Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya โ€“ Gonga94 Semajambo

MIRANDA (Binti Yangu) 1 - - - - - 5
Gonga94 ยท Stories

MIRANDA (Binti Yangu) 1 - - - - - 5

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.


SEHEMU YA 1
ANZA NAYO SASA......

Kuna ule msemo kuwa mpende yule anaekupenda na mthamini yule anaekuthamini,yes naweza kusema kuwa mimi nilibahatika kupendwa na kuthaminiwa bwana ๐Ÿ˜Š

Yaani binti yenu kwenye kupendwa sijui niseme nilizaliwa na ka nyota flani hivi ka kupendwa๐Ÿ˜ , yani nilipozaliwa mama aliwahi kuniambia nilipokuwa mdogo nilikuwa napendwa jamani๐Ÿค—

Haipiti siku watoto kutoka nyumba za jirani wanajazana nyumbani ili kunibeba ๐Ÿ˜… kuna wale msioamini ila kuna wachache sana wataamini maana wao walikuwa kama mimi

Okay loves, tuachane na bla bla za hapa na pale kwanza twende na utambulisho rasmi sasa, unaweza kuniita Mira ikiwa ni kifupi cha jina langu, jina langu ni Miranda yes Miranda never and ever nalipenda hili jina ๐Ÿฅฐ

Katika familia yetu mie ndio mkubwa wakifuatia wadogo zangu saba ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… mpaka naona aibu hata kuwatambulisha hawa wadogo zangu maana sijui wazazi walipania kuzaa aisee ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃukifika nyumbani unakuta vitoto vimefuatana balaa๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

Okay kwa sasa mimi naishi huku Oman ๐Ÿ‡ด๐Ÿ‡ฒ, na naishi kama mfanyakazi wa ndani katika familia moja hivi ya kitajiri sana, yani hii familia sijui hata niielezeeje maana wanajua kujali na kuthamin haki ya mtu

Wakati nilipokuwa tanzania niliwahi kusikia kuwa waarabu ni watu wa baya sijui ukienda huko wanaenda kukufanyisha kazi za ngono mara ufanye mapenzi na mbwa ๐Ÿ˜‚ my zangu naweza kusema sio wote wapo hivi

Msije mkasema nawatetea maana kwanza lazima niwatetee hawa ninaoishi nao maana hawa watu wananipenda zaidi ya hata hilo neno ๐Ÿค— hivi unajua maana ya kupendwa na familia nzima wewe ๐Ÿ˜ƒ yani napendwa mpaka kuna muda naogopa sasa ๐Ÿซฃ maana huku kwenye kupendwa aweee ๐Ÿ”ฅ

Sababu kuu ya mimi kupendwa ni kwa uchapakazi wangu lakini pia mimi niko na heshima kama zote, hivi mnaelewa maana ya kuwa na heshima zote iko hivi mimi naheshimu watu wa rika zote awe mkubwa au mdogo sijawahi kumzarau mtu kabisa

Basi nazani mmejua ka story kangu kafupi twende na story yetu,

Ni majira ya mchana jua lilikuwa kali sana, siku hiyo nilikuwa zangu jikoni nikiwa nimejiachia na sijali lolote, binti nilikuwa nimevaa nguo za stara yaani ikitokea umeona upaja wangu basi niite mbwa nimekaa pale ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mimi kwenye kuvaa nguo za stara huko uarabuni naweza kusema niko kwenye orodha ya watu wanaojistiri aisee, mimi ni mkristo pure kabisa lakini mavazi ninayovaa ni ya kiislam yani mpaka ushungi nafunga nabaki nimeonyesha macho tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

Mie bwana nimetokea kupenda sana dini ya kiislam kutokana na watu wengi wa huku kujistri sana, lakini uje hapa kwa boss wangu eeeh hawa watu wanajiachia aisee yani nusu ya miili yao iko wazi na hawajali lolote kama yupo baba or mama yao mabinti wao ni kujiachia tuu na vinguo vifupi imefikia muda mpaka mapaja yao yamenikinai sasa hata kuyaangalia ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Basi bwana niliendelea kupika na muda huo hapo nyumbani nilikuwa nimebaki mimi na mtoto mdogo wa madam ambaye bado mdogo sana ana miezi sita.

Mtoto huyu anitwa Nasrat na hili jina nilimpa mimi mwenyewe, najua mnajiuliza kwanini waruhusu mimi nimpe jina mtoto wao na ikiwa wao wapo, shoga enu kama nilivyowaambia mie napendwa na ninaaminiwa sana kwahiyo hakuna shida kitendo cha kuambiwa naletewa mtoto wa kumlea awee chapu nikampa jina akiwa bado tumboni ๐Ÿ˜‚

Nasrat nimemfanya kama mtoto wangu, yani imefikia hatua Nasrat ananiita mimi mama, kuna ka furaha huwa nakapata na upande wa mama yake yeye hajali lolote kuhusu mtoto yani hii familia naweza kusema kuwa huyu mtoto ni kama wamenizalia awe wangu

Nikiwa bize napika nikasikia sauti ya mtoto wangu analia, chapu nikaacha kupika na kwenda kumuangalia mwanangu, nilimkuta akiwa analia sana ๐Ÿฅน yani mtoto alikuwa analia na haikuwa kawaida yake

Nikiwa kama mlezi nilihisi kuchanganyikiwa haraka nilikimbia mpaka seblen na kumpigia simu doctor na kumuomba aje nyumbani haraka doctor alinihaidi atakuwa hapo baada ya nusu saa.

Nilikuwa nazunguka kama chizi nyie huyu mtoto nampenda kama nimemzaa mimi, nilitafuta namba ya mdam na kumpigia nikimuomba aje nyumbani mtoto wake anaumwa.

"Madam pleas Nasrar analia sana na sielewi shida nini..."

Nilisema huku machozi yakinitoka kabisa.

"Ila Mira, hivi umesahau kuwa huyo mtoto nimekuzalia wewe namaanisha kuwa huyo mtoto ni wako mie watoto watatu wamenitosha naweza kusema kuwa Nasrat alizaliwa kwa bahati mbaya maana sikuwa kwenye mpango wa kuongeza mtoto mwingine kwa kuwa sikutaka kuonekana mbaya kwa kukatili kiumbe kisichokuwa na hatia niliamua kumzaa na kukukabidhi wewe kwahiyo huyo ni mtoto wako na sio wangu

Kama ni shida kama zilivyo shida niko tayari kukusaidia kwa lolote lile lakini ni kwamba Nasrat sio mtoto wangu.."

"Madam huu sio muda wa kuongelea hayo mambo, tafadhali kama mzazi njoo umuone binti yako.."

"Mira, hivi wewe ni mtu gani usienielewa umeanza lini kunipandishia sauti nimesema hivi huyo ni mtoto wako kwahiyo pambana kuhakikisha anakuwa sawa na kuhusu gharama usisite kunijulisha.."

Alisema madam na kukata simu, nyie huyu mama hata simuelewi kabisa mara ya kwanza wakati wananiambia haya yeye na mume wake nilizani wananitania bwana lakini leo ndio nimejua wako serious aisee nilichoka.

Nikiwa nazunguka hapo sebleni huku nimembeba Nasrat doctor aliweza kufika pale, basi kwa haraka alianza kumfanyia matibabu, hali ya mtoto haikuwa nzuri hivyo ilimbidi kupelekwa hospitali kubwa ili kwenda kuangaliwa zaidi

Mkumbuke muda wote huo sikuweza kuingia jikoni hata kuzima jiko nilisahau kutokana na kuchanganyikiwa nilishindwa kukumbuka kama sikuzima jiko.

Basi tulibeba mtoto na kuelekea hospital, njia nzima nilikuwa nikimuomba mungu amuepushe Nasrat maana bado mdogo sana tena anamuhitaji mama yake na kama mlikuwa hamjui Nasrat toka azaliwe hajawahi kunyonya maziwa ya mama yake ๐Ÿฅน jambo hili linaniuma sana zaidi amekuwa akitumia maziwa ya ng'ombe.

Safari yetu ilienda kuishia hospital kubwa sana, tena ilikuwa hospital ya private haraka mtoto walianza kumfanyia matibabu, wakati huo nilishapiga karibia simu zote za ndugu zake lakini hata hawakujali lolote kuhusu mtoto zaidi ya Naina huyu ni dada mkubwa ndio wa kwanza kuzaliwa

Anafuata mvulana hata sijui anaishi wapi ila nasikiaga tu habari zake kuwa kuna mtoto wao wa pili ambaye anafahamika kama Anfrey sijawahi kumuona na sijui yupo wapi mie sijui

Kuna mwingine anaemfuata Anfrey huyu ni mdada anaitwa Swatii, binti huyu ni mcharuko yani binti hatulii na mwanaume mmoja kila mkaka anapita nae aisee huyu binti ni kiwembe

Na mtoto wao wa mwisho ndio Nasrat kama Nasrat binti yangu mzuri nyie ๐Ÿฅฐ yani ukikaaangalia hutaacha kukatazama lakini ndio hivyo binti hana bahati ya kupendwa na wazazi wake......

ITAENDELEA......
SEHEMU YA 2
SONGA NAYO.......

Basi baada ya muda Naina akawa amewasili pale, na kuniuliza habari za mtoto mie basi hata kuongea siwezi nilikuwa nalia tu ikabidi Naina achukue jukumu la kunituliza kwanza..

"Mira, najua wewe ndio umekuwa kama mzazi lazima hili likuume lakini nikutoe hofu hali ya Nasrat itakuwa nzuri kikubwa tumuombe Allah..."

"Lakini..."

"Kaa kimya Mira, hutakiwi kunieleza chochote vyote najua na sio kwamba sifahamu najua kabisa na usione mie nipo hapa kwa kupenda no nafanya hivi kwa sababu wewe umekuwa mtu mhimu katika familia yetu ndio maana nimeamua kuja ili kukupa moyo

Sihitaji kusikia ukinieleza chochote kuhusu mama or baba naomba focus na mtoto kwanza.."

Hata sikutaka kubishana nae nikakaa kimya huku nikijiinamia tuu nalia mwenyewe kwenye moyo wangu, basi matibabu yaliendelea hatiame kila kitu kilikamlika na doctor alitoka ili kuja kutupa majibu zaidi.

"Nahitaji kuonana na mama wa huyu mtoto..."

Alisema doctor, basi mie hata sielewi zaidi nikabaki namwangalia Naina.

"Unaniangalia nini, wewe nenda kaangalie afya ya mwanao..."

Nikawa hata sijamuelewa hapo.

"Unaongea kuhusu nini..??"

Nilimuuliza.

"Eeh Mira hivi siku hizi umekuaje wewe, kwani wewe sio mama mzazi wa Nasrat..??"

Eeh hapo kidogo kwanza nikamuangalia doctor, kisha nikamfuata maana kukaa nikibishana na watu ambao haiwaijali damu yao ni sawa na kuumiza Figo.

"Mwanao uliwahi kumnyonyesha mara ngapi toka umzae..??"

Baada ya kufika tuu kwenye chumba cha doctor, doctor alinitupia swali ambalo kwangu lilikuwa gumu kulijibu nikabaki nimetumbua macho nikimuangalia doctor

"Nafikiri haupo sawa kwa saivi nikuache upumzike kwanza.."

Doctor alisema huku akinyanyuka, nilimuwahi na kumuomba akae tuzungumze.

"Dr, kwanza nitangulize samahani, huyu mtoto mimi nilimuokota na kumlea kama mtoto wangu.."

Niliamua kudanganya sasa maana ningethubutu kuongea kuhusu madam basi ni kama naiweka familia kwenye matatizo makubwa.

"Oooho ndio maana, maziwa unayompa mtoto sio mazuri kwa afya yake hivyo itabidi kwanza nikupe dawa ya kuua vijidudu vya magonjwa kisha nitakuagizia mlo kamili wa watoto ambao wana miezi kuanzia miwili na kuendelea hii nakupa offer maana una moyo wa kipekee sana.."

"Asante, vipi hali ya mtoto kwa saivi..??"

"Anaendelea vizuri, ila kwa Leo hamtaweza kutoka hapa labda kesho.."

Alisema Dr huku akinyanyuka na kutoka ndani ya chumba hicho akaniacha mwenyewe kichwa kikiwa kizito kwa mawazo basi doctor aliweza kurudia akiwa amebeba dawa pamoja na chakula cha mtoto.

Alinipa maelekezo pale baada ya hapo aliniruhusu kwenda kumuona mtoto, sikupoteza muda yani ile naruhusiwa tu ni shwaa nikawa nimefika wodi aliyolazwa Nasrat.

Baada ya kufika mule wodini nilikakuta kakiwa macho, kanaangalia tuu juu ya dari yani kamepoa hata uso wa nuru hakana kabisa kalionekana hakana hata furaha maskini..๐Ÿฅน

"Nasrat.."

Nilkaita kakaniangalia, baada ya kuniona kakatabasamu nyie nilifurahi nikakashika vidole vyake kakawa kanacheka basi namie nacheka furaha yangu ni kumuona Nasrat akiwa na tabasamu

Nikiwa nacheka hapo na mtoto aliingia Naina, alipofika alikaa pembeni yangu na kuanza kuniangalia namna nilivyokuwa namcare mtoto.

"Wooow nakuona mwenyewe..."

Alisema Naina..

"Yaah kwanza hapa afadhali maana nilikuwa nawaza sio poa..."

Nilizungumza

"Inaonekana unampenda sana mtoto wako.."

"Yaap lazima nimpende kwa sababu ni mtoto wangu.."

Nilimjibu huku nikionekana kuchukizwa sana naaswali yake yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Hakusema neno zaidi alibaki akiniangalia tu na simu yake iliita akanyanyuka

"Naenda kupokea simu.."

"Sawa..."

Akatoka, mie nikabaki nasonya tuu watu sijui wana roho gani hawa yani ndio nimeamini kuwa kuna watu huwa wanatupa watoto wao wa kuwazaa maana siku zote zile nilikuwa nakataa kabisa ila kwa hili aaah niseme tuu nimeamini.

Basi baada ya muda Naina alirudi mule wodini na kunikuta nampa mtoto chakula

"Mira, najua unasumbuka kwa ajiri ya mtoto lakini kwanini usingezima kwanza jiko ndio hayo mengine yakafuata..??"

"Unaongea kuhusu nini..??"

Nilimuuliza maana hata sikuwa naelwa kabisa eti

"Kwanini hukuzima jiko wakati unaondoka.."

Hapo kidogo ndio nikakumbuka kuwa nilikuwa napika na jiko sikuweza kuzima, kwa hofu nilinyanyuka na kumuangalia Naina nawaza kama nyumba itakuwa imeungua yote nitafanyaje mimi.

"Eeeh Naina nilipitiwa tuu bahati mbaya, kwani nyumba imeungua au..??"

Hapo nauliza huku jasho likiwa linanitoka mwili mzima.

"Hapana.."

"Ila, nambie basi mbona unaniambia maneno nusu nusu sasa nitaelewa nini..."

"Hakuna chochote kilichotokea, maana mlinzi alienda kuzima jiko ila nikwambie kitu shoga angu kuwa makini na mali za watu..."

Naina aliongea kisha akaondoka, nikabaki nawaza kama nyumba ingeungua sijui ningefanyaje, sina hela labda ya kusema nirudishe mali za watu zilizoteketea ndio nikakumbuka na maneno ya Naina ndio kabisa nikaona hapa niwe makini naweza kutolewa Figo......

ITAENDELEA.........
SEHEMU YA 3
SONGA NAYO.......

Basi siku hiyo nilishinda hospital nikimuangalia mtoto, ilipofika jioni ilinibidi nirudi nyumbani kufuata mahitaji ya mtoto kama pampazi na vitu vingine.

Basi nilichukua usafiri mpaka nyumbani, baada ya kufika nyumbani nilikuta familia nzima ikiwa inapata chakula cha jioni yani inafutru

Nilifika na kusalimia pale, kisha nikamsogelea madam.

"Madam nilikuwa nao..."

"Kama kuhusu Nasra naomba usiniambie chochote.."

Eeh nikabaki namuangalia huyu mama huku nikimpima tuu kwenye mizani ya jicho, yani nilishindwa kumuelewa kabisa et

Imagine umebeba mimba miezi tisa na ukaumwa uchungu sijui masaa mangapi na tena ukajifungua kwa op ukauguza kidonda kwa miezi sita leo hii mtoto unamkana kabisa sio wako kweli hii inawezekana au mie niko ndotoni.

Niliona kama naota aisee nikajizaba kofi la shavu kwanza labda nilikuwa naota lakini ni uhalisia kabisa kwanza nilivyojipiga tuu madam akacheka kisha akantazama kwa umakini mkubwa

"It's the truth, sijawahi kupendezwa na Nasrat kwa sababu zangu binafsi, kama nilivyokwambia awali nilitaka kumtupa Laki..."

"Inatosha sasa inatosha..."

Nilizungumza huku nikilia kabisa, madam alinyanyuka kwenye kiti na kunifuata mapaka nilipokuwa alipofika akanikumbatia ๐Ÿฅน huku akinituliza yani kwangu niliona kama amenizarau kabisa huyu mama

Kwa hasira nilisukuma huko, nilitamani kumzaba kibao ila nikatulia

"Wewe ni mama wa aina gani ambaye hujali lolote kuhusu mtoto, hujui binti yako kule ana hali gani mtoto anaumwa kwa sababu yako mtoto anapitia kipindi kigumu ile hali mama upo hapa hivi nikuulize wakati unapan..."

"Binti taratibu sawa, umesahau kuwa mimi ni boss wako..??:

"Uwe boss au nani yangu lakini lazima nikwambie ukweli, nasema hivi kuanzia leo sitamujali tena Nasrat bora nimuache tuu apumzike kwa amani.."

Nyie nilikuwa nimechafukwa balaa huyu mama alikuwa ananiona mie kama matako yake, muda wote ule tunajibizana baba wa familia yeye alikuwa kimya akinywa supu huku anachezea simu yake.

"Mira..."

Madam aliniita baada ya kuona nimekasirika sana ukweli nilikuwa nimechukia na macho yalikuwa mekundu kama nilivuta bangi aisee ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

Nilimuangalia bila kumuitikia.

"Mira, kuna machaguo mawili.."

Aliniambia madam, mie nilikuwa kimya huku mdomoni nikitafuna karafuu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ eeh nilikuwa natafuna ili kuepuka kupiga mtu maana mie hasira zangu nazijua mwenyewe

"Chagua kuondoka hapa na unilipe milioni 50 kwa sababu umekiuka mkataba tulioweka baina yangu mimi na wewe either ubakie hapa na uendelee kumlea Nasrat sio kumlea tuu bali kumfanya kama mtoto wako na hutanilipa chochote mpaka Nasrat afikishe miaka 15 ndio utaondoka hapa na hutaondoka naye yaani utaondoka wewe kama wewe na Nasrat ndio utakuwa mwisho wake wa kuishi..."

Nilikuwa natafuna karafuu lakini mpaka niliitema maana nilisikia utamu na uchungu kwa pamoja, nilimuangalia madamu kisha nikamuuliza.

"Yani itakuwa mwisho wake kivipi.."

"Kama ulikuwa hujui, ngoja nikuambie kitu, Mira umeishi kwenye hii nyumba zaidi ya miaka mitatu si ndio..??"

Sikumjibu

"Usione huu utajiri unapatikana kwa nguvu zetu, hapana Mira bali tumejiunga na chama kikubwa cha freemason na tunatakiwa kutoa kafara ya mtoto wetu wa mwisho na hatutakiwi kumpenda ndio maana unaona mie mzazi sijali lolote kuhusu Nasrat lakini ukweli naumia sana tena sana kuona binti yangu anateseka vil..."

"Komea hapo hapo.."

Nilimwambia na sikutaka kusubiri neno jingine kutoka kwake nilishika njia na kuingia chumbani, yani kichwa kilikuwa kizito hii siku nilihisi chungu, nilikuwa nazunguka tu mle ndani na nisijue kipi nichague

Siku hiyo ilikuwa ndefu, kila nikikumbuka kuna mtoto kule hospital na ananitegemea mimi moyo ulikuwa unauma, basi nilichukua pampazi na nguo nyingine za kubadili nilitoka moja kwa moja

Nilipofika sebleni niliwakuta wakiwa wamekaa wanaangalia TV mie nikawapita kama siwaoni vile, nilitoka mpaka nje nilisimamisha usafiri nikapannda na safari ya hospital ikaanza.

Njia nzima nilikuwa nawaza kiasi kwamba nilipitilizwa kituo, basi nilishuka na kuchukua gari nyingine tena safari hii nilichukua ile ya kipeke yangu

Namshukuru mungu niliweza kufika salama na niliweza kumkuta Nasrat wangu anendelea vizuri, siku hiyo ilipita kwa mbinde sana na sikubahatika kurudi nyumbani kwa sababu ya mgonjwa.

Kesho yake majira ya mchana tuliweza kuruhusiwa huku doctor akinihimiza sana kumuangalia mtoto, basi nilichukua usafiri mpaka nyumbani nilikuta nyumba ikiwa kimya nilijua watu walikuwa hawapo

Nilimchukua Nasrat na kwenda kumlaza chumbani kwangu, baada ya hapo niliingia jikoni na kuanza kuandaa chakula cha mtoto maana nilitaka ale kwanza yeye harafu mambo mengine yaendelee

Baada ya kumaliza kuandaa nilimlisha kisha nikamuogesha, nilimbembeleza hadi akalala na mimi ndio nikapika chakula cha wote kisha nikala na kupumzika maana usiku mzima sikulala nilikuwa namuangalia mtoto.

Majira ya jioni nilianza kusikia milio ya gari ikimaanisha wana familia walianza kurejea nyumbani kwa kuwa sikuwa sawa sikujishughulisha kutoka.......

ITAENDELEA........
SEHEMU YA 4
SONGA NAYO.....

Nikaendelea kulala bila kujisumbua kwenda kusalimia huko sebleni

Nikiwa nimelala nilisikia nikigongewa mlango, basi kichovu nilinyanyuka na kwenda kufungua mlango nikakutana na madam, nilitamani kufunga mlango kila nikiiona hii sura moyo wangu unahisi hasira

"Umeshindaje..??"

Aliniuliza

"Salama..."

Nilimjibu kwa mkato siku hii sikumchangamkia kama zilivyo siku nyingine sijui pole na kazi aka siku hiyo nilikuwa mkavu

"Aaah nimekuja kukuita hapa kuna kitu nataka kukuonyesha.."

"Kitu gani..??"

"Mira bwana, nimekuletea wadada wa kazi wawili watakuwa wanakusaidia kwenye kufanya usafi na kuandaa chakula ila wewe jukumu lako ni kumlea mtoto basi.."

"Nashukru.."

Nilisema huku nikifunga mlango, akanizuia tena

"Arafu nimesahau, leo ndio unapokea mshahara wako so nikitoka hapa nitaenda kukuwekea kwenye account yako.."

"Asante.."

Hakuongea chochote aliondoka na mimi nikafunga mlango ila sikufunga mlango bali niliuegesha tuu kisha nikaanza kumchungulia madam namna alivyokuwa anaondoka.

"Cheki yale matako, lanamke lijinga tuu hata shape halina kazi kujaza minyama tuu.."

Nilijiongelesha, ๐Ÿ˜‚ ila mimi mara ya kwanza wakati nafika kwenye hii nyumba nilikuwa namsifia madamu kuwa yeye ni mzuri sana ila leo ndio nimeanza kumchunguza sasa na kumdadisi mwili wake.

Basi nilihakikisha nafunga mlango vizuri ili mtu yoyote asiingie chumbani maana nilikuwa na mashaka sana kuliko kawaida tena nilifunga na funguo kabisa kisha funguo nikaziweka kwenye nyoyo zangu๐Ÿ˜‚, baadae nikatoka ili kwenda kuona hao wadada wapya wa kazi.

Kweli bana kama alivyoniambia madam niliwakuta wakiwa wamekaa kishamba kishamba yani macho meupe wanashangaa tu.

"Shikamooo..."

Walinisalimia ndio nikajua kuwa ni watanzania wenzangu bwana maana waliongea kiswahili kabisa tena kilichonyooka, basi mimi ili nisionekane na mie nimekaa kizembe ikabidi niongee kiinglishi maana watu wote hapa tunaongea kingreza tu

"Habari zenu...??"

Niliwasalimia kingreza, wakabaki wananiangalia tuu wasinielewe, najua mioyoni walikuwa wanajiuliza huyu nae kumbe ni mwarabu bana ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†

Sikutaka kuichosha akili yangu ukizingatia nilikuwa namawazo yangu nikawaambia wanifuate basi bila ubishi walinifuata niliwapeleka mpaka jikoni.

Nilikuwa na kazi ya kuwaeleza namna ya kutumia jiko na ratiba za humu ndani, hivyo ilinilazimu kuongea kiswahili kama nilivyowaambia mie naheshimu watu wa lika zote basi taratibu nialianza kuwafundisha ili waweze kunielewa kirahisi.

"Ratiba za humu ndani mnatakiwa kupika chakula mara mbili kwa siku..."

Niliongea kisha nikawatazama, kwa mbali nilisikia sauti za nyayo ikionyesha mtu alikuwa akija jikoni kweli Swatii aliweza kufika mle jikoni..

"Da Mira..."

Swatii aliniita nawaambia huyu dogo ni kiwembe mjini ila ako na adabu kama zote yani ninachompendea Swatii ananijali sana na haipiti siku bila kuniletea zawadi.

Hata jana nilipokosana na mama yake yeye hakuwepo alikuwa kwa mabwana zake na alilala huko leo ndio amerudi sasa.

"Swatii mambo..??"

"Poa tu, mh naona vitu vipya..."

"Yaap.."

"Da Mira mbona jana ulinipigia sana simu yani mimi simu yangu niliweka silent hivyo sikusikia kabisa maana nilikuwa kwenye party, party ilipoisha ndio kuangalia simu nikakuta missed calls zako vipi ulikuwa na shida..??"

"Aaah nilikumiss tu si unajua tena wizo.."

"Wewe tena ila kuna zawadi yako nimekuletea..."

"Zawadi gani...??"

"Sikwambii mpaka umalize mambo yako, utakuja chumbani uchukue.."

"Sawa love ndio maana nakupenda mwaya.."

Nilimwambia.....

ITAENDELEA........
SEHEMU YA 5
SONGA NAYO.....

Basi tuliongea pale na swatii akaondoka, nikawageukia wale mabinti na kuendelea kuwafundisha pale baada ya kuelewa kila kitu niliondoka na kuelekea chumbani kwangu kumuangalia kipenzi cha roho yangu kama ameamka.

Nilimkuta akiwa bado kalala, basi niliingia bafuni nikaweka mwili safi baada ya kumaliza kila kitu nikatoka sikusahau kufunga mlango nikaelekea chumbani kwa Swatii

Nilimkuta akiwa amekaa kitandani anachezea laptop kwa kuwa mimi na yeye ni ma bff nilifika na kujitupia kitandani.

"Nipe zawadi yangu.."

Nilimwambia bila kujua anaongea na mtu kwenye laptop baada ya kuona sijibiwi ikabidi nisogee nione nini anafanya bwana bwana nilibaki nimekodoa macho yangu kiasi kwamba nililitoa mpaka nyuzi 100 za jicho

Nilikuwa nashangaa baada ya kuona likaka lizuri likiwa linaongea na swatii kwa mawazo yangu nikajua ni mpenzi wake hivyo nikamuuliza..

"Swatii, bwana ako mbona mzuri hivi...??"

"Hahahaha we toka lini ukaanza kusifia mwanaume...??"

"Toka zamani mbon, arafu naona hata hunizuii mimi kumtazama.."

"Weee naomba uniache Swatii mimi, yani mimi nina wivu balaa siwezi ruhusu rafiki yangu au hata dada yangu kuwa karibu na bwana yangu maana nitaumia sio poa..."

"Mbona mimi hujanizuia kumtazama au mimi sio mwanamke..??"

"Kwa sababu huyu sio bwana angu.."

"Ni nani...??"

Niliuliza huku macho yakiwa yamenitoka..

"Ni kaka angu..."

Kusikia kaka niliruka na kwenda kujibamiza kwenye furniture iliyokuwa mle chumbani bahati mbaya niliangukia mkono hivyo ukateguka, maumivu niliyoyapata yalisababisha Swatii afunike laptop na kuja kuniangalia mimi..

"Umeumia..??"

Swatii alinuliza baada ya kunifikia.

"Sio sana ila mkono umeteguka.."

"Dah leo ndio nimeamini kuwa hujawahi kuwa na mchumba, maana siku zote unaniambia huna mpenzi nikajua unanitania bana.."

"Tuachane na hayo bwan, hivi hajaniona..??"

"Nani..??"

Swatii dishi lake limeyumba, yani huyu binti ni mwepesi kusahau.

"Si kaka yako..."

"Sizani kama amekuona maana alikuwa busy na kazi, wakati mimi naongea nae macho yake yalikuwa pembeni.."

Hapo kidogo presha ikanishuka.

"Sawa.."

"Basi njoo nikukande.."

Swatii aliniambia huku akinisogeza kitandani na mara mlango ulifunguliwa akaingia madam

"Mira umeumia..??"

Madam aliniuliza kwa kujali yani nilitamani amjali binti yake na sio mimi..

"Sio sana mkono umeteguka tu.."

"Hapana kwa kweli nampigia simu doctor.."

Alisema kweli akatoa simu na kumpigia doctor kabla simu haijapokelewa niliichukua na kuikata kisha nikampa simu yake na kuzungumza.

"Niko sawa mama we unaweza kwenda Swatii atanihudumia.."

Niliongea kwa upole ili swatii asihisi kitu, basi madam hakuwa na lakufanya zaidi ya kutoka, baada ya madam kuondoka niliweza kusikia sauti ya Nasra akiwa analia basi niliachana na uzungu nikanyoosha mkono kwa nguvu ukalia kaaa ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

Swatii akabaki haelewi, mie nikatoka zangu mbio mbio kumuwahi mtoto.

Kwa uwezo wa Allah siku hiyo ilipita na siku nyingine ikashika nafasi, siku hiyo nilikuwa na ufuaji wa nguvu maana mimi napenda kufua kwa mkono kuliko kutumia mashine

Nilikuwa na ufuaji wa nguo zangu na za mwanagu basi hao wengi wanatumia mashine, basi nilifanikiwa kumaliza mida ya saa tatu na muda huu Nasra wangu alikuwa bado kalala

Nasra ni mtoto mtulivu sana, yani hanaga makelele na hata sijui huko nje wanajua kama madam anamtoto maana Nasra huwa hasumbui.

Basi nilipomaliza kufua niliingia ndani ambapo nilimkuta madame akiwa anaongea na simu yani kwa namna alivyokuwa hatulii ilionyesha alikuwa akiongea na mtu ambaye alimpa taarifa za kufurahisha sana......

ITAENDELEA.......

Maoni

You're not logged in


Tangazo - For this week only
For this week only
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MIRANDA (Binti Yangu) 1 - - - - - 5



SEHEMU YA 1
ANZA NAYO SASA......

Kuna ule msemo kuwa mpende yule anaekupenda na mthamini yule anaekuthamini,yes naweza kusema kuwa mimi nilibahatika kupendwa na kuthaminiwa bwana ๐Ÿ˜Š

Yaani binti yenu kwenye kupendwa sijui niseme nilizaliwa na ka nyota flani hivi ka kupendwa๐Ÿ˜ , yani nilipozaliwa mama aliwahi kuniambia nilipokuwa mdogo nilikuwa napendwa jamani๐Ÿค—

Haipiti siku watoto kutoka nyumba za jirani wanajazana nyumbani ili kunibeba ๐Ÿ˜… kuna wale msioamini ila kuna wachache sana wataamini maana wao walikuwa kama mimi

Okay loves, tuachane na bla bla za hapa na pale kwanza twende na utambulisho rasmi sasa, unaweza kuniita Mira ikiwa ni kifupi cha jina langu, jina langu...

๐Ÿ‘‰ Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/miranda-binti-yangu-1-5

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi miranda-binti-yangu
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 6
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 6
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 7
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 7
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 8
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 8
MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13
MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13
MIRANDA (Binti Yangu)     SEHEMU YA 9
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 9
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 34 na 35

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 34 na 35

1.03K
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11

244
MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13

MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13

214
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10

211
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 28

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 28

198
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 30

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 30

158
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 29

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 29

152
ACHA NIKUPENDE โค๏ธ1

ACHA NIKUPENDE โค๏ธ1

145
Happy International Womenโ€™s Day from: Senator Kobokoโ€™s Wife, OSATO and Lady Jasmine

Happy International Womenโ€™s Day from: Senator Kobokoโ€™s Wife, OSATO and Lady Jasmine

10

ZIMESOMWA ZAIDI

โ€ŽTUNDA LA  DADA โ€Ž โ€ŽSEHEMU YA KWANZA

โ€ŽTUNDA LA DADA โ€Ž โ€ŽSEHEMU YA KWANZA

11.6K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.34K
๐Ÿ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA๐Ÿ”ฅ  sehemu ya tisa.  ๐Ÿ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...๐Ÿ‘‡

๐Ÿ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA๐Ÿ”ฅ sehemu ya tisa. ๐Ÿ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...๐Ÿ‘‡

3.78K
๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya sita.  ๐Ÿ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...๐Ÿ‘‡  Shemeji inauma utanichana.

๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya sita. ๐Ÿ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...๐Ÿ‘‡ Shemeji inauma utanichana.

3.27K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 119 na 120.

2.84K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 108

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 108

2.72K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya 20.  ๐Ÿ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...๐Ÿ‘‡

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya 20. ๐Ÿ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...๐Ÿ‘‡

2.66K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 116 na 117

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 116 na 117

2.6K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 106 na 107

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 106 na 107

2.59K
๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya 16.  ๐Ÿ‘‰ nakupenda pia...๐Ÿ‘‡

๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya 16. ๐Ÿ‘‰ nakupenda pia...๐Ÿ‘‡

2.54K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 30 Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 30
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media Asubuh sasa . Mama aliniamsha niajiandae anataka kunitoa out. Basi nikajiandaaa nikatoka zangu sebleni. Nakutana na mzeee alinikata jicho hilo. Nikaona aibu jana si kasikia...

MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13 Post Mpya
MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13
@majario LIVE

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 12 SONGA NAYO....... Basi safari ilikuwa ndefu kidogo, kwa mara ya kwanza toka nifike Oman hii siku ndio niliigia supermarket bwana, hiviii kumbe waarabu wana pesa hivi na...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 29 Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 29
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media Basi nimefika home nimenuna kweli kweli.nikaona yule adrian kama alikuwa anataka kunitia nuksi tu. Mtu kashanikaa mbele ya wazazi . Na yeye ndo kasababisha ata...

Happy International Womenโ€™s Day from: Senator Kobokoโ€™s Wife, OSATO and Lady Jasmine Post Mpya
Happy International Womenโ€™s Day from: Senator Kobokoโ€™s Wife, OSATO and Lady Jasmine
@majario LIVE

If you are Proud to be a woman: Share this post Meanwhile who is waiting for PART 5 of OSATO the Pure Water Seller? If you missed any part, Iink...

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11 Post Mpya
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11
@majario LIVE

SONGA NAYO... Pale nje tulibaki wawili tu mimi na madam hao wengine waliingia ndani. Madam aliponiita nilimuangalia tu bila kumuitikia, huyu mama nikimuona nahisi kichefuchefu kabisa "Mira achana na hizi nguo, kesho...

ACHA NIKUPENDE โค๏ธ1 Post Mpya
ACHA NIKUPENDE โค๏ธ1
@majario LIVE

MTUNZI uhuru media " Pink ujue hapa Ni mjini na maisha ni magumu Sana pesa zinapatikana kwa shida hivyo unatakiwa kujiongeza sio Ila siku Mimi ni nikeshe...

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10 Post Mpya
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10
@majario LIVE

SONGA NAYO..... Muda ulienda majira ya saa nane nilitoka nje kwa lengo la kuanua nguo za mtoto, lakini nilipofika nilikuta nguo zote ambazo nilifua na kuanika zikiwa chini Tena zilionekana kabisa kuna...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 28 Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 28
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media Basi kesho yake jioni sana ndo baraka alianza kujiandaa mana alikuwa anaondoka na basi la usiku. Nilijisikia unyongea sana. Ila alinambia nivumilie mana ni miezi...

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 34 na 35 Post Mpya
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 34 na 35
@majario LIVE

Basi demu akaondoka zake na hasira zake, na mimi nikaludi zangu ndani, kisha sasa nikampigia mama ahmed, na kweli akapokea skmu , nikasema hivi we mwanmke unanizoea sanaaa, ...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 26  na 27. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 26 na 27.
@majario LIVE

๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ๐ŸŒผ Mwandishi; lissa wa huru media Asa mimi ni nani nimnyimeee weeeee sio kweli. Nikamsogelea kisha nikamuangalia kwa jicho la kulegea sana. Akatabasamu kisha akanivuta zaidi. Akanipa mdomo. Tukaanza kukisss taratibu....

MIRANDA (Binti Yangu)     SEHEMU YA 9 Post Mpya
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 9
@majario LIVE

SONGA NAYO.... Kisha kwa ujasiri mkubwa nikazungumza. "Madam kwanza nasema asante kwa kuniamini lakini pia kwa kunijali nikuambie kitu siwezi kuolewa na kijana wako ile hali mimi ni mfanyakazi wako, sina thamani...

UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 6 Post Mpya
UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 6
@majario LIVE

ENDELEA....... "Jitahidi uwe na utu kuna maisha baada ya haya, kuna kupanda na kushuka. Kuishi na watu vizuri ni hadhina pia binti yangu. Nakupenda sana na najivunia wewe ila ubinafsi wako...

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 33 Post Mpya
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 33
@majario LIVE

Basi zena akawa nataka kuingia ndani ,mama ahamd akasema we zena sijuh ndo nani tulia nikupashe shoga angu, apa bwana hakuna, kama umebeba mimba ukazani una bwana hapa hakuna....

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 31 na 32 Post Mpya
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 31 na 32
@majario LIVE

๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ Khaaaaa mi nikamtumia sms, nikamwambia mm sipo nyumbani, naomba uondoke apoo, mambo yasiwe mengi, akaniuliza upo wapi saa 6 hii, nikamwambia nipo kazini akanmbia kazini ndo hupokei simu? Upo...

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL.   SEHEMU YA 15 Post Mpya
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL. SEHEMU YA 15
@majario LIVE

. ๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹๐Ÿฆ‹ Iris alipoingia ofisini, Mr. Marvel alikunja uso. Alijua Iris si mtu mzuri baada ya kile alichomfanyia Noela, lakini hakutaka kuonyesha kwamba anamjua vizuri. Akaamua kuwa mtulivu na kusubiri kusikia shida...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest