.
Basi nikapokea maelezo kadhaa pale kisha huyo nikatoka nje, ile natoka tu uso kwa uso na Yule bff wangu Yaani Neha.
“Nilikuwa nakusubilia ili tubadilishane Namba niondoke mwaya mume wangu ameshamalizana na matibabu yake“
Basi tukabadilishana Namba pale kisha kila mtu Akashika njia zake, Kwa upande wangu moja kWa moja nikaenda Nyumbani kwetu Yaani kwa wazazi wangu.
“Mbona Kama hauko Sawa ??”
Mama yangu aliniuliza pale
Tu nilipofika Nyumbani.
“Twende chumbani mama tukazungumze kitu “
Nilimwambia mama yangu na pasi na kupoteza muda tukaenda chumbani, Yaani kwenye chumba ambacho nilikuwa nikikaaga mwanzo.
“Kuna shida gani ujue unanipa wasiwasi sana mwanangu”
Mama aliniuliza pale tu tulipoingia chumbani na kufanikiwa kufunga mlango.
Nilijikuta nikianza kulia tu maana hali yangu haikuwa nzuri kabisa, Yaani nilikuwa na maumivu makali mno, Kiukweli Nimekuwa nikipitia kila aina ya maumivu kwenye maisha yangu na sikuwai kumshirikisha mtu yeyote Yule.
“Mama Mimi ni mjamzito na hapa unaponiona nimetoka hospital”
Nilizungumza kwa sauti ya kwikwi.
“Kwahiyo mimba ndio inakuliza au ? Shamsa mwanangu watoto ni baraka sasa unalia nini ? Au mumeo ataki Tena Mtoto mwingine?”
Nilitumia muda wangu wote kumuelezea mama yangu hali halisi ya maisha yangu kWa ujumla.
“Unasemaje wewe ? Shamsa umewezaje kufumbia macho kitu Kama iko ? “
Mama yangu alishtuka sana baada ya mimi kumaliza kumsimulia kila kitu.
“Niliamini Kuwa ni kipindi cha muda tu mama lakini kwa sasa nimeshindwa mama yangu, nimeshindwa mama siwezi tena 😫”
Nilijibu uku nikilia sana.
Mama yangu akanisogelea na kunikumbatia kWa nguvu sana na kWa sauti ya huruma akazungumza.
“Nitazungumza na baba yako Leo akisharudi nina imani atakuwa na jibu la matatizo yenu yote na kila kitu kitakuwa Sawa Binti yangu Sawa “
“Nitashukuru sana mama, Naomba mnisaidiie mno nilipofikia sina sehemu ya kuegemea mama yangu “
Nilizungumza kWa maumivu makali sana.
Baada ya muda nikaaga na kurudi zangu Nyumbani, nilifika na kumkuta mume wangu Akizunguka uku na uku na aliponiona tu akaniuliza.
“Ulienda wapi ??”
Nilimuangalia kisha nikakaa kwenye kochi na kumsalimia.
“Za Saa hizi mume wangu “
“Hizo salamu nimeshapata sana tu umetoka wapi ? Yaani umefikia hatua unatoka tu Nyumbani kaama unavyotaka si ndio ? “
Walahi kuna muda niliona sasa Ananipigia Kelele tu ukizingatia sijisikii vizuri ndio kabisa mambo ni Mvulugano.
“Hamad zungumza kwa sauti ya chini mume wangu Mbona kila muda Una payuka tu jamani eeeh, ata hivyo asubuhi nilikuwa nataka kukuambia Kuwa nataka kutoka lakini ukutakaa ata kunisikiliza, nikakupigia na simu Mara Tatu mfululizo lakini ukupokea simu yangu, nikakutumia na ujumbe WhatsApp umefungua umesoma umekaa kimya maana yake nini sasa “
Hamad akaniangalia kwa hasira kisha akaniuliza..
“Kwahiyo wewe ndio unaumwa si ndio ?”
“Unaniuliza hivyo ukiwa Unamaanisha nini ! Hamad siko vizuri mume wangu AFYA yangu haiko Sawa”
Hamad akacheka sana na kuzungumza.
“Yaani AFYA yako haiko Sawa kwaajili ya iko kimimba chako au ? Kwahiyo mimba ni ugonjwa au ??”
Majibu ya hamad yalionesha wazi Kuwa tayali alishapata majibu kupitia daktari wetu ambaye yeye ni Rafiki yake wa Karibu sana
“Hili suala ndio limenifanya mimi niwai kurudi Nyumbani, Shamsa niliwai kukuambia Kuwa nataka Mtoto wa Tatu kutoka kwako ??”
Uwiiiiih ili swali la hamad Mbona Kama linanichanganya sana Yaani anataka kumaanisha nini, Kiukweli nilibaki njia panda na nikajikuta nikimuangalia tu.
“Usinitumbulie mi macho mie Sawa, sikia huyu Mtoto ni wako tu Mtoto wa Tatu namsubilia kwa Khadija tu na sio kwako, Shamsa hakuna zawadi ya kuzaa, hakuna sifa kwenye kuzaa Sawa”
“Unataka kumaanisha nini labda ? Hamad Mbona unanichanganya mume wangu “
“Huyo Mtoto mtafutie baba yake maana Mimi sina haja na Mtoto Tena, Yaani unashindwaje kujilinda mpaka unabaki Kubeba mimba Kama kichaa “
“Ulitaka nijizuie kWa njia gani hamad, uzazi wa mpango umenikataza, lakini bado unanitumia muda wowote ule ambao utaniitaji haya unataka mimi nijilinde kWa style gani ? Eti utaki Mtoto Kwahiyo Mimi peke yangu nitawezaje ?”
“Usinipigie Kelele mie, umeona madhara ya kutokuwa msomi kila kitu ninachokuambia unafanya au ndio unaleta ule msemo wa masikini na watoto wake ? Mtafutie baba huyo Mtoto wako”
Hamad alimaliza kuzungumza Shombo zake na kuondoka zake na kuniacha nikijililia Mwenyewe tu, kuna muda naona ni Kama Mungu ananionea tu maana haya sio majaribu ya kawaida kwakweli, Yaani hamad kWa sasa kila kitu kwake ni kibaya.
*********
Week nzima ilipita uku nikiwa sina amani na nikiangaika na ujauzito wangu ambao ulikuwa ukinisumbua sana, mimba za watoto wangu waliopita Wala azikuwai kunisumbua lakini huyu wa Tatu ni hatari jamani 🥹 huyu Mtoto hakuna chakula kinakaa mwilini nikila dakika 5 nyingi natapika, uvivu wa hali ya juu na nilijikuta nikianza kukonda na kubwa kuliko sikuwa napenda kuoga 🥹😂.
Ikiwa ni siku ya weekend, siku hiyo Nyumbani tulitembelewa na mama na baba yangu mzazi na siku hii walikuja kwaajili ya mazungumzo kati yangu na hamad baada ya Mimi kupeleka malalamiko Nyumbani kwetu.
“Hivi vizee vyako vimekuja kufata nini Nyumbani kwangu ?”
Hamad aliniuliza, muda huo Mimi na yeye tulikuwa chumbani.
“Hamad hao ni wazazi wetu usisahau “
“Ni wako sio wangu Sawa ? Halafu hapa ni Nyumbani kwangu si kwako, sasa mimi Sina Muda wa mazungumzo Sijui manini nini kawaambie waondoke sitaki kumuona mtu Nyumbani kwangu “
“Hamad, najua Una kiburi sana mume wangu lakini kwa leo please zungumza vizuri na wazazi wangu “
Hamad akaniangalia tu mwisho akatoka nje, kWa haraka na Mimi nikamfata.
“Shekhe Nafikili umekuja siku mbaya Mimi natoka na mke wangu Khadija “
Alizungumza Mume wangu kwa sauti ya dharau sana.
“Aaah kama mnataka Pesa ya mchele mchele hii hapa “
Alizungumza hamad na kutoa noti kadhaa na kutaka kumkabizi baba yangu.
“Hamad mwanangu Wala sikuja kwaajili ya Pesa Nimekuja kwaajili ya mazungumzo kati yako na mwenzako hapa juu ya matatizo yanaayoendelea”
Alizungumza baba yangu kwa sauti ya utulivu na yenye Hekima Ndani yake.
“Kwakuwa Binti yako ndio alikuambia Basi zungumzeni mkimaliza ondokeni “
Alizungumza hamad kisha akarudi chumbani yeye na Hadija wake.
Baba yangu alijikuta akichukia sana akanyanyuka na kwa hasira akazungumza.
“Nikikanyaga kwenye hii Nyumba yako Tena Basi nitafia mlangoni kwako sitafanikiwa kuingia Ndani”
Kisha baba akamshika mkono mama na wakaanza kuondoka.
Kwa haraka nikawakimbilia na kwenda kuwaomba radhi lakini baba yangu alikataa kabisa kunisikiliza.
Walahi nilijikuta nikiwa na hasira sana haraka nikarudi Ndani na moja kwa moja nikaingia chumbani kWa hamad ambapo nilimkuta yeye na Khadija wakiwa wanatokasana tu.
“Hamad ni nini kile umefanya kwa wazazi wangu ?”
“Watu masikini awaruhusiwi kwenye Nyumba yangu “
Aaah hapo hamad alinifanya niwe na hasira ya mbogo na pasi na kufikilia nikamchapa kibao cha shavu, nyieee 🥹🥹 kitendo cha Mimi kumpiga hamad kiliniponza jamani hamad alianza kunipiga pasi na kujali hali yangu, Yaani nilipigwa kuliko kawaida.
ITAENDELEA.
Full 1000
Whatsapp 0742133100.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments