Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

MR ARROGANT 💎 🔥 8

25th Aug, 2025 Views 44



Macho ya Leon na Jasmine yalikuwa yamefungwa kana kwamba kuna sumaku iliyokuwa ikivutana. Pumzi zao zilikutana, joto la miili yao likawa karibu mno. Leon alinyosha mkono wake kana kwamba anataka kugusa shavu la Jasmine, lakini kabla hajafanya hivyo mlango ulifunguliwa kwa kwa nguvu na kufanya washituke na kila mtu akarudi nyuma.
“ samahani Boss!” alijitokeza Paul, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni . Leon alimuangalia huku akiwa kakunja sura yake .
“Samahani, kuna dharura ya mikataba inahitaji sahihi yako haraka.
Kwa sauti kali Leon alijibu:
“Paul! Wewe huna adabu? Huoni niko busy? Toka nje nitakuita!
" Samahani boss...
Paul alijifuta jasho, akatoka haraka huku akionekana kuchanganyikiwa.

Baada ya mlango kufungwa tena, kimya kilitawala. Jasmine akamuangalia Leon kwa macho ya kejeli, akasema kwa sauti ya utani:
“Kwa hiyo Boss, ndiyo unaona suluhisho la kila kitu ni kufoka?
" Na wewe hebu kaa hapo umalize kazi , au chukua nenda kamalizie huko maana hapa unanichanganya tu kwa maneno yako ya kijinga.
"Ungekuwa umenibusu sasa hivi tusingekuwa tunafukuzana hivi?

Leon akashituka paji lake la uso .
" Jasmine sitaki ujichanganya na wala sikuwa na nia ya kukubusu .
Jasmine alicheka kicheko kidogo cha kuvutia.
“Ndiyo maana unasema hutashindwa, lakini moyo wako umeshajisalimisha zamani boss Wewe ni jeuri kwa ulimi, lakini moyo wako ni mfungwa wangu.
Leon akamsogea karibu tena, safari hii akimwangalia kwa macho makali lakini yenye kitu kisichoweza kufichika.
“Jasmine, usinipe sababu ya kukufukuza kazi. Sijazoea mtu kunizungumzia hivi. Naamini hakuna mwanamke anayeweza kunichanganya mimi.
" Itakuwa vizuri kama unanifukuza ili niondoke na ushindi wangu.

Kwa sekunde kadhaa ukimnya ulitawala ,Leon akageuka kwa ghafla, akachukua koti lake, akasema kwa sauti kali:
“Kesho utaripoti kazini saa moja kamili asubuhi. Na usithubutu kuchelewa kuna kazi muhimu ya kufanya.
Leon aliondoka , Jasmine alicheka kimoyomoyo huku akipumua kwa nguvu.
“Nimekushika, Leon. Na siwezi kukuachia mpaka nikushinde kwa moyo hili jaribio zuri sana kwangu.

Kesho yake, majira ya asubuhi Jasmine aliwahi kazini mapema kama alivyoamriwa na Leon. Alikuwa amevaa gauni la rangi ya baby yellow lililokuwa limeshika mwili wake mzuri na kuacha shingo yake nyembamba ikionekana vizuri.
Alijua kabisa leo kuna kitu kipya kitakachotokea, na aliahidi moyoni mwake atamshinda Leon katika mchezo wa hisia.

Alipokaribia karibu na jengo la ofisi Ghafla gari dogo lililokuwa linaingia kwa kasi halikujali hata alama za usalama, likapita karibu mno na Jasmine. Wakati anakwepa Aliteleza akajikuta anataka kuanguka. Mara akasikia
“kuwa muangalifu. sauti kali ya kiume ilisikika alafu kwa sekunde moja alihisi kushikwa kiunoni. Alipogeuka kuangalia alimuona Leon.
Waliangalia huku bado Mikono yake ilikuwa imezunguka kiuno cha Jasmine, pumzi zao zikakutana tena. Jasmine macho yake yakatazama macho ya Leon, moyo wake ukadunda kwa kasi lakini hakutaka kuonyesha udhaifu huo.
Wakati huo baadhi ya wafanyakazi walikuwa wameduwaa wakiangalia kama vile wanaangalia tamthilia.
“Boss, sasa umeanza kazi mpya ya kuwa ‘bodyguard’ wangu?” Jasmine alisema kwa sauti ndogo lakini ya kudhihaki.
Leon hakujibu alishusha pumzi kwa nguvu, macho yake yakiwa bado yameganda kwa sura ya Jasmine. Kisha taratibu akamnyanyua na kumweka vizuri kando.
“Huna akili kabisa, Wewe unadhani maisha ni mchezo? Kama sio mimi ungekuwa chini sasa hivi!” alisema kwa ukali, lakini sauti yake haikuwa na mkali kama siku zote kulikuwa na kitu cha upole kisichoweza kufichika.
Jasmine akajifanya kama vile anaumia, akashika mguu wake kwa makusudi.
“Ah… nafikiri nimejiumiza kidogo,” alisema kwa sauti dhaifu, akinyanyua macho yake kwa ulegevu kumuangalia Leon.
" Wewe si jeuri ninekusaidia ukaanza maneno yako ya ajabu pambana na hali yako.
Leon aliondoka na kumuacha akiwa kasimama.
" Patrick samahani naomba msaada wako tafadhali.
Kabla Patrick hajafika alipo Leon aligeuka kuangalia.
" Hey Patrick hebu nimfuate haraka achana na huyu msichana asiyekuwa na shukurani.
Patrick waliachana na Jasmine akamfuata boss.
Jasmine akatabasamu huku akisema:
Huu ndio mwanzo wa mtego wangu. Nitakufanya uingie kwenye hisia zako mwenyewe Leon.

Jioni Jasmine alikaa na Sasha wanacheza karata lakini akili yake ilikuwa mbali sana .
" Jasmine nasubiri ucheze kama huna ramba. Jasmine alitupa karata mezani.
" Aaaaah mchezo wenyewe hata sikuelewi.
" Wewe mjinga nini umeona nataka kukufunga unajishauwa huelewi.
" Sasha mwenzio akili yangu haipo sawa unajua namuwaza sana Leon.
" Unamuwaua kivipi?
Yani ile ujeuri wake imenivitia mpaka nimejikuta naanza kumpenda.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MR ARROGANT 💎 🔥 8  >>> https://gonga94.com/semajambo/mr-arrogant-8

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest