MR. ARROGANT ๐๐ฅ 3
Wiki moja badae Jasmine alikuwa anajiandaa kutoka mara Rafiki yake mkubwa, Sasha, alifika nyumbani kwao akiwa na furaha kubwa.
โJas! Leo nimekuja na habari nzuri.
" Habari gani?
"Hii ni nafasi yako. Kuna kampuni kubwa imetoa tangazo la kazi. Wanaajiri receptionists, secretaries na hata personal assistants. Jaribu bahati yako shoga yangu. Sasha alimkabidhi tangazo lililochapwa.
Jasmine alilisoma kwa makini, moyo wake ukijaa matumaini.
โKampuni ya Maxwell Empireโฆโ alisoma kwa sauti ya chini.
โHiyo ni kampuni kubwa sana. Ila watakubali kweli mtu kama mimi?โ
Sasha akamshika mkono.
โHakuna lisilowezekana. Wewe ni mrembo, una akili, na una ujasiri. Hebu jaribu. Hii inaweza kubadilisha maisha yako.
" Asante rafiki yangu kwa kunitia moyo .
Ilipofika Usiku Jasmine aliandaa CV yake vizuri, akakaa akiiombea nafasi hiyo kwa moyo wa dhati.
" MUNGU wangu naomba wakati huu ufike wakati ule uliopanga mimi nifanikiwe. Kesho niende kupata kazi kwenye hii kampuni kubwa.
Siku ya interview ilipofika, Jasmine aliamka mapema, akaivaa sketi ndefu nyeusi na blouse nyeupe iliyompendeza sana. Alionekana kama mwanamke wa ofisini.
Alikaa kwenye foleni kusubiri interview kuanza.
Interview ilianza baada ya dakika chache, na jambo la kushangaza ni kwamba Jasmine hakuulizwa maswali mengi wala magumu. maofisa walivutiwa na kujiamini kwake, na baada ya dakika chache walipeana macho kana kwamba tayari walikuwa wameamua.
Mmoja alimuangalia usoni alafu akasema
โTutawasiliana na wewe ndani ya siku tatu.
" Sawa , asanteni sana , muwe na kazi njema.
Ndani ya siku mbili tu alipigiwa simu kutoka kwenye kampuni ya aliyofanya interview
โHongera Jasmine! Umechaguliwa kujiunga na kampuni yetu kama secretary mpya!โ
Jasmine alipiga kelele za furaha, akamkumbatia Sasha ambaye alikuwa karibu.
โHii ni ndoto yangu imetimia. Hatimaye nimepata kazi kwenye kampuni kubwa!โ
" Hongera sana rafiki yangu .
" Niliomba sana jamani.
" Hata mimi nilikuwa nina matumaini kuwa utapata kazi. Jasmine na Sasha waliendelea kufurahia bila kujua ilikuwa jaribio kubwa la moyo wake.
Kesho yake jasmealiamka mapema sana na kuanza kufanya maandalizi, siku hiyo alivalia nguo yake mpya ambayo alichukua dukani kwa shangazi yake , nywele zake alizitengeneza vizuri na kuwa kwenye muonekana mzuri.
Jasmine alifika kazini akiwa na furaha, akitembelea jengo kubwa la kifahari la Maxwell Empire. Alivutiwa na ujenzi wa kisasa, magari ya kifahari kwenye parking, na wafanyakazi waliovaa suti safi.
Alipofika mapokezi, receptionist aliangalia orodha na kumwambia:
โKaribu, Jasmine. Utakuwa secretary wa boss.โ
Jasmine akatabasamu.
โBoss gani?โ aliuliza.
Receptionist akamjibu na kusema:
โMheshimiwa Leon Maxwell.โ
Jasmine alibaki ameduwaa.
โWhat?!โ alishusha pumzi, moyo wake ukianza kudunda kwa kasi.
โYaaniโฆ yuleโฆ yule mwenye jeuri ndio boss wa hii kampuni?!โ
Hapo macho yake yakajaa mshangao na hasira kwa wakati mmoja.
Mara mlango wa ofisi kubwa ulifunguliwa. Leon Maxwell mwenye suti nyeusi iliyompendeza sana akatokea, akitembea kwa kujiamini. Macho yake makali yakatua moja kwa moja kwa Jasmine.
Tabasamu la dharau likajaa usoni mwake.
โKaribu Jasmine. Sikujua mbinu zako tungefanya kazi haraka sana, sasa umekuja moja kwa moja kwenye himaya yangu. Huu mchezo sasa ndio unaanza rasmi.
Jasmine akavuta pumzi ndefu, akainua kichwa kwa ujasiri.
โHata kama wewe ndio boss, Leon, kumbuka kitu kimoja Mimi siogopi. Na usitegemee nitainama mbele yako....
Kabla hajamaliza kuongea leon alimkatisha.
" Wewe ni secretary wangu sasa , njoo ofisini kwangu haraka.
Leon alitangulia kuelekea ofisini kwake na Jasmine alibaki akiwa kasimama huku akiangalia baadhi ya wafanyakazi usoni.
" Huu ni ujinga Jasmine mimi sijawahi kuogopa kitu naenda. Alijisemea kimnya kimnya kisha akapiga hatua kuelekea ofisini kwa boss Leon ambae yeye alimpa jina la mr arrogant.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi










Maoni