AFANDE MILLAN๐ Sehemu ya 31 na 32
Khaaaaa mi nikamtumia sms, nikamwambia mm sipo nyumbani, naomba uondoke apoo, mambo yasiwe mengi, akaniuliza upo wapi saa 6 hii, nikamwambia nipo kazini akanmbia kazini ndo hupokei simu? Upo kwa maraya zako si ndio, ahaaaa mi sikumjibu wala.nn, nikaweka.simu mfukoni nikawa nipo busy na club, kwani nimemuoa, na ndo mana mi nilikuwa sitaki kumleta kwangu kwa ajili ya hizi iissue ,we unaendaje kwa mtu bila ya taarifa, mi nikamkaushia nikawa busy na mambo yangu, club ilinoga kisenga ,luka sana na watoto wazuri, apo nishakamata demu, alafu unajua mambo ya club mule mule mnamalizana, basi bwana usiku wa saa 9 mm ndo naludi kwangu,,, tena hii siku nilichoka tu mapema, mi naludigi club alfajir kabisaaa
Aseeee iyo saa 9 usiku nafika home, nakuta zena kakaaa getini kajiinamia khaaaaa, uyu demu ana akiri vizuri kweli, yani usiku mzima kakaa peke yake ananingoja, nilimmind kinoma, asa anakaaje nje usiku mnene kama huu ,akibakwa jee, nilizani nilivyomwambia kuwa sipo, atakuwa amesharudi nyumbani ,et akakaaa apa apa, alivyoona gari yangu n yeye akasimama, mi nikashuka nikaenda kufungua geti wal sikuongea nae, kisha nikaludi kwenye gari, na nikajngiza gari ndani na yeye akaingia,nilivyoshuka, nikamuuliza we demu huna kwako, ni nn kilikuwa kimekuweka pale mpaka sa hizi saa 9 usiku, nyie zena akniuliza umetoka wapi uhuu usiku na unanuka pombe hivi, nikamwambia we demu unataka kubishana na mimi, mi si nakuuliza na wewe unanaiuliza, au sio tunabishana kwaiyo, zena aknmbia millan ,umetoka bar kunywa ?, na ulikuwa na wanawake uko eeh, nikamwambia yaaa nilikuwa bar na wanawake zangu unasemaje, ndo kilichokufanya ukae apo getini usiku huuuu
Zena akanmbia ni mtoto wako ndo ananipelekesha millan, mda wote najisikia kuwa na wewe na sio lengine, mda wote natamani kuwa karibu yako na sio chengine, alafu wewe unanaijibu kabisa kuwa umetoka bar na ulikuwa na wanawake zako kweli. Millan, nikasema zena, mimba isiwe sababu, we ni mtoto wa kike, uwezi kuja apa usiku na unakaa kwenye geti na wakati nishakwambia sipo, zena sitaki hizi drama mm, mwanzo na mwisho kuja nyumbani kwangu usiku na mwanzo na mwisho kuja kwangu bila ya ruksa full stop,naomba ulielewe hilo, zena akanambia ooohh kumbe sawa, baada ga apo sasa, mi nikaanza kuingia ndani na yeye akawa ananifata , kimya kimya, tumefika ndni tukaingia chumbani, mi nikaingia bafuni mana nimetoka kutimba uko kama wanawake 2 tofauti, nikapiga maji nilivyotoka, nikamkuta zena kakaa kitandani, mi sikutaka kuongea nae ,nikajilaza kitandani nikapumzika zangu ata kumgusa sikumgusa , asubuh saaa 2 , nikamshwa na zena, et mpenzi amka huendi kazini, nikawmabia leo niko off niache nipumzike akanmbia sawa, mi nikavuta shuka nikaendelea kupiga usingizi
Mh nikaja kuamka saa 4, zena wala hakuwa kitandani, mi nikaenda bafuni nikapiga maji, kisha nikapokea simu kutoka kwa mkubwa wangu wa kazin,alinipa maelekezo nikayapokea, na kisha nikayafakisha mahari husika kwa mda huo huo,kisha sasa ndo nikatoka ndani, mh nakuta nyumba safi kwrli kweli, nikjua binti kujitima uyooo kashafanya usafi, basi zena alivyoniona akanikalibisha mezani kw afurahaa mnoo, alikuwa kashaniandalia chai, na chapati, na maandazi, basi nikakalibia na akanitengea vizuri kisha akanikalibisha waoow ,nikakaaa nikawa nakunywa chai, dooh basi zena akanmbia millan samahani kwa jana sitaludia kuja usiku kama ule, ila nilikumiss sana ndo mana ,na mimba ndo inanisukuma, nikikuona wewe ndo. Nalata amano
Nikasema.sawa zena yameisha but sio sawa ,unakujaje usiku kama.ule nanakwambia sipo bado unaendelea kuningoja ,sio sawa na umekosea mpenzi, akanmbia sawa basi nisamehe,nikasema sawa yameisha ummy umemuacha na nani, akanambia nimempeleka kwa shey leo yuko off, nikasema sawa malaiza kula ujiandae nikuludishe kwako ukamuangalie mtoto, zena akasema lakini mm nimekumiss nilikuwa nataka kukaa kwako ata siku 2, doooh kwangu akae siku mbili kufanya nn sio kweli, nikasema no nna kazi nyingi sana hii week, natakiw kufanya so ntakuwa busy sana ,so lazkma nikupeleke kwako, akanmbia lakini ata kama.ukiw abusy ni sawa ,mi sitakuzuia kwenda kazini, we nenda mimi ntabaki apa mpenzi, na usiku ukiludi tunaonana,nikasema no zena nimesema kula nikuludishe kwako, mimi ni mwanaume na nnapoongea na omba nisikilizwe full stop, basi zena kiunyonge akasema sawa ,kisha tukaw tunaendelea kula ila sasa zena akawa anakula kwa unyonge, ahaa mi kwangu bwana nakuachaje , na wakati nna wanawake kibao wanakujaga apao wakimmkuta si kitanukaa
Basi sasa tukiwa tunaendelea na kula, nikasikia mlango wangu wa kuingilia ndani,yani sebleni , unagongwa kwa nguvu mnoooo ,nyieeee mi nikajua kumekucha ,zena akaniukiza nani aangonga mlango hivyo, nikasema itakuwa wakusanya pesa za ulinzi na taka.,ngoja nikawaone, basi nikasimama nikaenda kufungua mlngo do si alikuwa mama ahmad, aseee nikamzuia uku uku njee, nikamuuliz mama ahmad shida nn, mbona unakuja kwangu bila ya taarifa, mama ahmad akanmbia wacha weee leo unanizuia kwa njeee mana maraya wako yupo ndani bila ya shakaaa,nakujua sana wewe , sasa sikia nataka kumuona kwanza uyooo asiekujua wwe vizur na akauvaa mkenge kama sie, nikasema mama ahamad ntakupiga nazani unanijua naomba sasa hivi usepe, akanmbia sawa nimefata pesa ya kula ya mtoto , ya jana na leo, na alafu nilikumiss ila kwa kuwa ndani una mwanamke mwengine hakuna shidaaa, mi naondokaa nipe pesa ,nikamungali uyu demu alivyo na matatizo yani usipotuma pesa ya mtoto siku moja, knakuwa tatizo ila sikutak zena ahisi kitu chochote jui ya iwepo wa mama ahamed nikaona nimalizane nae tu ,nikachomoa pesa nikampa mama ahmad nikamwmabia aya nendaa, aseee nikiwa naongea na mama ahmed zena si akafungua mlango kisha akatoka njeeee doooh
Mama ahmad akasema oooh kumbe ndani umekamata bonge la demu leo, ahaa leo umejua kuchagua mana mda mwengine unabebaga mpaka marehemu wanaotembea alooooooo, mi uyu mwanamke nilibug ,mtoto wa uswahilini anaongea uyu alafu mgomvi kinoma, zena akasema baby mbona sielewi ni nn kinaendelea, nikasema zena nenda ndani uyu anakusanya pesa za ulinzi we ningoje ndani, mama ahmad akasema weeee nani anakusanya pesa ya ulinzi, we mwanaume unachanganikiwaa, oohhhhh kumbe sababu ushamtia mimba na uyu, alooooooo, apo sasa zena alikuwa na mimba ya miezi 3 na ishaanza kuchomoza ,zena akanmbia millan mbona sielewi baba, nikafoka nikasema.zena nimesema nenda ndani, mh
๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ๐ฆ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni