VYOTE NDANI GONGA94
NILIZAA NA BOSI KWA BAHATI MBAYA SEHEMU YA 04
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
TULIPOISHIA .......
Bosi alikuwa anataka kusema kitu.
Niliona midomo yake ikifunguka taratibu, macho yake yakinitazama kwa umakini wa ajabu, kana kwamba alikuwa anapima uzito wa neno alilotaka kulitamka.
Lakini kabla hajazungumza
ANZA NAYO SASA......
GHAFLA
Simu yake Ikaanza kuita ...
Sauti ile ilikatiza kila kitu.
Alishtuka kama mtu aliyerudishwa ghafla duniani. Akavuta mkono wake haraka, akasimama, na kuchukua simu ile huku akigeuka pembeni.
“Hello?” alisema kwa sauti iliyobadilika kabisa, sauti ya bosi niliyoizoea.
Mimi nilikaa pale kitandani, moyo wangu ukipiga kwa nguvu.
Nilikuwa najilaumu, na wakati huohuo nikishindwa kuelewa nilichokuwa nakihisi.
Ni hofu?
Ni aibu?
Au ni kitu kingine ambacho sikuwahi kukijua tangu nizaliwe?
Baada ya dakika chache, alimaliza kuongea na simu.
Aligeuka kunitazama, macho yake sasa yakiwa mazito, yenye tafakari.
“Radhia… nadhani sasa jiandae twende kazini,Na kuhusu nguo fungua kabati luna nguo zipo humo..”
Nilitikisa kichwa, nikakubaliana kimya kimya.
Lakini swali nikajiuliza hizi nguo ni za nani na kaniambia yeye ni bachelor .
Yaani yuko single kama upanga ,sasa nguo hizi za nani ? Nilijiuliza na sikupata jibu nilichokufanya ni kwenda kabati na kufungua.
Nilikodoa macho nguo zilikuwa nzuri sana,zilikuwa rangi ya blue na viatu vyake yaani mpaka kipocho Kwangu nilijuwa nikivaa hizi ni BLUE DAY .yaani kama kamis fulani ukichukulia na huu wembamba wangu.....
Niliingia bafuni nikaoga harka nikarudi nikavaa lakini kilichokuwa kinanishinda ni kufunga zipu ya mgongoni nilikuwa na hangaika sana, mara gjafla nilishangaa nimeshikwa kiuno .Sio siri nilishtuka " Agggh"
Kisha nikawanafungea zipu huku bosi akiniambia sikioni' vitu vingine uwezi kufanya pekee yako omba msaada".Nilitulia maana kashika kiuno na kimeshikika .Baada ya hapo alinambia geuka ...
Niligeuka mtoto wa watu kwa mapozi kama miss dunia na kutabasama akasema " konyeza kidogo" nikafanya hivyo eti akawa anacheka na kuniambia maneno ambayo yalfanya kichwa kuongezeka ukubwa
" You look so beautiful Radhia ,kuna wanawake wazuri halafu kuna wewe" Nilitabasamu na kumshukuru na kisha nikamwambia
" Tuwazi tusije tukachelewa "
Nilitoka huku kanishika mkono alinifungulia mlango wa gari kama malkia ......Na tukaelekea ofisini ....
Humo kwenye gari ni mwendo wa kutazamana kila mtu anachekea upande wake .mwishowe nilimwambia
" Jamani bosi acha kuniangalia "
" Kwanini niache sasa?
' Na loose control mwenzako"
" Haya sawa"
Yaani nimetoka kumwambia hapo hapo bado ananitazama ila huyu bosi jamani sijuwi ana nini?
Nilifika kazini nje ya jengo kulikuwa kuna wafanyakazi wengi ,sasa kimbembe kwenye kushuka na nilivyopendeza mmmmmh maana watu wengi wanajua maisha yangu kuwa sina uwezo wa kuvaa vile .Adrian alishuka haraka na watu wakawa wanamsalimia hakuwajibu alikuja upande wangu na kunifungulia mlango ...
Sasa hapa ndo kaongeza ugumu wa mimi kushuka alisema kwa sauti lazima shuka ujuwe nachelewa kikao.Nilimwambia sawa nashuka nilianza kutoa mguu kisha nikashuka .Na nilikutana na macho ya wafanya kazi wezangu.
Macho yote yalinitazama mpaka nikajikuta aibu na wasiwasi vinanizidi lila mtu alitazama na kuangalia pembeni .Bossi aliniambia
" Kaa na aibu zako kama zitakufikisha popote"
" Mbona sina aibu jamani "
" Una uhakika ?
"Ndiyo ,nina uhakika"
Akanivuta mkono na kunisogeza kifuani kwake .Niliogopa ......nikawa nahema huku namtazama .
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nilizaa-na-bosi-kwa-bahati-mbaya-sehemu-ya