataka kuona mali mpya.
" Kuna binti yangu yupo huko unaweza kwenda kuangalia.
Leon alianza kuangalia nguo kabla hajamuona Jasmine .
Alivyozidi kusogea ndio wakitaja uso kwa uso. Leon alivua miwani yake na kumuangalia .
" Wewe kivuruge tumekusanya tena leo?
โLeo umekuja kununua nini? Au umekuja kuomba msamaha?โ aliuliza kwa dhihaka.
Leon akatoa macho yake makali yakimkodolea.
โMsamaha? Mimi? Kukuomba msamaha wewe?โ alicheka kidogo, sauti kwa dharau alafu akaendelea kusema
โHapana, nimekuja kukuonya. Mara ya pili ukigusana na gari yangu au mali yangu, utajuta kuishi kukifahamu.
Jasmine alicheka kwa sauti, wateja waliokuwa dukani wakageuka.
โJeuri zako hazinitishi Nimeshakuambia mimi sio wa kuonewa. Sasa ukitaka vita, vita tutapigana. Nani ashindwe ni hadithi ya baadaye.โ
Kwa mara ya kwanza, Leon alibaki kimya sekunde mbili, akimtazama tu. Ndani yake moyo ulianza kushtuka kulikuwa na kitu cha ajabu kwa msichana huyu. Ujasiri wake, namna anavyoongea bila woga .
Baada ya Nadia kuona kuna kitu hakipo sawa alisogea karibu.
" Jasmine kuna shida gani na mteja wangu?
Kabla Jasmine hajajibu Leon alijibu.
" Usijali dada Nadia mimi na Jasmine tunakutana na tupo kibiashara nenda kaendelee na wateja wengine.
" Sawa.
Nadia aliondoka akawa acha .
Jasmine alimuangalia usoni na kuachia tabasamu .
Leon nae alitabasamu kwa jeuri, akamsogelea karibu kabisa.
โBasi Jasmine kuanzia leo mimi na wewe utakuwa na mchezo wa paka na panya. Tuone nani atashindwa.
Jasmine naye hakurudi nyuma.
โNaona unaona kuwa wewe ni paka. Mimi si panya, mimi ni simba.โ
Kuna wateja wawili walikuwa walishindwa kujizuia, wakaanza kucheka kimnya kimnya
โHawa watu wawili wakioana lazima nyumba iwake moto.
Leon a akaondoka taratibu huku tabasamu la kijanja likibaki usoni mwake aliendelea kuchagua nguo huku Jasmine akabaki akitetemeka kwa hasira, lakini ndani ya moyo wake kulikuwa na kitu kipya mapigo yake ya moyo yalikuwa yanadunda haraka mno.
Alijisemea kimoyomoyo:
โHuyu Mr. Arrogant atanitesa lakini sitakubali hata kidogo.
Leon alichagua nguo anazitaja alipomaliza alipitia alipokuwa anapanga nguo Jasmine akasimama na kusema.
" Jasmine binti mwenye jina tamu lisiloendana na matendo yake. Nadhani tuna safari ndefu na huu ni mwanzo .
" Sawa mr arrogant. Safari ndefu niya kwenda mbinguni bila shaka tutaenda pamoja huku tukiwa tumeshikana mikono.
Leon alitoa tabasamu dogo kisha akaenda kulipia nguo zake na kuondoka.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi










Maoni
*1----2*
*