*___________*
*SEHEMU YA 06*
Tulibishana sana na Hemed pale nje kuanzia saa tatu mpaka saa tano nilipoona mida inazidi kusonga na chakula kinapoa ikabidi nikubali tu kuingiza chakula ndani tule wote..
Nilikuwa nasikia njaa mpaka utumbo unatetemeka lakini sikuwa na mpango wa kulaπ°..
Nilipanga chakula mezani nilipomaliza nikamkaribisha...
nilimnawisha mikono kwa adabu nikiwa nimepiga goti hahaaa ndo mama alivonilea jamaniπ
Hemed alikuwa ananawa tu bila kuiangalia mikono yake macho yake yote yalikuwa usoni mwanguπ₯Ίπ₯Ί..
Alimaliza kunawa nami nikanawa nikamuita na mdogo wangu poppy tukala pamojaπ₯°π₯°π₯°chakula cha wengi ndo kinakuwaga kitamu hivo..
Tulienjoy sana chakula tukashushia na juice ya baridi baada ya hapo tukapumzika kidogo tukiwa tunasubilia mgeni aondoke tuendelee kujisomeaπ€
Asije tu akang'ang'ania kulala kwetuπππmaana tutamtimua kama mwiziπ€£π€£π€£...
Hemed alikaa kidogo baada ya chakulaπππni kama vile kuna vitu alikuwa anatamani kuongea ila anashindwa kwa sababu mdogo wangu poppy yupo..
Hata hivo hakukawia alituaga akashukuru sana kwa chakula baada ya hapo nilimtoaπ₯°π₯°π₯° tulipofika nje Hemed aliniuliza kwanini mnakaa wenyewe wazazi wako wapi???
Angejua hilo swali linavoniumizaπππ sikumjibu chochote zaidi ya kurudi ndani na kufunga mlango bila hata kumuaga nilimuacha pale nje akiwa anashangaa haelewi..
Hata hivo Hemed alinitumia msg akaniambia samahani sana Bella nakuahisi sitokuuliza tena hilo swali maana nahisi ni swali linalokuumiza sana..
Siku iliyofuata ilikuwa weekend jpili hatukuenda kufungua ofisi kwa sababu tulikuwa tunafanya usafi maana kesho yake ilikuwa siku ya mdogo wangu kwenda shule na ilikuwa siku yangu ya kurudi chuoni..
Siku hiyo usiku nilimwandalia Hemed chakula kama kawaida baada ya hapo nikamwambia poppy ampelekee nje sikutaka kuonana naye maana angeweza kulazimisha alie tena pale kwetu..
Nilimwambia poppy amwambie mie sipo Hemed baada ya kuambiwa sipo usiku ule alichanganyikiwa like kaenda wapi sasa hivi usiku???
Alianza kunipigia sikushika simu bali niliizima sikuwa mbali nilikuwa ndani chumbani kwangu namchungulia dirishaniπ
Dada huwa ana tabia za kutoka toka usiku??? Hemed alimuuliza poppy akamwambia hapana ni leo tu ndo ametokaππ..
Oh aliitikia kisha akashukuru kwa chakula na kuondoka huku kichwa kikiwa kinawaka motoπ€£π angejua mwenzie niko tu ndani wala asingechanganyikiwa vile..
Siku iliyofuata asubuhi wakati namsaidia poppy kufanya maandalizi ya shule tulisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yetuπ³π
Lazima ni Hemed huyoπnilijisemea kabla ya kuchungulia... hata hivo tulisikia Hemed akiwa anabisha hodi nilipochungulia nilimuona akiwa amesimama mlangoni na vile vyombo vya chakula..
Nilikwenda kumfungulia na nilikuwa nimependeza hatariπ€ππ nilikuwa nimevaa mavazi mazuri sana maana nilikuwa namsindikiza poppy shuleni..
Hemed alizoea kuniona kwenye vijoraπππsiku hiyo kwa mara ya kwanza aliniona kwenye kigauni fulani hivi kifupi cha kubana na viatu virefu..
Nilikuwa nimependeza mnooo jamaniππjamaa alipigwa butwaa baada ya kuniona akaniuliza Bella ndo unarudi nyumbani sasa hiviπ₯Ίπ₯Ί..
Nikashangaa mbona ananishautiaπ³ππ wala sikumjibu nilichukua vyombo alivokuwa navyo nikarudi ndani wala hatukusalimiana
Ye si ndo alianza na shouting bila hata salamπ namimi sikuona kama kuna umuhimu wa kumsalimia nilichukua zangu vyombo nikamuacha pale mlangoni akiwa amechukiaπ
Poppy alimalizia kujiandaa tukatoka na Hemed hatukumkuta pale nje..
Tulikwenda tukapanda daladala mpaka shuleni kwa mdogo wangu..mimi ndo kama mzazi wake na kwa siku kama hizo wanazokuwa wamefungua shuleni ni lazima kumpeleka...
Ada niliyokuwa nayo ni kidogo sana yani ni kama robo tatu ya ada kamiliπ°kibaya zaidi siku hiyo tuliambiwa wanafunzi wote wa kidato cha nne
Wanatakiwa waanze kuishi shuleni na ni lazima siyo ombiπ°π°ilitakiwa pesa ya kulipia hostel na chakula..
Nilitamani kulia siku hiyo shuleni lakini nilijikaza mdogo wangu asijue chochote ninachokipitia..
Dada umesikia mwalimu mkuu alivosema kuhusu kukaa shuleni na ni week ijayo natakiwa nishone na sale za hostel pia..
Usijali mdogo wangu ngoja niende nikakufanyie mpango nilimpa matumaini tu lakini kiukweli sikuwa najua wapi naenda kupata pesa maana mimi mwenyewe huko chuoni kuna mitihani natakiwa kufanya ila sina ada..
Wakati naondoka pale shuleni nilikuwa napangusa machozi nina majukumu ambayo sijui nitayatatuajeππ wakati nalia ghafla kuna mtu akanigusa bega na kunipatia tissue nifute machoziπ³π³..
Itaendeleaaaaaa
*SEHEMU YA 07*
Mmhhh baada ya kuguswa bega niligeuka haraka haraka kumwangalia ni nani alonishika begaπ€π€
Alikuwa mbaba mmoja hivi alinipatia tissue akaniambia futa machoziπ³π³π³huyu ni nani???ndo swali nilikuwa najiuliza
Hata hivo alijitambulisha akaniambia yeye anaitwa Mr Martin...
Vipi tunafahamiana??. Nilimhoji...akajifanya ni kama hajalisikia vizuri lile swali na muda huo simu yake ilikuwa inaita alipokea simu bila kunijibu swali langu..
Mr Martin aliongea na simu baada ya hapo akaniuliza sorry unaelekea wapi??.
Nikamwambia mtaa ninaoenda akaniomba nipande kwenye gari anishushie huko maana ndo anaenda kupita huko..
Nilipanda kwenye gari maana hata hiyo pesa ya kwenda kupanda daladala sikuwa nayoπ°π°
Hiyo gari yake sasaπ³π³π³ ni V8ππ kwenye gari nilijua nitaanza kuongeleshwa like kutongozwa au kuombwa namba lakini wala..
Mr Martin alinifikisha sehemu nilipotaka kushukia nikamwambia akanishusha nilimwambia thank youuu
Akajibu okay take care akafunga mlango wa gari na kuondokaπ³π³π³yani hata kuniomba hamna jamaniπ°π°π°..
Kwa mara ya kwanza nikajihisi kama sijakamilika ujue mara nyingi nimekuwa natongozwa na wanaume mbalimbali wananishobokea nawakataa..
Kilichoniuma zaidi ni vile Mr Martin aliniona kabisa nalia akanipa tissue nifute machozi lakini hakuniuliza nilikuwa nalia niniπ°π₯Ί
Na kwanini hajanitongoza nimkataeπ°π°π°au nimeshaanza kuwa mbaya??.
Niliumia mno ujue mwanamke ukitongozwa kuna namna unakuwa unajiona bado nalipa mimi kumbe ni mrembo...
usiombe ukakutana na mwanaume akaonesha kukujali alafu mwisho wa siku asikuombe namba wala kukutongoza inaumaa..
Nilitembea mpaka nyumbani kama mtu alomwagiwa maji ya baridi mwiliniππ
Baada ya kufika nyumbani nilienda moja kwa moja chumbani kwangu kulala..wakati nimelala simu yangu ilianza kuita..
Alikuwa anapiga Hemed nilipokea simu nimsikilize...Hello Hemed.. akaitikia yes Bella mbona sauti yako iko hivo??.
Sauti yangu ilikuwa ya majonzi majonzi sana nilimwambia niko sawa usijali..
Hemed aliniomba tutoke kuna kitu alihitaji kukizungumza na mimi...nilimwambia siwezi kutoka kwa sababu mchana nina kazi ya kumwandalia mwanafunzi chakula..
Hemed aliniambia yeye atanunua chakula cha poppy huo mchana atampa mtu amletee nyumbani..
Aliniomba sana mpaka nikakubali...aliomba nijiandae ye atakuja kunichukua nyumbani..nikamwambia sawaaa..
Niliamka nikajiweka sawa baada ya muda Hemed alikuja kunichukua...sikujua tunaenda wapi na isitoshe bado ilikuwa ni asubuhi sana..
Hemed aliendesha gari umbali mrefu kidogo mpaka kwenye hotel fulani nzuri sana..
Aliweka gari parking tukatelemka alinishika mkono nikashuka kwenye gari baada ya hapo akaniambia umependeza sana Bella..
Wewe ni mzuri sanaβ€οΈβ€οΈ nilimjibu asante alinishika mkono tukawa tunatembea kuingia ndani ya ile hotel..
Hemed ni handsome sana kiasi kwamba nilikuwa naogopa kuruhusu moyo wangu umpende maana nilikuwa nahofia kuumia..
nilijua kabisa kwa yule kaka sitakuwa peke yangu..ni mzuri mno kiasi kwamba ukiwa naye unakuwa hata hujiaminiπππ
Tulikwenda tukaketi kwenye kisehemu kizuri mhudumu akaja kutusikiliza ... kwa vile bado ilikuwa ni asubuhi tuliagiza breakfast tukaletewa..
Tukaanza kulaπ₯°π₯°π₯°Hemed alikuwa anakula lakini muda wote macho yake yalikuwa yananiangalia tu mimiπ
Baada ya kunywa chai Hemed aliniomba tuongeeeππnilikubali kumsikiliza..
Hemed alinitongoza aliniomba kama itawezekana mimi na yeye tufungue ukurasa wetu mpya tuzame katika ulimwengu wetu wa mapenziππ
Alidai tangu siku ile ya kwanza aliponiona moyo wake ulivutiwa sana na mimiππ
Mtoto wa watu alikuwa very serious alirudia mara mbili mbili kuniambia Bella I love you please naomba unikubalie..
Je Bella atakubali??? Itaendeleaaaaa
Full 2000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments