VYOTE NDANI GONGA94
NILIZAA NA BOSI KWA BAHATI MBAYA SEHEMU YA 03
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nilishtuka ghafla.
Nilikuwa nimelala juu ya kitanda kikubwa, cheupe, chenye harufu ya manukato ya kiume. Pazia la dirisha lilikuwa likiruhusu mwanga wa asubuhi uingie taratibu, na saa ya ukutani ilionyesha saa kumi na moja alfajiri.
Moyo wangu ulianza kupiga kwa kasi.
"Nimefikaje hapa?"
"Hii siyo ofisi."
"Hiki ni kitanda cha nani?"
Nilijaribu kukumbuka. Kichwa kilikuwa kizito, mwili umechoka lakini hakuna maumivu.
Niliangalia nguo zangu nilikuwa bado nimevaa vizuri, japokuwa suti ilikuwa imelegea kidogo kana kwamba nililala nayo.
Nilinyanyuka taratibu, nikakaa kitandani huku nikishika kichwa changu.
Ndipo mlango ukafunguliwa.
Aliingia bosi wangu Mr. Adrian.
Alikuwa amevaa shati jeupe, mikono imekunjwa, uso wake ulikuwa mtulivu sana kuliko nilivyomzoea.
“Umeamka?” aliuliza kwa sauti ya upole.
Nilimeza mate.
“Bosi… nipo wapi?” niliuliza kwa sauti ndogo.
Alikaa kwenye kiti karibu na kitanda, hakunisogelea sana kana kwamba anaheshimu mipaka.
“Hapa upo nyumbani kwangu , Jana ulisinzia ghafla, usingeweza kuendelea na kazi wala kuondoka peke yako.”
Nilifumba macho kwa sekunde chache nikivuta pumzi ndefu.
“Naomba unisamehe bosi… sikukusudia.”
Alicheka kidogo.
“Usijilaumu. Ulichoka. Nilikuleta kwangu upumzike.”
Nilihisi. Aibu, maana toka nizaliwe sijawahi lala kwa mwanaume hata kuwa karibu na hao viumbe .....
Nilimtzama na kumuuliza bosi ......
“Nililala muda gani?” nikauliza.
“Karibu masaa manne. Nilikubeba na kukuleta hapa i, nikakuhakikisha uko sawa.”
Nilimtazama machoni.
Kulikuwa na kitu kipya pale… si macho ya bosi tu, bali macho ya mwanaume.
Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa.
“Radhia…” aliniita kwa sauti ya chini, “kile kilichotokea jana… hakitakiwi kutokea tena.”
Nilitikisa kichwa haraka.
“Ndiyo bosi. Ni kazi tu.”
Niliinuka nikiwa na wenge wenge tu na kuyumba yumba ,nilitaka kuanguka ghfla bosi alinirukia kitandani tukaagukia ,macho yetu yakitazamana ,jamani nilikuwa naona aibu maana sio kwa jicho lile la bosi
Bosi alikuwa akitabasamu huku akiyatazama madimpozi yangu akawa anayashika na kuzipanga nywele zangu ...Jamani nilisikia raha sana
Bosi akanitazama na kutaka kusema kitu kabla hajasema mara ghafla
ITAENDELEA......
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nilizaa-na-bosi-kwa-bahati-mbaya-sehemu-ya